Makamu wa Rais, Samia Suluhu akutana na Mkuu wa Kanisa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo

Makamu wa Rais, Samia Suluhu akutana na Mkuu wa Kanisa KKKT, Dkt. Fredrick Shoo

Maoni ya askofu shoo wa kaskazini akimpa ushauri askofu mteule Laizer wa kutoka kaskazini pia huku akinukuu maneno ya Mwanasiasa Nyerere badala ya maneno ya Mungu yaliyoko kwenye Biblia.Askofu Shoo joho lake avae tu gwanda la chadema juu avae hilo kofia la uaskofu itapendeza zaidi
Wafia Dini ya Poleni sana ungana na Ustadh mwezako Barabosa

Naona rangi halisi za maustadh humu

Pole Ustadh Yehodaya

Mmejaa udini Ustadh Yehodaya naona Mama Leo kaenda kanisani kuweka mambo sawa mneumia sana

Lengo lenu serikali isishirikiane na KKKT mmekwama
 
Kuna mtu kanitonya kitu hivi hiyo dayosisi eneo la mpanda ni sehemu ya hiyo dayosisi ya askofu mteule Laizer?
Ustadh Yehodaya naona udini na chuki zinawasumbua sana, Sakata hili maustadh Wafia Dini Kama wewe na Barbarosa mmeshindwa kuvumilia

Mlisubiri vita ya serikali na KKKT sasa mnatokwa povu
 
Wewe sijui hata huwa unaandika nini,pumbapumba tupu!

Sasa hapa ndio umeandika uzwazwa gani?

Wapiga debe wa CCM awamu hii ni kinyaa kitupu!
Chizi huyo. Tunamjua vizuri wala hatusumbui. He is a deranged irrational CCM zealot and a "yes-man" with a severe slavery mentality but without a single ounce of rational critical thought. Mpotezee tu mkuu. Hiyo ndiyo dawa yake.
 
Ogopa sana watu aina hii!
images
Magfully type...
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Hayo mamlaka unaelewa ni yapi?
Na je serikali ni mamlaka?
 
Huyu Mama commands respect from the public. Anaonekana ni mwenye hekima, siyo mtu wa kuzua taharuki, siyo mropokaji, ametulia akilini na moyoni. Na sijawahi kuwasikia watu wakimsema kwa lolote baya, iwe kwa wale wa wakereketwa wa CCM au wafurukutwa wa upinzani au wale wasioegemea kokote.

Tanzania would be better with her.
hebu fumba macho uvute kumbukumbu ni makamu yupi wa rais uliwahi kusikia akisemwa kwa baya? kama hayupo basi ni nature ya nafasi sio mtu. yule ndie mshauri mkuu wa rais ukute pengine 40% yanayofanywa na rais ni ushauri wake.
 
Umeumia sana ustadhi Barbarosa , Mama samia kukutana na Askofu

Pole sana ustadhi Barbarosa ndio maisha hayo, Ustadhi Umeumia sana umetanguliza chuki, uchama na Dini yako ndio inakusumbua sana
Hivi Barbarosa si kabinti? Mbona unamuita Ustadhi?
 
Kamanda Shoo amenukuu maneno ya Mwl NYERERE....utofauti wa kamanda Shoo na Lema haupo
 
Hongera sana Baba Askofu Dr Shoo ujumbe wako kwa Baba Askofu Dr Laizer umesheheni na kubeba ujumbe mzito sana.
 
Niulize tu, Mama Samia amejituma kwenda Tabora kukutana na Baba Askofu? Mama Samia alijichagua kuwa Makamu wa JPM? Kama jibu ni hapana, ametumwa na JPM, alipendekezwa na JPM, sasa mwenye busara zaidini nani? Naamini hata huo mwaliko ulipelekwa Kwa Rais!Ninachoona mimi ukubwa in jalala! Makosa yoteya Govt lazima abebeshwe JPM! OK. Ikatokea ilivyotokea wamekaa ikaonwa who is neutral ,aende Kwa ajili ya utangamano wa nchi hata JPM ana busara sana ila kwa vile watu tumeguswa tu kwa mengi! Lakini Kwa mstakbali mwema was Taifa, tumtakie meme!
kama yey jpm ndiye mkubwa na anashindwa kuyakemea unataka nani sasa abebeshwe hayo makoma
 
Huyu Mama commands respect from the public. Anaonekana ni mwenye hekima, siyo mtu wa kuzua taharuki, siyo mropokaji, ametulia akilini na moyoni. Na sijawahi kuwasikia watu wakimsema kwa lolote baya, iwe kwa wale wa wakereketwa wa CCM au wafurukutwa wa upinzani au wale wasioegemea kokote.

Tanzania would be better with her.
if they give a chance to run for presdency
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Unapotosha.
Hilo neno limeandikwa wapi kama sio kwanye vitabu vya dini?
Kwa nini mnatumia hilo andiko moja tu wakati mengine kama haki ,hekima, na kumtii Mungu mnayakwepa?

Vitabu vya dini vimeelekeza kutendea wengine kama ambavyo kila mtu angependa yeye atendewe.
Je, mnatenda mema kwa wenzenu kama ambavyo mngependa nanyi siku mkiwa nje ya madaraka mngetaka mtendewe?

Kutii Mamlaka ni neno pana sana.
Mamlaka zimewekwa kwa misingi ya katiba sio misingi ya vitabu vya dini! Kila MTU anapaswa kuheshimu na kuilinda katiba. Mamlaka zina na dola na katiba yake.
Kutii mamlaka ni kulinda ,kuitetea na kuheshimu katiba.
Kufichua uhalifu wa kuvunja sheria na katiba ni kuitii mamlaka mana ndivyo serikali inavyoelekeza kuwa watu wafichue uhalifu.
Uhalifu ni pamoja na ule unaotokea kutokana na watendaji wa serikali kuwa waovu.

Kutii mamlaka ni kufuata sheria zilizowekwa na mamlaka . Zipo sheria nyingi. Sheria za ndoa,sheria za ardhi ,sheria za usalama barabarani, sheria za biashara,sheria za vyama vya siasa,sheria za uchaguzi, sheria za mambo ya nje, sheria za uhamiaji, sheria za mambo ya anga,sheria za mambo ya fedha sheria za utumishi wa umma. n.k. Mtu yeyote anayetii mamlaka anafuta sheria hizo na kuzitii.

Viongozi wa dini na waumini wao duniani kote wanatii sheria zinazowekwa na mamlaka.

Sasa nikuulize swali:
(1).Watu kupotea na kutekwa ni sheria zilizowekwa na mamlaka ili kwamba MTU akipinga utekwaji aambiwe kuwa hajatii mamlaka?

(2) Je,Mkurugenzi kuvuruga uchaguzi ni sheria zilizowekwa na mamlaka ili watu wore watii na kuheshimu hiyo hali wasije wakatenda dhambi ya kutoitii mamlaka?

(3)Je, watu kukatana mapanga wakati wa uchaguzi ni utaratibu uliowekwa na mamlaka ili watu wote wakae kimya wasiseme wasije wakaingia katika dhambi ya kutoitii mamlaka.

Bila shaka wasiotii mamlaka ni wale wasiotii sheria na katiba ya nchi. Mtu yeyote anayevunja sheria kwa maana yoyote ya ama kujinufaisha kisiasa au kimadaraka huyo ameshindwa kuitii mamlaka.

Na mtu yeyote anayetenda dhambi ya kutoitii mamlaka anakemewa na viongozi wa dini kama ilivyokuwa kwa Mussa kupambana na Faraoh ,Samweli Kumkemea Mfalme Daudi. Yesu kumkemea mfalme Herode na Pia Yohana kumkemea Mfalme Herode hadi kuuawa.

Imetokea kwa muda sasa watu wanavunja sheria na kushindwa kutii Mamlaka kwa kisingizio cha kusema yule hajatii mamlaka asulubiwe na hata kutoa maneno machafu bila kujua kuwa mamlaka ina vyombo vyake vya ulinzi vilivyosomea kwa kiwango cha juu kabisa ,vinapaswa kuachiwa majukumu yake ya kujua nani hajatii na nani ametoa maoni na nani amekemea kama wajibu wa mwananchi na raia mwema.
 
Labda kama Kanisa la Muzungu lkn siyo KKKT, usichanganye Kanisa la Muzungu na Kanisa la Mwafrika, KKKT ni Kanisa la TZ na kila kitu kinaishia hapo acheni kujidanganya!
Hata uovu kwa sababu ni mamlaka inafanya kanisa litii? Uwe unafikiri kabla ya kuchangia.
Tutajua nani sikio nani kichwa..twendeni tu..leo wanatumiwa na wanasiasa..kesho watatumiwa na mataifa makubwa dhidi ya serikali..sio jambo la kupuuza..hawatakiwi hata kuchekewa hao waendekeza matumbo.
Kwa nini awamu hii inajikita sana kwenye kusingizia watu kuwa wanatumiwa na watu wa nje.
Hivi hamuoni kuwa mnadhalilisha nchi na vyombo vyake vya dola?

Hivi nchi hii nani asiyelipenda taifa hili ambalo shangazi,mama,baba,wajomba na n.k wote wamo humu humu.
Nchi ambayo tangu Enzi za mkoloni watu waliishi kwa amani na kuka pamoja. Hata Uhuru wa nchi hii haukupatikana kwa kumwaga damu pamoja na kwamba wakoloni walinyanganywa Mali zao lakini hakuna damu zilizomwagwa. Iweje Leo watu wanaokosoana tens kwa hoja zenye mashiko wahofiwe kutumika kuchafua amani.

Ninachoona ni hofu ya kushindwa kwenye uchaguzi kwa baadhi ya watu. Hofu ya kukaa benchi ni mbaya sana na ilianza tangu wakati mwalimu anangatuka.
Walimpamba kuwa ukiondoka amani itatoweka lakini hawakumaanisha hivyo Bali amani ya matumbo yao kukosa ulaji.

Nchi yenye jeshi imara kabisa na lenye ni dhamu kubwa kabisa duniani kuwa na viongozi wanaoogopa maaskofu walioshika fimbo zao za kiibada ni aibu kubwa. Eti wanataka kupoteza amani. Hivi mnafikiri amani ya nchi hii imeanza Leo au Jana.

Ni nani anaweza kujigamba kuwa aliikuta hii nchi ikiwa na vurugu halafu yeye na chama chake akaituliza?

Niliwahi kusimuliwa na bibi yangu kuwa wamisionari walipokuja walifanya kazi kubwa ya kuzuia vita za kikabila.
Makabila na machifu wao walikua na tabia ya kuvamia makabila mengine na kupora Mali na wanawake.Lakini wamisionari walikomesha Bali hii na kusema Mara kwa Mara vita imekwisha.

Tuache dhana mbovu na dhaifu ya kutangazia wananchi kuwa kuna watu wanataka kumwaga damu wakati watanzania wanapendana kweli kweli wabaya ni wale wenye hofu ya kupoteza madaraka bila kujua kuwa kupoteza madaraka kwenye sanduku la kura ni jambo linalowezekana na lipo kisheria.


Wakati wa awamu ya 3 na 4 ambayo ukaribu wa watawala wetu na watu wa nje ulikua mkubwa sana lakini ndizo awamu zilizokuwa na kupingana kukali sana kwa hoja, maandamano mengine,migomo mingi na vyombo vya habari kushambulia serikali Lakini hapakuwa.Awamu hii ambayo hayo hayapo lakini baadhi ya watu wanahofu isiyo na tija zaidi ya kufilisika kisiasa na kujaza watu hofu.

Vyombo vyetu vya dola vinatosha na vinaweza kuilinda amani ya nchi vikiachwa vifanye majukumu yao bila wanaeiasa kuingiza maneno ya kujenga hofu kwa wananchi.
 
Hao maaskofu wanasiasa kuna namna ya kushughulika nao..kanisa haliizidi serikali maana hata andiko limetoa maelekezo kwa waamini kutii mamlaka sio mamlaka kunyenyekea kanisa..
Huelewi ulichoandika!
 
Bas
Labda kama Kanisa la Muzungu lkn siyo KKKT, usichanganye Kanisa la Muzungu na Kanisa la Mwafrika, KKKT ni Kanisa la TZ na kila kitu kinaishia hapo acheni kujidanganya!
Basi, endeleeni na mchakato wa kuliadabisha KKKT!
 
Kamwambia asitawaliwe na kiburi cha madaraka
 
Back
Top Bottom