Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Makamu wa Rais, Samia Suluhu amtembelea Tundu Lissu hospitalini Nairobi

Alienda Nairobi kwenye ziara yake akaona aibu ikabidi apitie.

WATANZANIA SIO WAJINGA.
 
Kwa kawaida jasiri haachi asili atakuwa jasiri tu.

Nakumbuka mama Samia akiwa makamu wa Rais wa JMT ndio kiongozi pekee wa juu katika mihimili yote mitatu aliyekuwa na ujasiri/ uthubutu wa kwenda kumjulia hali mhanga wa shambulio la risasi mbunge Tundu Lisu pale Nairobi hospital

Huyu mama ambaye sasa ndio Rais wa JMT ni jasiri.

Tunakumbushana tu.

Maendeleo hayana vyama!
Yupo na mwingine ambaye alikuwa balozi lakini baada ya kumsalimia Lissu alirejeshwa nyumbani.
 
sami1sd-660x400.jpg

Historia huwa inatukumbusha matukio ya watu wenye moyo wa utu , mtu huyo alipokuwa katikati ya pori la wanyama wakali na wenye uwezo wa kukuangamiza.

Hilo tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu liliwashitua hata wana CCM.
 
Mama Mungu akubariki kwa kwenda kumwona Lisu. Tunakuombea Mungu akupe hekima. Tupo pamoja nawe. Ninaomba tumsaport mama kwenye mitandao. Kumbuka si vizuri kumsema mama vibaya.
 
Mungu hulipa na kuenzi wema wa mtu.
Mungu, The Omnipotent, Muweza wa yote, katuonyesha kitu katika uhai wetu, tutakacho wahadithia vizazi na vizazi vijavyo.

Lissu, mtu mwenye kukosoa kwa maneno makali alimchukiza Mfalme.
Mfalme alikasirika sana na kuna walioamua kumlipizia kisasi kwa niaba yake.

Wauaji walimmiminia Lissu risasi nyingi sana, lakini Mungu alikataa kumuondoa duniani.
Ingawaje aliumia sana lakini akaendelea kupata nafuu na kupona.

Mfalme alikataa kufanya ucgunguzi wowote juu ya jaribio la kumuua Lissu.

Lakini Mungu ni wa ajabu sana.
Miaka kadhaa ilipita, huku Mfalme akilindwa sana na askari hatari waliosheheni silaha nzito nzito zenye uwezo wa kuangamiza hata wale wenye fikra ya kumdhuru Mfalme.

Watu wakashangaa, sijui adui alipita wapi.
Akamkaba mfalme vibaya mno hadi walinzi wake na wananchi wasijue la kufanya.
Na adui alimkaba Mfalme hadi kumtoa roho.

Maajabu aliyemiminiwa risasi nyiiingi, yu hai.

Kweli Mungu ni wa ajabu.

Warumi 12:19-21
Kisasi ni juu yangu mimi; anena Bwana.
 
Katika hali ya kawaida huwa namuona Mama Samia kama anasifa nyingi sana za kuwa ni Top Tz maana hakuna sehemu anayopwaya ikifika kutumia busara. Nategemea kumuona 2020 akitupigania baada ya kuongozwa na mzalendo wa kweli JPm.
😆😆😆
 
Back
Top Bottom