Mungu hulipa na kuenzi wema wa mtu.
Mungu, The Omnipotent, Muweza wa yote, katuonyesha kitu katika uhai wetu, tutakacho wahadithia vizazi na vizazi vijavyo.
Lissu, mtu mwenye kukosoa kwa maneno makali alimchukiza Mfalme.
Mfalme alikasirika sana na kuna walioamua kumlipizia kisasi kwa niaba yake.
Wauaji walimmiminia Lissu risasi nyingi sana, lakini Mungu alikataa kumuondoa duniani.
Ingawaje aliumia sana lakini akaendelea kupata nafuu na kupona.
Mfalme alikataa kufanya ucgunguzi wowote juu ya jaribio la kumuua Lissu.
Lakini Mungu ni wa ajabu sana.
Miaka kadhaa ilipita, huku Mfalme akilindwa sana na askari hatari waliosheheni silaha nzito nzito zenye uwezo wa kuangamiza hata wale wenye fikra ya kumdhuru Mfalme.
Watu wakashangaa, sijui adui alipita wapi.
Akamkaba mfalme vibaya mno hadi walinzi wake na wananchi wasijue la kufanya.
Na adui alimkaba Mfalme hadi kumtoa roho.
Maajabu aliyemiminiwa risasi nyiiingi, yu hai.
Kweli Mungu ni wa ajabu.
Warumi 12:19-21
Kisasi ni juu yangu mimi; anena Bwana.