Makanisa Nchini Mjitafakari

Makanisa Nchini Mjitafakari

Daaah Binadamu Mtakatifu Unajikosesha Baraka kwa Kutokutoa Sadaka kwa Hao Wa Kanisani!?

Mungu amekuuumba Kwamba usipompa Anakunyima Baraka! Yaani Mungu amekuumba Amekupa Uwezo wa kutengeza Pesa ila Ukimnyima hizo Pesa Anakunyima Baraka

Ungejiuliza kwanza Hata Washenzi..Wezi..Majambazi..malaya..Mafisadi.. Wachoyo wamepewa Baraka za Kuishi vizuri hapa Duniani kuliko wale ambao Hawafanyi madhambi hayo

Mungu amekuwekea Akili Hapo Ulipo baraka zako utazipata Ukitumia akili zako vizuri kutafuta Vitu. Hao wanaoiba ..wanafanya ufisadi .. wanaofanya uzinzi.. wote wanamtegemea Mungu ila Wanachokosa ni Kumtii Mungu basi
Mimi hua natoa sana
 
Ngoja Nikuambie Kitu kimoja Ndugu yangu. Ulishajiuliza kwanini Kuna Mirundikano ya Michango ila Ina Badilika Majina Tu. Leo Sadaka.. Kesho Zaka. Kesho kutwa Harambee..Mwakani hiki na hiki n.k Ni njia ya Kukupumbaza Ili uone Mungu ndio anataka Kumbe Sivyo

Mungu hakuchukii usipotoa sadaka wala Zaka. Mungu hachukii Mtu Yeyote yule ni Wewe na Akili yako Keshakuumba . Hana Haja ya Kuhitaji Chochote kile angehitaji hayo Asingekuwa Mkamilifu Huyo Mungu maana Anahitaji vitu kutoka Kwako ili Akamilike.
Kujiwekea Hazina isiyo haribika mbinguni ni kuwa mtoaji hapa duniani sisemei kanisani tu ila hata kwa wajane maskini na wasio jiweza ni bora kila mtu akabaki na imani ambayo anaamini itamponya...
 
Kujiwekea Hazina isiyo haribika mbinguni ni kuwa mtoaji hapa duniani sisemei kanisani tu ila hata kwa wajane maskini na wasio jiweza ni bora kila mtu akabaki na imani ambayo anaamini itamponya...

Wape Hao uliosema Hapo utakuwa Unafanya Jambo Bora Na La Kibinadamu zaidi ila Usifanye kwa kisingizio unampa Mungu. Sema Tu nimempa Mjane.. Yatima hivyo Ndivyo Mungu katuumba Tujisaidie sisi Kwa Sisi Yeye haitaji Hayo.

Muombe Mungu Majala Naye Atakujalia Majala hayo
 
Hivi humu wapo wachungaji, itabidi tuwaunge humu kwa nguvu wapate ufunuo
 
Tafuta saccos ujiunge maana naona unataka makanisa yaanze kufanya majukumu ya saccos.

Kanisa ni kanisa na saccos ni saccos.

Jitahidi kuheshimu nyumba ya Ibada.
 
Tafuta saccos ujiunge maana naona unataka makanisa yaanze kufanya majukumu ya saccos.

Kanisa ni kanisa na saccos ni saccos.

Jitahidi kuheshimu nyumba ya Ibada.
Inaonyesha kiasi gani hujapata ukweli. Soma tena mada. Utaendelea kunyonywa halafu kizazi chako kitakuja kuona huyu mzee Alipotoka maana tunakoelekea Hakuna atakayeyaamini hayo makanisa
 
Sasa kwa mfano Mimi ni mmakonde nalaaniwa na mzimu wa shimo la mungu au Mungu wa wa Ebrania?
Huo umakonde wako hauta jalisha kitu kwa MUNGU wakweli Aishiee pia laana inatoka kwa aliye ijua kweli ila akaamuua kuendelea na mizimu yake
 
Huo umakonde wako hauta jalisha kitu kwa MUNGU wakweli Aishiee pia laana inatoka kwa aliye ijua kweli ila akaamuua kuendelea na mizimu yake
Swala la unamuabudu nani na kwa namna gani halipo wazi hata kwenye kitabu Chako Cha dini, Kuna uhuru mkubwa wa kuchagua utakachotambua kama ukweli kwa mtazamo wako, mf Kuna kristo zaidi ya mmoja kwenye kitabu Chako Cha dini Ila wewe na wenzako mnamtambua Yesu ndio Kristo pekee
 
Huo umakonde wako hauta jalisha kitu kwa MUNGU wakweli Aishiee pia laana inatoka kwa aliye ijua kweli ila akaamuua kuendelea na mizimu yake
Kwani Hao wanaoitwa Watakatifu huko Makanisani si Mizimu!? Mpaka Muone Wengine wanaendelea na Mizimu Wakati hata huko makanisani Wapo Pia
 
Usichojua wasomi ndio wamejazana huko kwenye makani ya manabii na waganga.

Imeandikwa watakula madhabahuni
“Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili" 1 Wakorintho 9:14
sema hawa jamaa siku hiz wengi hawaubiri injili bali wamekuwa motivational speaker na wafanya biashara
 
Usichojua wasomi ndio wamejazana huko kwenye makani ya manabii na waganga.

Hivi na Wewe unawaona Wasomi wa Tanzania ni Wasomi kweli kweli. Na Elimu hii hii ya Wakoloni!?

Imeandikwa watakula madhabahuni
“Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili" 1 Wakorintho 9:14
sema hawa jamaa siku hiz wengi hawaubiri injili bali wamekuwa motivational speaker na wafanya biashara

Hayo ni Maneno ya Wanadamu wanaopiga Michongo kwenye Biblia ila Msije kuwahukumu Huko mbeleni wakimsingizia Mungu kwamba Kawaambia Wale Madhabahuni
 
Hapa ndipo mnapochanganya kanisa sio jengo, kanisa ni wewe, mtume Paulo anasema hamjui ya kuwa mwili ni hekalu la roho mtakatifu?? Ok Labda unazungumzia madhehebu, dhehebu ni kusanyiko la hiari mahali fulani kwa ajili ya kumuabudu Mungu, kumbuka lengo kuu ni kumuabudu Mungu, ndio hapo Yesu anasema watakapokusanyika wawili au watatu na Mimi niko kati yao, na Katika ibada yoyote sadaka ni lazima. Na Mungu alishatoa utaratibu wa matumizi ya sadaka itakayotolewa mahali ambapo waliokusanyika ni Kwa ajili yake, kwamba sadaka itatumiwa na walawi, wajane pamoja na Yatima. Sadaka ina mambo matatu:

1. Imani, sadaka inaambatana na Imani ya mtoaji
2. Hiari, sadaka ni hiari Kwa kadri Mungu alivyombarikia mtu
3. Moyo wa kupenda

Ukitoa sadaka kwa utaratibu huo hautamuuliza mchungaji wako sadaka yanguu imetumika wapi kwakuwa ulimpa Mungu ukiona Kuna ukakasi muulize Mungu. Michango hiyo inapaswa kuulizwa kwa sababu mchango sio sadaka, mmeona jengo letu halijakaa sawa basi mnapitisha mchango Kwa ajili ya Hilo jengo matumizi yake lazima mhoji.

Ukiona mtu amekomaa ooh sadaka zinaliwa ooh zinaliwa ndio wale hata kutoa huwaoni matajiri huwa hawapigi kelele kwasababu wanajua maana ya sadaka. Mtu anaenda Kwa mganga anadaiwa kuku anatoa na kuku anachinjwa mbele yake hasemi haonji hata supu wala haongei hahahaha
 
Ungempa Huyo Jamaa Yako Usingepoteza.

Maana Kumbuka Tayari ulishatoa Sadaka Kanisani kwa mungu wa Kanisa hilo..

Kama Tayari umeshatoa Jua Kwamba Ulinyemnyima Muujuza Wa Mungu mwenye vyote umekufundisha Jambo. Hao uliowapa Hawajawahi mpa Mungu hizo sadaka wanapeleka wanapopeleka

Sadaka zote hizo utfikiri kodi ya wavuvi

Hao watu wanapata wapi ujasiri wa kutoa hela zote kwa mtu mmoja?

Unampita masikini barabarani unajifanya humuoni na hela unazo mfukoni kumbe unapeleka kanisani ambapo hela zote hizo ndio zimezungusha uzio na kujenga maduka 100 na kila mwezi wanakusanya kodi zaidi ya 5m kiulaini

Kweli wajinga waliwao
 
Back
Top Bottom