Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji!

Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji!

HATA ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA ........JUA ILO🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾



SO DODOMA HAITAJENGWA KWA SIKU MOJA PIA..............
 
HATA ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA ........JUA ILO🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾🙏🏾



SO DODOMA HAITAJENGWA KWA SIKU MOJA PIA..............
Kama tunajenga Roma nyingine basi tufanye kweli siyo kuimba mistari ya historia huku ground ni kama scene ya Walking Dead usiku.
 
Nimependa ulivyojitahidi kutetea Dodoma kwa mantiki ya karne ya 20, huku ground ikiwa giza saa mbili na stendi ikifanana na hifadhi ya Taifa.

Ofisi za serikali kuwa mchana ni kweli – ila usiku kuna wananchi wanaotoka safari, na ndio maana kuna neno public service – si VIP silence.

Kuhusu “mabasi matatu kunitosha”, hiyo ni sarcasm ya mtu aliyekaa kwenye ofisi yenye AC na hajui ground level.

Na ile ya kujituliza kwa mkono... 🤣 kaka kama hicho ndo kiwango chako cha hoja, basi pole sana – utulivu wa Dodoma hauwezi kusaidia akili isiyopumzika
Nimekuelewa pointi zako ndugu yangu, kuhusu hizo taa za barabarani/side walk, ni muhimu kweli kwa usalama wa raia, kuhusu mabasi ya usiku hili si tatizo la serikali bali wafanyabiashara/wenye mabasi, probably wameona hawapati faida kutokana na uchache wa abiria wanaotaka kusafiri usiku. ( who knows )
 
Ukweli usemwe Jiji la Dodoma hawajajipanga. Kuna maeneo wamepima mapoli lakini hata barabara za kuchonga hamana watu watajengaje? Maeneo ya Kikombo, Lugala, Ntyuka, Mahomanyika yote yamepimwa viwanja lakini barabara hazijachongwa zaidi ya miaka mitano huu ni utapeli.
Mji gani Tanzania hii zilianza kuchongwa barabara kabla ya watu kujenga?
 
Mji gani Tanzania hii zilianza kuchongwa barabara kabla ya watu kujenga?
Wewe ni mpuuzi na uelewa wako ni mdogo. Ubongo pilitoni. Mji wa serikali mtumba barabara zilichongwa kabla ya ujenzi. Barabara walau za greda inabidi ziwepo kabla ya ya watu kujenga. Au watabeba kichwani vifaa vya ujenzi?
 
Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌

Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.

Lakini balaa lilianzia hapo!

Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.

Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:

Harakati za usiku

Mabasi ya safari za usiku

Taa za barabarani na stendi

Miundombinu ya usalama

Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."

Maswali yangu kwa wana JF:

1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?

2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?

Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Taratibu kuwa mvumilivu
 
Kukosolewa siyo dhambi, labda uwe chukuwachakomapema!
Sikiliza na soma maoni, jiulize ni kweli?
Kama uongo tupa kule, kama kweli yafanyie kazi, full stop!
 
Ah, kumbe hoja zako zinapimwa kwa ID ya kujiunga JF, siyo yaliyosemwa? Hii nayo mpya

Nanenane kuwa km 7 haina maana kama usiku ukishuka hapo ni kama unaingia kwenye episode ya Survivor: Dodoma.

Na kuhusu "usalama", utulivu usiku bila huduma ni sawa na kuwa na kasri lenye mlango usiofunguka. Mtu akishindwa kupata usafiri, taa zikiwaka lakini watu hakuna – huo si utulivu, ni jiji linalopumua kwa masaa.

Wewe endelea na PowerPoint zako – sisi tulioenda ground tutaendelea kusema tulichokiona, sio kupaka lipgloss kwenye matatizo.
Haya ni kama majibu ya ChatGPT hivi. Ulikuwa unaiomba ChatGPT ikusaidie kukupa majibu ili ushinde kwenye JF arguments? Just asking 🤔
 
si ungeondoka na mabus ya aubuhi nawewe nae,yaani ulitaka bus likupeleke Dar jioni abiria mmoja
 
Trust the process. , everything will be okay hata ROMA haikuwa hivyo tunavyoiona , hata NEW YORK HAIKUWA HIVYO TUnAVYOIONA .
 
Trust the process. , everything will be okay hata ROMA haikuwa hivyo tunavyoiona , hata NEW YORK HAIKUWA HIVYO TUnAVYOIONA .
Yes kama tuna jenga roma ,New york nyingine tuanze na mambo madogo kama ayo ya ndani so unaenda stend unakuta taa haziwaki kweli
 
Back
Top Bottom