Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji!

Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji!

Itakuwa Dodoma ya Zanzibar hiyo, Dodoma ninayoujua mie Haina shida ya usafiri, ungeuliza wenyeji.

Kwanza unaenda stand kufanya nini, unategemea utapata usafiri stand?
 
Kinachofanya mji uchanganke sio majengo ya ghorofa, majumba ya starehe wingi wa magari bali ni shughuli za kibinadamu zenye uhitaji zinazoambatana na fursa za utafutaji na kipato kinachopelekea matumizi.

Dodoma inajengeka taratibu lakini kuilinganisha na Dar es salaam ambako idadi ya watu na mzunguko wa pesa wa watu million tano, ni vitu viwili tofauti. Baada ya miaka 10 kuanzia sasa Dodoma itakuwa mwao....Labda!.

Mwaka huu mwanzoni nilipita Dodoma kama transit... Nilikuwa na muda wa masaa 8 ya kuivinjari Dodoma na budget ilikuwepo, nilitafuta tax driver mzoefu pale anipeleke sehemu anayoamini ndio Icon ya mji ule kwa mtu anayehitaji kutumia pesa yake kwa maana ya utalii wa ndani....Ilishindikana!.

Sehemu zote alizonipeleka na kunionyesha naweza kusema tu hazifai labda ujilazimishe kuridhika. Mwisho wa yote niliamua kwenda kushinda SGR_TZ hadi nilipoondoka Dom saa 12 jioni.

Najuta tu kuwa nilisahau kwenda Msalato kwenye mahakama ya wanyama kula nyama choma.
 
Kinachofanya mji uchanganke sio majengo ya ghorofa, majumba ya starehe wingi wa magari bali ni shughuli za kibinadamu zenye uhitaji zinazoambatana na fursa za utafutaji na kipato kinachopelekea matumizi
Kwa kukusaidia tu Dom wanaongoza mapato ya halmashauri Tanzania na mapato ya TRA wapo top 5
Ubora wa mji wowote duniani haupimwi kwa eti "kuchangamka usiku" ingekua hivyo nadhani Las Vegas ingekua inaongoza Marekani kupita hata New York au Los Angeles.

Dodoma wanaongoza Tanzania kwa mipangomiji bora,miundombinu,mtandao mpana wa barabara za lami,miradi mingi inayojengwa na inayotarajiwa kujengwa n.k
 
Sisi ndo wakaz wa Dodoma wenyewe, ukiongea Dodoma, usiongelee pale Jamatini pekeake. Nenda huko Mpwayungu, sanzaa, kondoa huko!, pita pale mto bubu!! Uone Kama Kuna daraja lolote mpka sasahivi tangu lile la Mwanzo kusombwa na maji.

Msiishie Laptrona, The bistral, Chakonichako, Rainbow, au Bambalaga... Nenda huko chipanga, chiguruka na chikopelo angalia Hali halisi.

Dodoma haishii Jamatini na Nyerere square
Nadhani unachanganya mambo.. mtoa mada kazungumzia Jiji la Dodoma sio mkoa wa Dodoma
 
Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌

Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.

Lakini balaa lilianzia hapo!

Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.

Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:

Harakati za usiku

Mabasi ya safari za usiku

Taa za barabarani na stendi

Miundombinu ya usalama

Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."

Maswali yangu kwa wana JF:

1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?

2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?

Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Hata ukiwa na kipaji cha roho mbaya,kuna mda jifunze hata kuona aibu kusema uongo.
 
We unasema dodoma ya somalia au? Coz naona umeandika upupu tu kuhusu jiji letu la ddm
 
Mkuu,Maisha ya Usiku yanajengwa na Spending Power,Attractions,Activities,Security and Safety na Populations.Sasa Dodoma Kwa design yake ya Sasa na Economic Structure yake bado inahitaji uwekezaji mkubwa na Pouplation Kubwa ili iwezeo kuwa na Active Life Usiku na Mchana.

So Kimsingi Night life Haijengwi kwa matamshi bali kwa engagement.
 
Mkuu umeandika thesis ya uchumi, lakini ground bado ni giza na vichaka. Huku tunazungumzia maisha halisi ya watu, si presentation ya PowerPoint.

SGR inafika Dodoma lakini mtu akishuka usiku anabaki na swali: “Je, niko Tanzania au nimeingia bush safari?”

Nightlife haitaki grammar, inataka mwanga, watu na shughuli. Hadi basi la usiku lipatikane bila kuomba dua.
 
Kwahiyo unaona Daslam ndo jiji la maana mshamba wewe?
Basi kama kuipenda Dodoma ni lazima kubeza Dar, umeshindwa somo la mijini.
Jiji la maana si lile lenye title – ni lile linaloishi. Ukiamua kuipenda Dodoma, usibandike stress zako kwa Dar.
Na kuhusu mshamba... mtu anayepanic kwa kutajwa stendi kimya ndiye mshamba. Ulikuwa stendi lini mkuu? Au unasimulia
 
We unasema dodoma ya somalia au? Coz naona umeandika upupu tu kuhusu jiji letu la ddm
Acha hasira za kizalendo kipofu kaka 😂

Hatusemi Dodoma ni Somalia, ila usiku bila mwanga wala magari unaweza hisi uko kwenye Survivor Bush Edition.
Sema ukweli ukomboe jiji – siyo kila anayesema changamoto ni "anaharibu jina".
 
Tanzania yote maisha ya usiku yanaanza Alhamis
😂😂Maisha kuanza Alhamisi si hoja ya msingi – maana hata disco likiwa limefunguliwa, kama taa za stendi hazipo na usafiri hakuna, utacheza mziki kwa torch light?
 
Dodoma ipi unazungumzia mzee
Dodoma ya kuingia saa 2 usiku ukakuta basi 3 tu na stendi kimya kama msitu wa hifadhi, taa hakuna, njia ni vichaka.
Kama wewe unajua Dodoma nyingine yenye hekaheka na mwanga usiku, basi labda unaishi kwenye Dodoma ya Google Earth, si ya ground.
 
😂😂Maisha kuanza Alhamisi si hoja ya msingi – maana hata disco likiwa limefunguliwa, kama taa za stendi hazipo na usafiri hakuna, utacheza mziki kwa torch light?
Bado unapanda mabasi wenzio wako kwenye SGR
Ila masikini wenzio usiku wanapandia pale CBE malori
 
Sitaki kuingilia biffu lenu lakini kwa uhakika Miji iliyoendelea, BUS unatakiwa upandie Bus Stand na siyo Barabarani.

Ni kama Treni huwezi panda Treni vichakani, ina vituo vyake rasmi na ndivyo inapaswa kuwa kwa Buses.

Bus linapaswa liwe Stand na Liwe na Vibao au Electronic Sign kueleza linakwenda wapi kupitia wapi.

Na Kila Bus Linapaswa kuwa na Ofisi yake, Waweke Number za huduma kwa mteja, au Muda wa Bus Kuondoka na linaelekea wapi, ili abiria wake wawe na sehemu ya kuuliza au pa kuanzia.

Siyo kufanya mambo kiholela kama dala dala halafu tuite huo ndio ujanja.
Wenzake wanapandia gari Makole yeye unapuyanga kwenda 8 8 usiku.
 
Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌

Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.

Lakini balaa lilianzia hapo!

Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.

Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:

Harakati za usiku

Mabasi ya safari za usiku

Taa za barabarani na stendi

Miundombinu ya usalama

Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."

Maswali yangu kwa wana JF:

1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?

2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?

Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Masaa ya ofisi za serikali / bunge ni asubuhi , mchana hadi jioni , SIYO USIKU.

Sasa wewe ulikuwaunatafuta MACHANGU au Mabasi ?
Abiria mmoja mabasi matatu hayakutoshi ?

Kumbukakuwa, makao makuu yanapaswa kuwa katika mkoa ambao una utulivu na upo in-ze mido ya nchi , ili waheshimiwa waweze kukutana kwa urahisi na waweze kufocus. Ndiyo maana Dar haina sifa ya kuwa makao makuu ya nchi, makelele ni mengi, hali mbaya ya hewa, mabasi ni mengi sana [ sori nimemaanisha machangu]
Kila la kheri mkuu, I hope ulikuwa mbunifu ukatumia mkono kujituliza baada ya kutofanikiwa kupata mabasi ya usiku.
 
Back
Top Bottom