Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji!

Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji!

Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌

Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.

Lakini balaa lilianzia hapo!

Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.

Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:

Harakati za usiku

Mabasi ya safari za usiku

Taa za barabarani na stendi

Miundombinu ya usalama

Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."

Maswali yangu kwa wana JF:

1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?

2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?

Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Mshamba utamjua tu, ulitokea bara lipi hp duniani?
 
Ndio kabisa, hali ni hiyo halisi. Dodoma bado ina changamoto kubwa za miundombinu na usimamizi.

Kuna maeneo yamepimwa lakini hayajapokea maendeleo halisi, barabara bado ni changamoto kubwa.

Hii ni changamoto ambayo inahitaji serikali na wananchi kushirikiana kwa dhati kuboresha maisha ya watu
Dodoma ipi yenye changamoto ya barabara au umesimuliwa tu aisee🤣🤣. Kwa mujibu wa TANROADS Dom inazidiwa na Ilala CC pekeyake kwa Mtandao mpana wa barabara za lami. Hakuna mji wowote Tanzania ambao unafika hata nusu ya ubora wa Dom kwenye mipangomiji na miundombinu.
 
Hapo umenena mkuu! Dodoma bado ni jiji kwa jina tu – kimatendo ni kama mji wa kata uliolazimishwa ukuaji.
Saa mbili usiku stendi kimya, maduka yamefungwa, mitaa kama haina roho. Mbeya, Arusha hata Mwanza viko mbali mbele kwenye uchangamfu na maisha ya jiji.
Serikali inatakiwa iangalie hili kwa jicho la pili, vinginevyo Dodoma itabaki ni makao makuu ya ofisi tu, si maisha ya watu
Yaani mtu unajadili eti "uchangamfu wa mji usiku" 😂😂 kwako ndio kigezo cha kupima ubora wa Jiji duuh rudi facebook.
Nilitegemea ungejadili hivi vitu kama mtu aliyeenda shule👇👇
-Mipangomiji
-Mtandao mpana wa barabara za lami
-Miundombinu
-Huduma za Kijamii
-Vyuo Vikuu
-Mapato(Halmashauri+TRA)
-Viwanda
-Uwepo wa mashirika ya kimataifa
-Ofisi nyingi za serikali
-Maghorofa
-Miradi ya ujenzi inayojengwa na inayotarajiwa kujenga n.k
 
Sitaki kuingilia biffu lenu lakini kwa uhakika Miji iliyoendelea, BUS unatakiwa upandie Bus Stand na siyo Barabarani.

Ni kama Treni huwezi panda Treni vichakani, ina vituo vyake rasmi na ndivyo inapaswa kuwa kwa Buses.

Bus linapaswa liwe Stand na Liwe na Vibao au Electronic Sign kueleza linakwenda wapi kupitia wapi.

Na Kila Bus Linapaswa kuwa na Ofisi yake, Waweke Number za huduma kwa mteja, au Muda wa Bus Kuondoka na linaelekea wapi, ili abiria wake wawe na sehemu ya kuuliza au pa kuanzia.

Siyo kufanya mambo kiholela kama dala dala halafu tuite huo ndio ujanja.
Kwahio, hayo mazingira yoote uliyosema ndo yanapatikana Dar? 😂😂😂.. kaka aaah
 
Dodoma ipi yenye changamoto ya barabara au umesimuliwa tu aisee🤣🤣. Kwa mujibu wa TANROADS Dom inazidiwa na Ilala CC pekeyake kwa Mtandao mpana wa barabara za lami. Hakuna mji wowote Tanzania ambao unafika hata nusu ya ubora wa Dom kwenye mipangomiji na miundombinu.
Ya kweli mzee? Tusisifie vitu ambavyo sio
 
Aisee CBE sio Dodoma yote, na si kila mtu anashuka na Alphard kama wewe na ndoto zako za V8.****

Mimi nilienda kwa SGR, nikarudi kwa basi – ground reality nikaiona: stendi ya usiku ni kichaka, taa hakuna, mabasi hakuna. Huu si ushamba, ni uhalisia.

Na by the way, , unahangaika na comments – tunaishi maisha, wewe unawaza options.

Endelea na mbwembwe, sisi tupo kazini na ground tukisema ukweli. 😉
Hio stend anayosemea ni ile ya nane nane, au stend za daladala, Kama sijamuelewa! Sisi wengine tumesafiri sana usiku.. aeleze vizuri
 
Maswali yangu kwa wana JF:

1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?

2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?

Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Mimi nimepapenda Dodoma palivyo vile vile kiporipori usiku
 
Hio stend anayosemea ni ile ya nane nane, au stend za daladala, Kama sijamuelewa! Sisi wengine tumesafiri sana usiku.. aeleze vizuri
Itakua Nane Nane ndio karibu na Nzuguni
 
We ndo mshamba ungesema hujui machimbo tungekuelewa, umezoea huko Madongo kuinama kwamba sehemu iliyochangamka na amsha amsha ni Stendi ya mabasi 😅
Hapo mabasi yanapitia kukatwa ushuru afu ndo yanaingia town Sasa,
 
Ya kweli mzee? Tusisifie vitu ambavyo sio
Mkuu, Tanzania hii hakuna mji uliopangiliwa vizuri kama Dodoma..lami kila sehemu.Vilevile Dom unaweza kutembea usiku wa manane katikati ya mji bila kuogopa chochote..Kwa kifupi hali ya usalama ni kubwa mno ndiomana ni mara chache sana kusikia matukio ya wizi mkubwa au ujambazi Dom.
 
Unapajua kizota, chang'ombe, au buyuni kule...
Wezi wadodoma wanakukaba na wanaua kabisa...
Unawajua Team barakoa wew?
" Number one kwenda mpaka mpalanga Kuna lami gan?
... Daah we unaisoma dodoma sisi tunaishi
 
Kwa kuwa umetoka kufanya interview, tutakupangia Nachingwea ambako ni mjini ili ukale maisha huko na wenzio msio na jema kwa serikali yenu.​
 
Unapajua kizota, chang'ombe, au buyuni kule...
Wezi wadodoma wanakukaba na wanaua kabisa...
Unawajua Team barakoa wew?
" Number one kwenda mpaka mpalanga Kuna lami gan?
... Daah we unaisoma dodoma sisi tunaishi
Hiyo ni mitaa ya uswahilini ndio unakuta vibaka kwamfano Mkalama,Chaduru,Swaswa,Changombe nk lakini kiujumla Dom mitaa yote ni salama (japo tahadhari ni lazima kuchukua) ndiomana sijawahi kusikia mfano uporaji au uvamizi wa mabenki Dom kama ilivyo miji mingine mikubwa Tanzania
 
Makao Makuu Gani Haya? Dodoma Usiku ni Kama Kijiji! 🏙️❌

Wakuu, nashindwa kuvumilia hili nisilitupie JF. Nilikwenda Dodoma hivi majuzi kwa ajili ya interview, nikasema acha nipange basi kwenda mapema – nifanye interview asubuhi, nimalize mambo yangu, then nitafute basi la kurudi usiku huo huo.

Lakini balaa lilianzia hapo!

Baada ya interview nikawa nime enda restaurant fulani nikiikilia interview nikakimbilia stendi jioni kuelekea usiku, nikashangaa stendi yenyewe ipo pembeni kabisa karibu na kichaka! Ukishuka tu, unasafiri kwa miguu kwenye njia za bush hadi ufike ndani ya stendi. Yaani taa nyingi hazifanyi kazi, na hakuna hata ulinzi wa maana. Usiku ule nikaona mabasi matatu tu ndani ya stendi. Nikauliza nikaambiwa:
"Dodoma hakuna mabasi ya kuondoka usiku. Yale yalikuwepo ndiyo yamebaki hapa kwa kesho.

Nikabaki najiuliza: hivi tunalazimisha Dodoma kuwa makao makuu kwa nguvu za kiserikali tu au kuna mpango wa kuiendeleza kweli? Mji mkuu wa nchi unakosa:

Harakati za usiku

Mabasi ya safari za usiku

Taa za barabarani na stendi

Miundombinu ya usalama

Sasa kama mimi mgeni ningeibiwa pale au hata kushambuliwa, nani angenisaidia? Hii ni aibu kwa mji unaoitwa "Makao Makuu ya Taifa."

Maswali yangu kwa wana JF:

1. Kwa nini Dodoma bado haijawa na maisha ya usiku licha ya kuwa makao ya Serikali?

2Tunalazimisha au tunajenga maendeleo ya kweli?

Naomba tupige stori bila chuki, lakini kwa uzalendo wa kweli.
Interview itakuwa imekuvuruga wewe, aliyekuambia.Dodoma hakuna usafiri wa usiku nani? Kwamba ulifika stendi ukauliza wauza maji na matunda kwenye mabasi wakujibu wakati Hadi unamuuliza hajauza hata chupa.moja akujibu nini? Labda nikusaidie hakuna mkoa wenye usafiri mwingi Kama Dodoma, hapa hapa Dodoma kuna mabasi yanoyosafiri usiku, mtu anatoka Dodoma saa nne usku saa tatu asubuhi yupo Zanzibar. Kama ulikosa gari la kurudi kijijini kwenu nitakuelewa maana magari ya vijijini yako pembeni mwa mji. Dodoma ipo katikati ya nchi kuna mageri ya kwenda mikoa karibu yote wewe ulitaka usafiri wa wapi ukaukosa na basi zote lazima ziingie stand kuu Kama Magufuli wanavyofanya. Wewe ulikurupuka kwenda kufanya interview bila kujiandaa unaona matokeo yake, siku nyingine jiandae anayeijua Dodoma akisoma uzi wako atakushangaa Sana. Halafu basi zetu siku hizi ni za mizigo na abiria wachache, tunasafirisha mizigo kwenye basi tunapanda SGR au ndege tukifika jiona tunakwenda kuchukua mizigo yetu iliyosafirishwa kwa mabasi, sema lingine sio usafiri
 
Mpe 95% kaongea ukweli
Sisi ndo wakaz wa Dodoma wenyewe, ukiongea Dodoma, usiongelee pale Jamatini pekeake. Nenda huko Mpwayungu, sanzaa, kondoa huko!, pita pale mto bubu!! Uone Kama Kuna daraja lolote mpka sasahivi tangu lile la Mwanzo kusombwa na maji.

Msiishie Laptrona, The bistral, Chakonichako, Rainbow, au Bambalaga... Nenda huko chipanga, chiguruka na chikopelo angalia Hali halisi.

Dodoma haishii Jamatini na Nyerere square
 
Back
Top Bottom