Makapuku Forum

Makapuku Forum

Kiungo wa Juventus, Paul Pogba amekiri kwamba alifikiria kustaafu soka kufuatia madai ya unyang’anyi yaliyohusisha familia.Kiungo huyo wa kimatafa wa Ufaransa alitishwa na genge la watu wasiojulikana ambao walifunika nyuso ikidaiwa walimfosi kutoa mamilioni ya pesa huku kaka yake Mathias Pogba akihusishwa katika mpango huo wa kiharamia.
.
Mathias alichunguzwa na polisi kutokana na madai hayo aliyohusishwa akiwa mahabusu pamoja na watu wengine wanne kwa miezi miezi mitatu mwaka jana. Kaka huyo wa Pogba alikana shutuma hizo akidai hana hatia katika jaribio la unyang’nyi dhidi ya ndugu yake na aliachiwa huru kufuatia amri ya mahakama na alipigwa marufuku kuwasiliana na mdogo wake.
.
Kiungo huyo aliyewahi kubeba Kombe la Dunia 2018 aliripoti polisi kutoa ushahidi na amezungumzia sakata hilo lilivyoiathiri familia yake; “Pesa zinabadili tabia ya mtu. Familia inaweza kuvunjika. Vita inaweza kutengenezwa,” alisema Pogba.
.
“Kuna wakati nilikuwa nikifikiria nilitamani kutokuwa na pesa tena. Sikutaka kucheza soka tena, nilitaka nibaki kuwa mtu wa kawaida watu wanipende kama mimi na sio kwa sababu ya umaarufu wangu. Kuna wakati inakuwa ngumu sana.”Pogba aliwaambia polisi kwamba genge hilo la wahuni lilianza kumtishia tangu Machi, mwaka jana huku likimsisitiza atoe Pauni 11 milioni.
Screenshot_20230912_133215_Instagram.jpg
 
[emoji599] Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametajwa kuwa mrithi sahihi wa Hansi Flick baada ya kutimuliwa katika timu ya taifa ya Ujerumani. Uamuzi huo umefuata Ujerumani kupokea kichapo cha mabao 4-1 ilichopata Ujerumani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Japan, juzi.
.
Licha ya Klopp kuweka wazi kwamba atajitolea zaidi kuinoa Liverpool, lakini alikiri litakuwa jambo la kujivunia endapo atakifundisha kikosi cha Ujerumani ambako ndiko kwao.
.
“Kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani ni jambo la kujivunia. Hakusa maswali kuhusu hilo, lakini siwezi kuondoka Liverpool kwa sasa halafu nikaifundishe kwa muda mfupi. Huwezi kufanya kazi kwa namna hiyo kama ikitokea natakiwa kuwepo muda wote kwa ajili ya timu,” alisema Klopp
.
Kabla ya kufukuzwa kazi, Hansi alisisitiza kwamba anastahili kupewa muda zaidi wa kukisuka kikosi chake baada ya kichapo walichopata dhidi ya Japan, lakini mashabiki wengi wa soka Ujerumani walionyesha masikitiko yao mitandaoni.
Screenshot_20230912_133415_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom