Makato anayokatwa Mwalimu mwenye Digrii kwenye mshahara

Makato anayokatwa Mwalimu mwenye Digrii kwenye mshahara

Mwalimu wa Bachelor analipwa 750,000/= ???🥺🥺😳😳😳😳😳😳😳😳
Mbona Pesa Ndogo sana??
Wee unatoka Burundi! Taaluma nyingine wanalipwa kiasi gani kama siyo chini ya hapo. Starting salary ya waalimu ndiyo kubwa kuliko taaluma nyingine ukiondoa afya na baadhi ya taaluma za sayansi kama za geology na engineering.
 
TURUDI DARASA LA QWANZA KIDOGO.


1. 15%- HESLB LOAN
=115,650/-

2. 2%- CWT contribution.
=15,420/-

3. 5%- SECURITY FUND.
= 38,550/-

4. 25%- PAYE.
=192,750/-

5. 3% - NHIF.
=23,130/-

TOTAL:- 385,500/-
LEFT WITH:- 385,500/-

NA HAPO BADO-
✓ Kodi.
✓ Bando.
✓ Babe.
✓ Food.
✓ N.k

Makato ya PAYE (Pay As You Earn) kwa mwalimu mwenye degree yanategemea kiwango cha mshahara wake. Tanzania ina viwango mbalimbali vya kodi ya mapato kulingana na mapato ya mwezi. Viwango vya kodi ni kama ifuatavyo:

- Kiasi cha mshahara kisichozidi TZS 270,000: Hakuna kodi.

- TZS 270,001 - TZS 520,000: 8%

- TZS 520,001 - TZS 760,000: 20%

- TZS 760,001 - TZS 1,000,000: 25%

- Zaidi ya TZS 1,000,000: 30%

REJEA MFANO WA SLIP YA MALIPO APO CHINI: PIA TOA MCHANGO WA MAONI YAKO VP HII KAZI INALIPA AU LAAH.?

View attachment 3041578
Huwa mnapata faida gani mnapopika majungu? Hizo % za PAYE umeitoa wapi? Kwa nini hujasema hiyo 20% au 25% ni ya kile kinachozidi kwenye 520,000/=?
 
NAHITAJI MWALIMU MMOJA ANIONESHE HIYO PAYING SLIP.
LENGO NI KWAMBA NAHITAJI NIONE HIZO ASILIMIA ZA MAKATO KWA SASA.
✓ NHIF- ASILIMIA NGAPI.?
✓ PAYE - ASILIMIA NGAPI.?
✓ CWT- ASILIMIA NGAPI.?
KIPI KIMEONGEZEKA NA KIPI KIMEPUNGUA NDY LENGO KUU!
Mbona Prakatatumba abaabaabaa amepost na akaionyesha ulikuwa wapi??
Maana kapost salary slip yake ikiwa na makato halisi na mpaka Take home
 
Wee unatoka Burundi! Taaluma nyingine wanalipwa kiasi gani kama siyo chini ya hapo. Starting salary ya waalimu ndiyo kubwa kuliko taaluma nyingine ukiondoa afya na baadhi ya taaluma za sayansi kama za geology na engineering.
Hapana mkuu..
Taja taaluma inayolipwa Chini kuliko walimu!
Mahakama au Ardhi au Ni Utawala ni wa kina nani hao Fedha??
 
Mleta mada maisha ni kujipangia mwenyewe kuna mtu alikuzuia labda usisomee fani zinazolipa vizuri au kuna anayekulazimisha usibadili fani usome ingine unayoona ina pesa kuliko ualimu

Maisha yako ulipanga yaende huko unakuja kumbwekea nani humu mjinga wewe?

Badili course au ajira au ka retrain kasomee kingine chenye pesa
 
Mleta mada maisha ni kujipangia mwenyewe kuna mtu alikuzuia labda usisomee fani zinazolipa vizuri au kuna anayekulazimisha usibadili fani usome ingine unayoona ina pesa kuliko ualimu

Maisha yako ulipanga yaende huko unakuja kumbwekea nani humu mjinga wewe?

Badili course au ajira au ka retrain kasomee kingine chenye pesa
UMEFIKA MBALI SANA,, NDUGU SIO VIZURI KUTUKANANA MATUSI.
 
Ndyo boss Nimeshangaa kwa sababu Ni mshahara wa Tabibu wa cheti (Clinical assistant aliyekaa kazini Miaka mitatu)..

Na ni Mshahara wa Tabibu ( Clinical officer ) Diploma na pia ni mshahara wa Nurse aliyekaa kazini miaka mitatu au Mshahara wa Afisa muuguzi msaidizi anayeanza kazi..

Na pia ni mshahra wa Kuruta ambaye Yuko mafunzoni RTS aliyeishia Form four na Ni just Constable tu..

Na ni mshahara wa Afisa Ugani wa Kilimo mwenye Certificate aliyefanya kazi kwa Miaka mitatu na Ni mshahara wa Afisa Ugani wa Kilimo na Mifugo mwenye Diploma anayeanza kazi..

Kiukweli Nimeshangaaa sana bhasi ndyo maana walimu Wanadharaulika sana
Kasome upya uhamie kwenye hizo fani zinazolipa badala ya kukaa unashangaa shangaa humu jamii forums
 
Nimekwambia zote kasoro hizo nilizotaja hapo juu. Nenda kalinganishe kwa mfano TGS E ya mwalimu na TGS E ya taaluma nyingine.
Mjadala Maridadi kabisa nipo nafatilia Mkuu wangu..

ila ningependa kuchangia kidogo..

Mwalimu hana TGS ana TGTS..
Na kingine Scale za Serikali haziangaliwi Kwa kufuata scale ila taaluma

Kuna vingi nimeona huyu kijana anajiita Truth Bot AI anapost Viko sahihi Vingine naona Ana mzuka sana na Huenda Ni mwalimu na anawachukia Walimu..

Kwa mfano Tulinganishe Afya na Elimu..

Scale ya Elimu kwa Certificate ni TGTS B
Scale ya Afya kwa Certificate ni TGHS A

Scale ya Elimu kwa Bachelor ni TGTS D
Scale ya Afya kwa bachelor inaanzia TGHS D kwa (Nursing, maabara,phamarcy na kozi zingine) na TGHS E kwa Daktari. Na Daktari ambaye ni Specialist ni kuanzia TGHS G

So huwezi kulinganisha scale kabla hujajua Wenye hiyo scale ni level gani ya Elimu..

Mjadala mzuri ila kama hamjapata Jinsi ya kuujadili mtakesha..

Niliona pia Prakatatumba abaabaabaa alitoa ushahidi mzuri sana nimependa kwa kweli..

Na hii ndo Jf ya Zaman hakuna blah blah kama huna taarifa hakuna haki ya Kuongea
 
Back
Top Bottom