Maketa: Tendo la ndoa kinyume cha maumbile ni chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika

Maketa: Tendo la ndoa kinyume cha maumbile ni chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika

Sababu nyingine wamama wamegeuka kuwa wababa wakati wahenga waliagiza Kazi ya Juma ni kuchuma na mwajuma Kukaa ndani! Hata kama Juma ni maamuma! [emoji56][emoji24]
 
Siyo kweli, wafanye research aje na sababu halisi na za kweli.

Kwa research ya JF tunajuwa sababu ni nini lakini siyo hiyo anayotaka kutuaminisha huyo Joyce.
WEKA NA WEWE SABABU ZAKO ACHA KIPINGA BILA SABABU
 
Afisa Ustawi wa Jamii wa Jiji la Dar es Salaam, Joyce Maketa, amesema kwamba miongoni mwa mambo yanayovuruga ndoa hadi kupelekea wanandoa kuachana inasababishwa na wanaume kuomba mahusiano kinyume na maumbile.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 6, 2022, jijini Dar es Salaam, kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio mara baada ya taarifa kuonesha kwamba kila mwezi ndani ya jiji la Dar es Salaam takribani ndoa 300 zinavunjika.

"Kumekuwa na mahusiano mapya (Kwa wanandoa) yanayopelekea wakati mwingine kuomba kuwa na mahusiano kinyume na maumbile hicho kimekuwa ni moja ya kitu ambacho kimekuwa kikivuruga ndoa nyingi na watu mwisho kuachana, tuachane na hizo tabia tunazozi-copy na tuishi maisha yanayompendeza Mungu,"amesema Joyce

====

Haya yanajiri baada ya kamati ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya jamii kutoa ripoti Septemba 5, 2022 iliyoelezea kuwa mkoa wa Dar es salaam unaongoza kwa uvunjifu wa ndoa nyingi nchini ambapo wastani wa ndoa 300 huvunjika kila mwezi.

Kamati hiyo ilibaini pia kuwepo kwa mmomonyoko mkubwa wa maadili na ukatili mkubwa wa kijinsia hasa ule unaohusisha watoto.

EATV

Yeye aliombwa halafu akavunja ndoa yake?
 
Back
Top Bottom