Makinda abadili gia angani, asema kuhesabiwa ni siku saba

Mdukuzii

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
2,552
Reaction score
6,422
Kutoka moyoni tumekwazika, tumesubiri makarani kutwa nzima kumbe ni zoezi la siku saba. Kama ni zoezi endelevu, kwanini leo ikawe mapumziko?

Sensa ya kuhesabu siku saba itakupa majibu ya uongo maana watu hawatulii sehemu moja kama mawe. Kuna watu hawatahesabiwa au watahesabiwa mara mbili bila kujijua.

Mfano leo, nipo kwangu Lushoto hamjaja. Kesho nitakuwa safarini Ludewa ndio mtakuja kwangu Lushoto, nikifika Ludewa nitakuta mmeshapita, hapo nani kamchenga mwenzake.

Zoezi mmeliharibu wenyewe
 
Toka mwanzo walisema ni siku 7.
 
Hata mimi na majirani zangu bado.
Na kesho kazi kama kawaida. Nilipoituma hii post humu,wengi hawakuelewa. Nadhani sasa mmepata logic!😃😃nimecheka sana!
NB: Hajabadili gia. Utaratibu uko hivyo kwa miaka yote!
 
Yaani wameniudhi mimi, nilikuwa na mishe zangu za ufundi bomba mteja kanipigia nikamtolea nje
 
Sensa ni ama mahali unaposhinda wakati wote (hii kufanyika nchi zilizoendelea)

Au Sensa ni mahali ulipolala usiku wa kuamkia tarehe 23 Agusti, 2022. Hii ni sensa ya nchi zinazoendelea

Kwahiyo, we chunga tu tarehe 23 Agusti ulipoamkia hata wakija siku ya 7 majibu ni yale yale
 
Tatizo dodoso refu sana wangeweza kumaluza keo ,nani atakariri kuwa tarehe 23 alilala wapi,wengine walilala njiani wanatafuta maisha
 
Kuna mapungufu mengi, leo asubuhi nimefikiwa na karani kuhesabiwa saa 3:53, saa 5:27 nikapokea mgeni aliyetoka safari Kigoma wakati karani ameshaondoka, nikajiuliza, huyu ni mgeni mmoja, je kuna watu wangapi wako safarini na huko waendako watafika wenyeji wao wameshahesabiwa, je ni watu wangapi wameamkia kwenye hotels, lodgings na guest houses wataingiaje kwenye takwimu?
 
Kwa walioko safarini ikiwa walilala nyumba za wageni au kituo cha bus, ilipaswa karani apite usiku kuwahesabu na wangepewa beji maalum yakuonesha kuwa wamehesabiwa (dodoso lao ni maalum) Kama alilala nyumbani, basi hapo alipolala wanapaswa kutoa taarifa zake.

Dokezo langu: inasikitisha ikiwa hadi mwanajf hajui kuhusu utaratibu wa wanaotakiwa kuhesabiwa. Je, huko sigimbi?
Mbwembwe zote zile za hamasa zilikuwa na faida gani ikiwa watu hawajui utaratibu?🤔
 
Mzee wewe mgumu kuelewa

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Huyu aliyefika kwangu saa 5 hajakutana na karani popote, in other words wamesafiri usiku kucha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…