Jamani mimi nashindwa kuelewa, hivi hatujawai kuhesabiwa? Hii ni mara ya kwanza?
Karani hata akija kesho kutwa yeye atakua interested na watu waliolala tarehe 23.
Kiuhalisia, ingewezekanaje kuhesabu watu wote kwa siku moja?
Tuwe wavumilivu,tutulie leo siku ya kwanza, tuwape muda, changamoto zitakuwepo lakini ni kazi gani inakosa changamoto.
Wakati nasoma o level, chemistry, ilikua tukiingia lab kufanya test mwalimu alikua anasema " ukiona umepata jibu haraka ujue umekosea" nataka kusema nini?
Zoezi hili ni la kitaifa litachukua walau siku kadhaa kufanikishwa, lingekua rahisi mimi ningemkumbuka mwalimu wangu kuwa " ukiona unapata jibu haraka ujue umekosea"
Tuwe watulivu, tutahesabiwa.