Makinda abadili gia angani, asema kuhesabiwa ni siku saba

Makinda abadili gia angani, asema kuhesabiwa ni siku saba

Nyuzi zingine bwana!!!

Karani wa sensa wala hashangai hayo wewe unayoyaletea hoja hapa; namaanisha kwamba kila kitu kinachofanyika kwenye sensa hii basi jua ni copy paste and install ya kilichoandikwa katika miongozo ya sensa

Swala la sensa ni siku sita na ikitokea kaya hazijakamilika/hazijaisha kuhesabiwa basi kutaongezwa siku moja kwajili ya kumalizia kaya hizo... mbona hilo lipo wazi kabisa kwenye mwongozo!!!? Tatizo hamsomi!
 
Kuna madodoso ya makundi maalum mfn wasafiri waliolala guest house watoto wa mitaani makahaba wanaojiuza waliolazwa mahospitalini walio kwenye mabweni mahotelini n.k kwa kifupi hakuna atakayeachwa usidhani hilo halikuwekwa katika consideration
Kuna watu walidandia fuso jana Kiomboi wamesafiri usiku kucha kwenye gari, mtazungukia magari yote kusaka taarifa zao?
 
Kuna watu walidandia fuso jana Kiomboi wamesafiri usiku kucha kwenye gari, mtazungukia magari yote kusaka taarifa zao?
Aidha Taarifa zao zimeachwa mahala walipotokea au watakapofikia watahesabiwa au watahesabiwa kama wasafiri.Nasisitiza hakuna atakayeachwa!
 
Mimi nilitimka mapema asubuhi kuendelea na harakati zangu maana naijua Tz kwenye utendaji.Na niliporudi wala sikuuliza mrejesho.
 
Suala la sensa kwa siku saba maana yake ni posho kwa siku 7.

Mbona taifa halikuambiwa kabla kuwa sensa itakuwa ni siku 7? Kuna mtu lazima awajibike kwa hili.
 
Kaka hilo la kusema watu hawaelewi, watanzania wangapi wanaelewa? Wana elimu hiyo ya kuelewa? Hata maswali tu ya sensa yanazunguka WhatsApp. Kuna mtu hata simu hana. Si bora wangekusanya hizo taarifa manually tu.
Dunia haiwezi kusubiri watu wasioelewa. Watu wanapaswa kujichangamsha na kuelewa mambo yalivyo.
 
Kutoka moyoni tumekwazika, tumesubiri makarani kutwa nzima kumbe ni zoezi la siku saba. Kama ni zoezi endelevu, kwanini leo ikawe mapumziko?

Sensa ya kuhesabu siku saba itakupa majibu ya uongo maana watu hawatulii sehemu moja kama mawe. Kuna watu hawatahesabiwa au watahesabiwa mara mbili bila kujijua.

Mfano leo, nipo kwangu Lushoto hamjaja. Kesho nitakuwa safarini Ludewa ndio mtakuja kwangu Lushoto, nikifika Ludewa nitakuta mmeshapita, hapo nani kamchenga mwenzake.

Zoezi mmeliharibu wenyewe
Hivi Hajat Amina Mrisho Said Yuko wapi ?aliratibu zoezi la sensa la mwaka 2012 vizuri sana na hizi figisu hatukuzisika Sasa Hali imekuwa si Hali zoezi muhimu hili linaenda kufeli
 
Mimi naona mfumo wa sensa haukuwa rafiki!
Siku nyingine sensa kila kitongoji kila mtaaa wapewe mafunzo , vifaa na posho wakazi wa hapo wqjihesabu wenyewe na kupeleka idadi Kwa viongozi wa serikali za mtaa Kisha wilayani.... Ingekuwa siku Moja tu. Siku ya pili kukusanya taarifa
 
Mfano leo, nipo kwangu Lushoto hamjaja. Kesho nitakuwa safarini Ludewa ndio mtakuja kwangu Lushoto, nikifika Ludewa nitakuta mmeshapita, hapo nani kamchenga mwenzake.
Maelekezo yao yalikuwa kuhesabu watu waliolala kwenye nyumba husika usiku wa kuamkia tarehe 23 August 2022

Bahati mbaya sana hili hata mabalozi (wajumbe wa nyumba 10) hawalielewi

Lakini swali linakuja kwa yule ambaye alilala hotelini usiku huo atahesabiwa wapi? Hii sensa itakuja na data za kupikwa tu
 
Kwenye takwimu kuna kitu kinaitwa "recall bias", mpaka sasa kuna watu wameshasahau ni akina nani walilala kwenye nymba yao usiku wa kuamkia tarehe 23 August, kuna watu watahesabiwa zaidi ya mara moja au hawatahesabiwa kabisa. Hii itachananya uhalisia wa takwimu zitakazopatikana, mimi niko dsm lakini hadi leo sijahesababiwa sembuse huko kamsamba?
 
Kutoka moyoni tumekwazika, tumesubiri makarani kutwa nzima kumbe ni zoezi la siku saba. Kama ni zoezi endelevu, kwanini leo ikawe mapumziko?

Sensa ya kuhesabu siku saba itakupa majibu ya uongo maana watu hawatulii sehemu moja kama mawe. Kuna watu hawatahesabiwa au watahesabiwa mara mbili bila kujijua.

Mfano leo, nipo kwangu Lushoto hamjaja. Kesho nitakuwa safarini Ludewa ndio mtakuja kwangu Lushoto, nikifika Ludewa nitakuta mmeshapita, hapo nani kamchenga mwenzake.

Zoezi mmeliharibu wenyewe
Hajabadili gua sema ni upuuzi wako wa kutoelewa
 
Kwa iyo ulidhani nchi nzima wangemaliza siku hiyo kuhesabu? Ulikuwa husikii matangazo
It was possible to do that in a single day. How? Every ten-cell leader with 4 clerks can manage to finish within a day the ten houses. And you select the clerks from within those ten houses whenever possible
 
Back
Top Bottom