Makinda abadili gia angani, asema kuhesabiwa ni siku saba

Makinda abadili gia angani, asema kuhesabiwa ni siku saba

Jamani mimi nashindwa kuelewa, hivi hatujawai kuhesabiwa? Hii ni mara ya kwanza?

Karani hata akija kesho kutwa yeye atakua interested na watu waliolala tarehe 23...
Mkuu hilo tunalijua ila watu wanauliza:

1 kwa nini leo 23.08.2022 ikawa siku ya mapumziko?

2.Je hizi siku saba zinazotoka mfuko wa nyuma nazo zitakuja na mapumziko?

3 Je mimi niksema kesho au kesho kutwa siendi kazini kwa sababu ninamsubiri karani nihesabiwe nitakuwa nimekosea?
 
Wakati mwingine naona watanzania na serikali yenyewe tuna complicate mambo sana, hata kama mtu asipohesabiwa mwisho wa siku sioni kitakachoongezeka au kupungua kwenye mahitaji ya jamii yetu...
Sio kweli, usifananishe zamani na sasa. Hii ni sensa ya kipekee usipange kukosa kwani utajipunja maendeleo
 
Mkuu hilo tunalijua ila watu wanauliza:-
1 kwa nini leo 23.08.2022 ikawa siku ya mapumziko?
2.Je hizi siku saba zinazotoka mfuko wa nyuma nazo zitakuja na mapumziko?
3 Je mimi niksema kesho au kesho kutwa siendi kazini kwa sababu ninamsubiri karani nihesabiwe nitakuwa nimekosea?
Kama ulisikia vizuri walisema, leo mapumziko ili watu waweze kuandaa vitu vyote muhimu na pia iwe rahisi kupata wale ambao walikua stendi tayar kusafiri.
 
Basi wangeongeza vishikwambi na makarani. Au wangepunguza maswali toka 100 ya Sasa na kubakia 3 tu.

Ili ndani ya dakika 10 kaya 5 zihesabiwe.
Hivi huko mliko vishikwambi havijapotea potea??
 
Wakati mwingine naona watanzania na serikali yenyewe tuna complicate mambo sana, hata kama mtu asipohesabiwa mwisho wa siku sioni kitakachoongezeka au kupungua kwenye mahitaji ya jamii yetu...
Mbwembwe nyingiiiii tu naona

Ova
 
Jamani mimi nashindwa kuelewa, hivi hatujawai kuhesabiwa? Hii ni mara ya kwanza?

Karani hata akija kesho kutwa yeye atakua interested na watu waliolala tarehe 23...

Sasa haya mapumziko ya leo yalikuwa ya nini kama utulivu unatakiwa? Nilipoona tu hili zoezi limemilikiwa na CCM moja kwa moja nilijua litakuwa na kiwango duni. Na dalili zote zinaonyesha litakuwa na upikwaji mkubwa wa data. Kama kweli mnahesabu kwa maana ya kuhesabu, iweje viongozi ndio mnawapa kipaombele kwenye kuhesabiwa?

Kipaombele Chenu ni watu kuhesabiwa au viongozi ndio lazima wahesabiwe? Mazoezi kama haya ndio huonyesha uwezo duni wa watendaji wa serikali, na hii ndio sababu utasikia tukosoeni kwa staha. Ukishasikia mtu anasema nikosoe kwa staha, na hataki ushindani, basi ujue ana uwezo mdogo sana, hivyo anajua akikubali ushindani udhaifu wake utakuwa hadharani.
 
Jamani mimi nashindwa kuelewa, hivi hatujawai kuhesabiwa? Hii ni mara ya kwanza?

Karani hata akija kesho kutwa yeye atakua interested na watu waliolala tarehe 23...
Pepa la dk 40, mimi nakamilisja kilijibu kwa dk 30, halafu napata alama 90% nitakuwa nimefeli?
 
Mbona taarifa ilitoka kwamba sensa ni siku sita hadi saba, hivyo unapaswa kuweka kumbukumbu za watu waliolala usiku wa kuamkia tarehe 23.

Kwahiyo kama nilikuwa nje ya mkoa sintohesabiwa maana sikulala hapo kwenye makazi yangu siku ya tarehe 23? Itabidi nirudi huku nilipolala ndio wanihesabu?
 
Sio kweli, usifananishe zamani na sasa. Hii ni sensa ya kipekee usipange kukosa kwani utajipunja maendeleo

Kwani watu wanafananisha nyakati za sensa au tija ya hiyo sensa? Zoezi linafanyika kijima kupita maelezo. Au zile tablets za kuendeshea hilo zoezi ndio unaona ni kipimo cha ubora wa hilo zoezi?
 
Uko sahihi, hebu nisaidie hili. Leo niko Mwanza kikazi na sijahesabiwa hapa, narudi alhamisi Dar ambako ndiko makazi yangu yalipo. Je sintokuwa na sifa ya kuhesabiwa huko Dar maana sikuamkia huko tarehe 23/8/22?
Hapo Mwanza ulikolala ndio watatoa taarifa zako kwa karani
 
Mbona taarifa ilitoka kwamba sensa ni siku sita hadi saba, hivyo unapaswa kuweka kumbukumbu za watu waliolala usiku wa kuamkia tarehe 23.
Wangekuwa wanatulipa ningeweka hiyo kumbukumbu hata kwa mwaka mzima ujao.
 
Wakati mwingine naona watanzania na serikali yenyewe tuna complicate mambo sana, hata kama mtu asipohesabiwa mwisho wa siku sioni kitakachoongezeka au kupungua kwenye mahitaji ya jamii yetu...
Bwana wee. Sensa kwa nchi zetu hizi hazina umuhimu wowote. Ni globalists tu wanataka random takwimu za kidunia. Maana inatarajiwa watu kufikia 8 B dunuani.

Maana hata tukihesabiwa huwezi pata huduma yoyote bure. Kwetu huku usipokuwa na pesa binafsi utakufa kwa ugonjwa, utalala njaa kwa kukosa chakula, utalala giza kwa kukosa umeme, maiti yako itakwama mortuary kwa kukosa pesa. Bima yenyewe ya afya pamoja na kulipia walitaka utibiwe mara tatu tu kwa mwezi.

Nchi za wenzetu sensa ina maana sababu kupitia kodi mwanachi anapata huduma ya afya, chakula, nishati, na baadhi ya huduma ni free kabisa. Yaani hadi maji ya moto.

Nchi
 
Hapo Mwanza ulikolala ndio watatoa taarifa zako kwa karani

Nani ananijua huku, jana nimelala guest na hakuna aliyenihesabu. Huoni hiyo dhana yako inakosa nguvu kwenye hili? Au hapo watapika Data as usual?
 
Back
Top Bottom