Wapuuzi sana. Kaka ukishayapatia maisha mbona wengine unawaona ni wajinga tuuHawa jamaa ndio wanaokaa na Hela zetu katika mifuko ya hifadhi ya jamii hata pale tunapositishiwa mkababa na mwajiri, Kisha wanatulazimisha tutafute kazi ingine
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wapuuzi sana. Kaka ukishayapatia maisha mbona wengine unawaona ni wajinga tuuHawa jamaa ndio wanaokaa na Hela zetu katika mifuko ya hifadhi ya jamii hata pale tunapositishiwa mkababa na mwajiri, Kisha wanatulazimisha tutafute kazi ingine
Halafu utakuta watoto wa ndugu zake anawachomeka serikaliniNi speaker mstaafu anapata 80% ya stahiki za Spika aliyeko,ni Mwenyekiti wa NHIF iliyofilisika na ni kamisaa wa sensa na upuuzi mwingine..
Majitu kama haya yasiwe yanathubutu hata kunyanyua midomo yao.
Hela ya kubet wanatoa wap? Hivi unaijua michezo ya betting kweli? Kubet inahitaji pesa hata mimi na betWengi wanabet na kucheza michezo ya bahati nasibu ndio ajira pekee waliyonayo kwa sasa hakuna anaependa kukaa bure mtu amesotea elimu zaidi ya miaka 15 usimchukulia poa you must show some respect to them, wamepambana kuitafuta elimu kwa jasho, shida na taabu angalau wameelimika..
Wakishavimbewa,wanapanda "vieite" watajua shida saa ngapi,aliyeshiba hamjui mwenye njaa
Wakati kilio cha watu kukosa ajira hasa kwa vijana kikiendelea kushika kasi, Kamisaa wa Sensa Tanzania Bara, Anne Makinda, amesema kuna idadi kubwa ya wasomi wanaoishi kwa wazazi wao wakila bure kwa kutotaka kufanya shughuli za kuingizia kipato.
Makinda ametoa kauli hiyo leo ijumaa, Septemba 23, 2022 ambapo amesema jambo hilo halifurahishi kwa sababu elimu anayopata mtu anatakiwa aitumie kupambana na mazingira.
"Tumeambiwa kuwa elimu ni ufunguo wa maisha na wala sio ufunguo wa ajira, watu wanahangaika kila kukicha kusaka ajira" amesema
Kamisaa Makinda amesema idadi ya watu inazidi kuongezeka kila kukicha na mbaya zaidi wengi hawafanyi kazi.
“Ni jambo la kushangaza kuona wasomi hawapendi kujishughulisha na vitu vya kuwaingizia kipato, hawafanyi hata biashara wakati wasiosoma wanafanya shughuli za kuingiza kipato” amesema.
Ameongeza kuwa Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwezi uliopita itasaidia kupatikana kwa takwimu zitakazotumika kutunga sera mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Burian, alimweleza Makinda kuwa makarani wa sensa wawili walifariki mkoani humo ambapo mmoja alijiua kutokana na matatizo ya kifamilia na mwingine alifariki akiwa katika nyumba ya wageni aliyofikia baada ya mafunzo ya siku 21.
Amesema mwingine alijeruhiwa baada ya kupata ajali wakati akienda kutuma taarifa za Sensa na mguu wake kushoto kusagika na hivyo kukatwa na hivi sasa wanafanya utaratibu wa kumtafutia mguu wa bandia.
Dk Batilda amesema awali walikadiria kuhesabu kaya 490,000 lakini hasa wanakamilisha walihesabu kaya 577,128 sawa na asilimia 118.
Chanzo: Mwananchi
Yeye mwenyewe baba yake alikuwa rc...so alichomekwa.Halafu utakuta watoto wa ndugu zake anawachomeka serikalini
Anafikiri tukaa nyumbani kwa kupenda au kwamba hatupendi kupata kipatoo.. Huyu bibi bombaaa anazingia tuu mwanawaneNational Anthem mwanawane tunasufwa huku na bibi yetu.
Acha kabisa anatuchukulia sie mafala...nakwambia ukishatoboa kimaisha unaona wengine wajinga kumbe shukuru familia uliyozaliwaAnafikiri tukaa nyumbani kwa kupenda au kwamba hatupendi kupata kipatoo.. Huyu bibi bombaaa anazingia tuu mwanawane
Waswahili wanasema alie shiba hamkumbuki mwenye njaa, kama ana watoto kaisha waweka kwenye position nzuri.. alafu anaanza kunanga watoto wa wenzake.. Tutaendelea kukaa sana kwa nyumbani hatujaua makwetu na wana tutunza na kutupa chakula cha bureeAcha kabisa anatuchukulia sie mafala...nakwambia ukishatoboa kimaisha unaona wengine wajinga kumbe shukuru familia uliyozaliwa
Hivi mimi ndo sijui kuzidisha??
kaya 577,000× 5(wastani wa wanakaya)=2,850,000
kwo kwa haraka tuna watu 2850000 tu??
Ee Myezi Mungu wafanyie wepesi wasomi wote wanaodhalilika kwa kosa ajira, waepushe na masimango wape ujasiri wa kutokujiunga na uhalifu na wajalie afya imara. Amen
Kabla hatujaangalia hiyo mitaala, hebu kwanza tuzitazame tabia za hao wanaowasema watoto wa wakulima wasio na connection.Unahesabiwa ili usimangawe (jokes).
===
Kuna shida kwenye mitaala yetu maneno ya Mama Makinda yapewe uzito unaostaili. Wahitimu wetu wanashindwa kutumia elimu waliyopata kujitengenezea sehemu za kujiingizia kipato. Hili ni tatizo (serious). Litatuliwe.