Makofi mengi bungeni kwa Ndugai yanamaanisha nini?

Makofi mengi bungeni kwa Ndugai yanamaanisha nini?

Nadhani wabunge wote waafiki alichokisema Ndugai juu ya suala la madeni ila tu hawana namna na hawawezi kusema.
Nadhani ukimuuliza mbunge mmojammoja pembeni sio hadharani ataunga mkono hoja ya Ndugai ila kwasababu ya Maslahi hadharani hawezi kusema.
 
Pana mawili kwa mtazamo wangu kwanza labda wabunge walikuwa wanamhitaji bado ili awaongoze maana hawakumpigia kura ili ajiudhuru au yalikuwa makofi ya kama kufrahia kitendo cha kijiudhuru kwake.
 
Moja ya sifa uwapo bungeni hakikisha mahala pakugonga meza pako wazi,Huyu hajavaa vizuri makofi,viuno vya wanaume vimelegea makofi.
 
Sisi binadamu tulivyo hata ufanyiwe jambo gani bado utamuona huyo aliyekufanyia ni mbaya, kuna watu wanasema ni makofi ya heshima, unafiki, kumpongeza n.k pia asingepigiwa makofi bado watu mngeongea tu.
Sisi watu hatuna uelekeo sahihi kila mtu anatapika kilicho mdomoni bila kufikiria ni sahihi au siyo.
 
Mimi ningemuona shujaa Kama asingekanyaga bungeni. Ila kitendo Cha kukanyaga bungeni Ni ishara kuwa ana njaa Sana na anoagopa kufukuzwa bungeni.
Kila post kwetu ni ajira kamili
 
Back
Top Bottom