Mowwo
JF-Expert Member
- Aug 15, 2015
- 1,083
- 1,628
Ripoti za uwezekano wa makombora ya Urusi kulipua kijiji cha Poland yaiamsha NATO.
Watu wawili waliuwawa katika mlipuko huko Przewodow, kijiji cha mashariki mwa Poland karibu na mpaka wa Ukraine. Poland wamesema washirika wa NATO wanachunguza ripoti endapo mlipuko huo ulitokana na makombora ya Urusi.
Shirika la habari la Associated Press hapo awali lilimnukuu afisa mkuu wa Kijasusi wa Marekani akisema mlipuko huo ulitokana na makombora ya Urusi kuvuka hadi Poland.
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imekanusha ripoti kwamba makombora ya Urusi yamepiga eneo la Poland, na kuyataja kama "uchochezi wa makusudi unaolenga kuichafua urusi"
Poland ni mshirika wa NATO. Je NATO akiingilia kati itayokea vita ya tatu ya dunia?