Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Migogoro mikubwa nchi hii inahusu ardhi. Polisi, Mahakama.

Ni hivi, kigogo anachukua ardhi yako, ardhi ya mama yako, ardhi ya yatima, mjane, analindwa na polisi, mahakama.

Unafanyaje?
 
Hii kauli sijaielewa chama kikubwa kuliko serikali? Yaani CCM ni Kubwa kuliko wananchi wenye nchi yao ?
Wananchi ndio walioichagua serikali kupitia chama ambacho ni CCM.kwa hiyo serikali ikifanya vibaya ,wanchi wao watakuja kukiadhibu chama kupitia sanduku la kura kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake na mkataba wake unaoitwa ilani ya uchaguzi.kwa hiyo ni lazima chama kihakikishe ya kuwa kinasimamia vyema serikali yake katika utekelezaji wa ilani.
 
Kuna sehemu nimesema chama kinapaswa kukaa kimya? Si umeona ulivyo na matatizo ya kuelewa?

Narudia tena, Makonda kama mtumishi wa Chama hana mamlaka yoyote ya kuwasimamisha watumishi wa Umma au kuwapigia simu majukwaani na kutaka maelezo yao na kuwapa amri.

Chama kinafanya hivyo kupitia vikao. Nyie endeleeni kuhalalisha ujinga kwakuwa ni wajinga ila msilazimishe watu kuamini na kuuishi ujinga wenu.
 
Itakua ni ufala kumtumbua Bashe kwa ajili ya falla Bashite.
Bashe anajua anachokifanya lkn Bashiboy anasaka tonge na umaarufu
Mheshimiwa Makonda ni maarufu sana na mwenye jina kubwa sana katika nchi hii.kwa hiyo hana sababu ya kutafuta umaarufu mwingine zaidi ya huo alio nao kwa sasa.
 
Mwambie Basi Bashe kama hataki kuulizwa na chama na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayogusa wizara yake basi ajiuzulu hataleo tu ili Mheshimiwa Rais wetu mpendwa ateue mtu mwingine.
 
Wanatuadaha Kwa mambo Yao ya kipuuzi huku ya kwao yakitimia na kuendelea kuzitafuna Kodi zetu tukija shtuka tumepigwa siku mingi wao wanagonga chiazi za mvinyo wa bei ghali toka ufaransa!!
Watu wengi sana hawawezi kuliona hili.
 
 
Aliyemrudisha Bashite kwenye siasa ndo atajibu kwa Mungu wetu wa mbinguni. Sick!!!!!
 

makonda anakubalika na wananchi kuliko bashe!!

Makonda anagusa hisia za watu

Hakunaga mashindano ya hisia na Akili mzee !!
Hisia muda wote hushinda akili[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mwenezi ndie boss wa mawazir wote hawataki watenganishe serikali na chama
 
Bashe anakiburi sana mwendie Makonda ananyota Kali sana mwanza uko kashangiliwa kuliko ata Nchimbi
 
Mwenezi ndie boss wa mawazir wote hawataki watenganishe serikali na chama
Waziri anayeona hawezi kuagizwa na chama basi Aachie uwaziri haraka sana ili Mheshimiwa Rais wetu mpendwa ateue mtu mwingine.maana chama kina watu wengi sana wanaoweza kuwa mawaziri.kwa hiyo asije waziri akajiona kama Mungu mtu.

Nampa angalizo Bashe kuwa asilete ujuaji na dharau kwa chama.asije hisi ana akili sana.kama anataka akae pembeni .
 
Bashe anakiburi sana mwendie Makonda ananyota Kali sana mwanza uko kashangiliwa kuliko ata Nchimbi
Tena siyuletee kiburi hapa.mheshimiwa Makonda ananitafutia Mheshimiwa Rais kura za ushindi mwakani.halafu yeye anaanza kuleta majibu ya dharau mpaka eti anapindisha mdomo.kama hataki basi akae pembeni huko.
 
Bashe keshachoka uwaziri. Anatamani kuwa back bencher
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…