Pre GE2025 Makonda amjibu Waziri Bashe, asema atamhoji sababu yeye ndiye anakitafutia kura chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
waaambie hapana chezea sukuma gang
 
Hebu kwanza tumalize hili mkuu kwa urahisi tu. Halafu sina hasira yoyote, umesoma tu ujumbe wangu kwa hasira.

Waziri hapa Tanzania anapokea amri kwaajili ya utekelezaji kutoka kwa nani?
 
Bashe Kawa akili kubwa lini? Mbona nyie CHAWA mmejazwa humu na wahuni?
 
Hebu kwanza tumalize hili mkuu kwa urahisi tu. Halafu sina hasira yoyote, umesoma tu ujumbe wangu kwa hasira.

Waziri hapa Tanzania anapokea amri kwaajili ya utekelezaji kutoka kwa nani?
Soft tune. Hongera
Waziri ni mwanasiasa anayepokea kutoka mamlaka ya uteuzi kusimamia shughuli zote za serkali iliyopo madarakani ambayo ipo hapo kupitia siasa.
Nimejibu kifupi. Kama nime hit the bush. Niambie
 
Soft tune. Hongera
Waziri ni mwanasiasa anayepokea kutoka mamlaka ya uteuzi kusimamia shughuli zote za serkali iliyopo madarakani ambayo ipo hapo kupitia siasa.
Nimejibu kifupi. Kama nime hit the bush. Niambie
Ndio mkuu, umezunguka sana na wakati jibu lilipaswa kuwa jepesi tu.
 
Ccm.ktk kufanya watu wawazungumzie tu wako vzr iwe kwa baya au kwa zuri .wao wanachotaka ni kuwa hewani tu
 
Bashe aache Kiburi na kujifanya anajua
Sio anajifanya anajua, Bashe ni smart. Ana mapungufu tu ya kibinadamu na siasa zetu, ila kumlinganisha Bashe na Makonda ni kulinganisha Jigga na Joh Makini.
 
Bashe akili kubwa???? Basi kama akili kubwa ndio hio nchi itakua imejaa vilaza.Maana kwenye kundi la vilaza, kilaza wa juu anaonekana Akili kubwa.
 
Acha kumpa kiburi kisicho na msingi.yeye hayupo juu ya chama na ni lazima Bashe akiheshimu Chama san.asilete kiburi na jeuri kwa chama na viongozi wa chama
 
Mkuu. Kwani waziri sio mwanasiasa? Chama kikimvua uanachama atabaki waziri?
Mkuu, sasa sijui tafsiri nzuri ya mwanasiasa, ila naona bado unazunguka.

Labda turahisishe iwe hivi, naamini wewe ni mtu na akili zako nzuri tu.

Mamlaka ya uteuzi ya waziri ni Rais, na anafanya hivyo kwa kushauriana na Waziri Mkuu na Makamu.

Rais ni rais kwasababu alidhaminiwa na chama cha siasa kugombea nafasi hiyo.

Rais akiisha kushinda uchaguzi, anakabiliwa na jukumu la kuunda serikali na hapo atatafuta Mwanasheria mkuu, atateua waziri mkuu kutoka katika chama chenye wabunge wengi bungeni. Na baada ya hapo atateua Mawaziri wake ( akina Bashe hao)

Katika zoezi hili la kuteua mawaziri, Rais haingiliwi na Chama chake, ni busara zake na kuona wapi aweke nani na nani anamfaa wapi!

Hivyo basi, nyie kama chama hamjui amepata vipi watu wa kumsaidia kufanya kazi zake yeye kama mtu mliyemdhamini kuupata urais.

Rais sasa ndio ana mamlaka ya kuwatuma na kuwaambia wafanye nini na wakati gani, hata Waziri mkuu akitoa maagizo kwa mawaziri anatoa kwa mamlaka aliyopewa na Rais.

Sasa tuelewane nataka kusema nini, Chama kilichomdhamini Rais kama kina madukuduku na maelekezo hayo anapewa mtu wao waliyemdhamini akawa Rais na sio kuanza kuwaita na kuwahoji watumishi wa Umma.

Sasa wewe Omulasil ungekuwa mbunge kwa kudhaminiwa na Chama, na kisha Rais akakuona akakupa uwaziri, hapo chama kinauwezo wa kukuwajibisha wewe kama mbunge kwa kazi zako za kibunge na sio uwaziri wako.

Hapa sasa tusipoelewana sijui shida itakuwa wapi.
 
nafikiri kiongozi safi na makini hachagui wa kumuhoji hata mlala hoi anapaswa kumuhoji bila ya kunyanyua mabega
 
πŸ™πŸ™πŸ‘
 
Dah kabisaa...ni sawa na uweke plan...na katika plan uweke tena plan ambayo hiyo plan hutaitekeleza na kufanya plan nyingine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…