Makonda anaufedhehesha muhimili wa Mahakama; Hana madaraka lakini Mahakama inamtii

Makonda anaufedhehesha muhimili wa Mahakama; Hana madaraka lakini Mahakama inamtii

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Mahakama ya Tanzania Sijui imekosa nguvu Kwa sababu ya chama au Kwa sababu ya serikali au Jaji mkuu ameshindwa kuwapa Imani waliopo chini yake?

Raia anaitwa na Mahakama yupo Kigamboni au Masaki anagoma kufikia mahakani Wala kutuma mwakilishi na uongozi wa Mahakama upo kimya.

Hakimu anadai anapeleka tangazo kwenye mbao za matangazo na nyumbani Kwa mtuhumiwa. Je, watuhumiwa wote wanafanyiwa haya? Au Kuna watanzania daraja A na B?

Mahakama inalega Hadi wanyonge wanaiona siyo sehemu ya HAKI. Polisi wapo, wanashindwa kumkamata?
 
Ni kweli kuwa Mahakama zetu kwa kiasi fulani hazina meno kwa watu fulani LAKINI katika hili sioni tatizo.

Makonda ni mtuhumiwa lakini barua ya wito haijamfikia kwa kuwa hakuna aliyemuona ili amkabidhi wito rasmi.

Hatua iliyochukuliwa ili wito umfikie kwasasa ni sahihi.

Baada ya tangazo gazeti, kitakachofuata ni kutafutwa na polisi popote alipo.

Nafikiri kwa hili sio sahihi kuilamu mahakama.

Katika sheria mimi ni sawa na ngumbaro tu.
 
Unaelewa ulichoandika ni upotoshaji mkubwa sana wa namna utaratibu wa kumuita mtu mahakamani hufanyika kwenye kesi ?

Aliyefungua kesi ni kubenea, mtu hitafutwa na ofisa wa Mahakama apewe copy ya wito pamoja na documents ambazo zimekuwa files mahakamani ili nae aweze kuandaa majibu na kufaili mahakamani.

Huyu hajapata wito ambapo imekuwa ngumu kumpata ndio maana imetoa amri kwamba Ile summons iwekwe magazetini na huo bado ndio utaratibu Sheria inavyotaka.

Baada ya hapo asipoonekana kesi itasikilizwa ex parte (upande mmoja ) na hukumu itatoka dhidi yake . Sasa ikishatoka hukumu Ina maana mnaikazia hukumu anageuka kuwa convict na inachoendelea ni kumsaka na kumpeleka jela.

Sasa ulichoandika hapa its a big lie na huu ni kujidhalilisha Mahakama. Nakushauri ufute huu uzi
 
Hiyo ndio first step kisheria iliyofanywa na mahakama, kuacha copy ya wito wa kuitwa mahakamani sehemu zote ambazo amezoeleka kuwepo, muda wa kufika mahakama na tarehe vyote vipo kwenye huo wito.

Akikaidi hapo ndio ataanza kutafutwa na polisi nchi nzima baada ya mahakama kutoa amri, binafsi namuona Makonda mjinga ameifanya hii issue iwe kubwa bila sababu na italeta attention zaidi kwa public kwa huu ujinga wa kutofika mahakamani alioufanya.
 
Mkuu kabla ya kuandika bandiko la kuishutumu na kuidhalilisha mahakama unapaswa kwanza kufahamu taratibu za mahakama katika kuendesha mashauri.

Nikushauri tu mkuu sio vyema kupotosha na kuzua taharuki bila sababu kwa porojo ambazo kwa kweli hazina uhalisia wowote.

Fahamu kwamba kesi iliyopo mahakamani ni ya kuomba kibali tu na sio kwamba eti ndio mashtaka rasmi yamewasilishwa??

Pia hatua ya sasa ni kuhakikisha kwamba moja wapo ya watu muhimu (makonda) anashiriki hatua hii muhimu.

Mtu anapopelekewa wito na hapatikani huwa kunakuwepo na namna ya kufanya ili taarifa ya kuhitajika mahakamani imfikie.

Hata hivyo uwepo wa mtu mahakamani kwa mashauri ya aina hiyo sio lazima sana kwani anaweza wakilishwa na mtu yeyote atayemchagua ikiwemo wakili wake ama la mahakama itakapomhitaji yeye mwenyewe.

Mpaka hapo ukae ukitulia na kuiacha mahakama ifanye kazi yake.

Kama hujui jambo ULIZA.
 
Tusubiri ya Jacobo Zuma yalio jiri South Afrika
Vigezo na masharti kuzingatiwa
Ndege tunduni huyoooo!
Ushauri wangu kesho Bashite nenda kwa Pilato mwenyewe!!
 
Mimi nona muhimili wa mahakama ndio umejifedhehesha wenyewee.
 
Hiyo ndio first step kisheria iliyofanywa na mahakama, kuacha copy ya wito wa kuitwa mahakamani sehemu zote ambazo amezoeleka kuwepo, muda wa kufika mahakama na tarehe vyote vipo kwenye huo wito.

Akikaidi hapo ndio ataanza kutafutwa na polisi nchi nzima baada ya mahakama kutoa amri, binafsi namuona Makonda mjinga ameifanya hii issue iwe kubwa bila sababu na italeta attention zaidi kwa public kwa huu ujinga wa kutofika mahakamani alioufanya.
Makonda hajawai kuwa mwerevu, ni mjinga kitambo
 
Unaelewa ulichoandika ni upotoshaji mkubwa sana wa namna utaratibu wa kumuita mtu mahakamani hufanyika kwenye kesi ?

Aliyefungua kesi ni kubenea, mtu hitafutwa na ofisa wa Mahakama apewe copy ya wito pamoja na documents ambazo zimekuwa files mahakamani ili nae aweze kuandaa majibu na kufaili mahakamani.

Huyu hajapata wito ambapo imekuwa ngumu kumpata ndio maana imetoa amri kwamba Ile summons iwekwe magazetini na huo bado ndio utaratibu Sheria inavyotaka.

Baada ya hapo asipoonekana kesi itasikilizwa ex parte (upande mmoja ) na hukumu itatoka dhidi yake . Sasa ikishatoka hukumu Ina maana mnaikazia hukumu anageuka kuwa convict na inachoendelea ni kumsaka na kumpeleka jela.

Sasa ulichoandika hapa its a big lie na huu ni kujidhalilisha Mahakama. Nakushauri ufute huu uzi
Acha UCHAWA ,Jacob Zuma alikaidi wito wa mahakama,hatimaye mahakama ikatoa amri akamatwe.
 
Back
Top Bottom