Makonda anaufedhehesha muhimili wa Mahakama; Hana madaraka lakini Mahakama inamtii

Makonda anaufedhehesha muhimili wa Mahakama; Hana madaraka lakini Mahakama inamtii

Makonda alimtabiria SSH huu urais alionao sasa. Aliiva vizuri na rais mtarajiwa. Kama ulikuwa ni shabiki mmojawapo wa wale walionyanyaswa na JPM jipange haswa.

Nadhani nguvu ya rais aliyeapa umeshaiona kwa Ndugai na jeuri yake yote ya awamu ya tano. Rais anayekuwa ameapa ana nguvu na ushawishi mwingi sana.
 
Kwa hiyo mpaka muda huu Mahakama bado ina-act on his favour, kwa lengo la kumuepusha na hukumu ya inayoweza kutokana na kusilkilizwa kwa upande mmoja, na ambayo inaweza ikaja ikawa ina madhara makubwa kwake, just in case.

Katika hali hii, kuonekana kwake ni bora zaidi kuliko kuendelea kujificha, unless kama ana uhakika kabisa kuwa ataendelea kujificha moja kwa moja maisha yake yote pasipo kukamatwa
 
Ni kweli kuwa Mahakama zetu kwa kiasi fulani hazina meno kwa watu fulani LAKINI katika hili sioni tatizo.

Makonda ni mtuhumiwa lakini barua ya wito haijamfikia kwa kuwa hakuna aliyemuona ili amkabidhi wito rasmi...
Baada ya hapo kesi itaendelea upande mmoja, polisi hawatahusika kumtafuta wala kumkamata

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Naona sasa ameamua kujificha kabisa.....
 
Mahakama za mchongo tangu lini zikawa na weledi , yani hata shauri la kuiba kuku lazima waombe ushauri kutoka juu, shame on us all
 
Bashite anawachora tu mahakama

Makonda.JPG
 
Acha UCHAWA ,Jacob Zuma alikaidi wito wa mahakama,hatimaye mahakama ikatoa amri akamatwe.
Tatizo haujataka kusoma uelewe nyie watoto wa siku hizi.

Nimeeleza utaratibu wa kimahakama ambao ndio upo kisheria kuonyesha namna gani Mahakama ipo sahihi .

Hata huyo Zuma hawakutoa hati ya kumkamata hebu kasome utaelewa hiyo amri ilifuata baada ya kudharau Mahakama aliitwa Mara tatu na akatafutwa kwa magazeti hakutokea.

Unapaswa kufuatilia mambo hata Kama hauna elimu jielimishe unaongea na mtu anayeshinda Mahakamani young man haikusaidii kuwa keyboard hero, nobody knows you out here.
 
Ni kweli kuwa Mahakama zetu kwa kiasi fulani hazina meno kwa watu fulani LAKINI katika hili sioni tatizo.

Makonda ni mtuhumiwa lakini barua ya wito haijamfikia kwa kuwa hakuna aliyemuona ili amkabidhi wito rasmi.

Hatua iliyochukuliwa ili wito umfikie kwasasa ni sahihi.

Baada ya tangazo gazeti, kitakachofuata ni kutafutwa na polisi popote alipo.

Nafikiri kwa hili sio sahihi kuilamu mahakama.

Katika sheria mimi ni sawa na ngumbaro tu.
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu, mahakama huwa haikurupuki katka mahamuzi yake
 
Mahakama ya Tanzania Sijui imekosa nguvu Kwa sababu ya chama au Kwa sababu ya serikali au Jaji mkuu ameshindwa kuwapa Imani waliopo chini yake?

Raia anaitwa na Mahakama yupo Kigamboni au Masaki anagoma kufikia mahakani Wala kutuma mwakilishi na uongozi wa Mahakama upo kimya.

Hakimu anadai anapeleka tangazo kwenye mbao za matangazo na nyumbani Kwa mtuhumiwa. Je, watuhumiwa wote wanafanyiwa haya? Au Kuna watanzania daraja A na B?

Mahakama inalega Hadi wanyonge wanaiona siyo sehemu ya HAKI. Polisi wapo, wanashindwa kumkamata?
Mnalaumu mhimili bila sababu yoyote. Raia kibao wanaitwa mahakamani wanaingia mitini. Sio jambo jipya hilo. Huonagi kwenye magazeti wito wa kuitwa mahakamani? Mara nyingi hao huwa wamekula kona baada ya kutafutwa kwa njia za kawaida. unaona ni jambo jipya kwa sababu linahusu mtu prominent!
 
Katiba Mpya muhimu sana.

Unaona huko Dodoma wanataka kupitisha mswada wa kuwalinda Polisi dhidi ya uovu.
 
Ila hata Musiba aligoma kwenda mahakamani Zenji akasema haitambui, ila mashehe wa uamsho walishtakiwa bara
 
Tutofautishe Kati ya kesi ya jinai na kesi ya madai hapo ndiyo tutajua nini mahakama inamwogopa au laa.
 
Wiki mbili zilizopita tulikuwa naye Kijijini Kolomije kwenye msiba wa Ndugu yake mmoja hivi
 
Sina ufahamu, ila kwa akili ya kawaida, ukiitwa na mahakana na ukakaidi unafuatwa na pingu. Ninayaona katika mahakana za mwanzo. Labda za juu ni tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa ni mchawi sana anayejificha kwenye mwavuli wa ulokole.

Aliharibu nyumba ya Mzee Sitta, nyumba ya Mkwere, Magu etc.

Jamaa ameshampumbaza akili Farisayo Mkuu
Alitembea na wake zao, sivyo? Hebu ieleze vizuri Mahakama Mkuu.
 
Makonda alimtabiria SSH huu urais alionao sasa. Aliiva vizuri na rais mtarajiwa. Kama ulikuwa ni shabiki mmojawapo wa wale walionyanyaswa na JPM jipange haswa.

Nadhani nguvu ya rais aliyeapa umeshaiona kwa Ndugai na jeuri yake yote ya awamu ya tano. Rais anayekuwa ameapa ana nguvu na ushawishi mwingi sana.
Mbona ye hakujitabiria kuwa ataishi mapangoni,
 
Back
Top Bottom