Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu

Makonda ashtakiwe kwa udhalilishaji alioufanya kwa mwanakamati huyu

Ale kodi asile,wakati mwingine serikali inajiaibisha. Anajisikia sana na kujiona wa maana, kana kwamba hana mifano. Kiongozi mwenye busara,hawezi kulopoka ovyo vitu kama hivo. Hata kama ni utani,angetania kiutani si kashfa nzito hivo.
 
Aliambiwa mara nyingi aongeze sauti.Wacheni kutetea ujinga.Unapotakiwa kutoa maelezo ili wananchi wakusikie inabidi uzungumze kwa sauti ili usikike.Alihimizwa azungumze kwa sauti mara zaidi ya mbili akawa anarudia vile vile.
Kurudia vile,kunahusiana na nini na mchumba? Mke mzuri,ameongelewa kusaidia nini kwenye hizo hoja? Anamzidi yupi hapo? Aongeae hapo nae ni mzuri kwa mtu mwingine
 
Watanzania wamepata mada ya kupotezea muda. Watz hawana muda wa kuzalisha ni wavivu na majobless. Wamepata jambo la kutumia bando. Hamna udhalilishaji pale. Kile chama kilichotoa tamko nacho hakina agenda na vitu vya kufanya.
 
😂😂😂 we mzalishaji kazalishe uwape kazi majobless.
 
Ingekuwa nchi zinazojitambua angeshajiuzulu asubuhi ya leo
 
Akiwa kwenye ziara yake Longido, Makonda kama kawaida yake akiwa anatatua kero za wananchi, kamati hii ilihojiwa sababu ya ujenzi wa shule kusuasua.

Wakati mwanakamati huyo anajieleza Makonda alimwamvia haongei na mchumba wakw bali wananchi, nina mke mzuri nyumbani!

Kwamba alokuwa anaongea kwa lengo la kumtega? Na yeye angemjibu nina mume handsome nyumani angekuwa amekosea? Maadili ya kazi yanasemaje? Hata kama unamhoji mtu ameiba ndio unatakiwa umdhalilishe namna hiyo?

Chuki tu hizo
 
  • Thanks
Reactions: Tui
nimejaribu kutafuta kosa mnalomtuhumu Makonda silioni yaani mnataka kiongozi wa kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa, hamkuwahi kufanya kazi na General Kiwelu ukizingua hata makofi alikuwa anakuweka, yeye alikuwa anaonyesha ishara kwa fimbo ole wako usifuate, kazini alikuwa wa kwanza ofisini saa 1 asubuhi ole wako uchelewe,, lakini ni mkuu wa mkoa pekee anayekumbukwa zaidi kwa reform ya mkoa wa Rukwa, tunahitaji viongozi ambao hawarembi kama hawa, tena siku hizi walau amepunguza kidogo anaongea kwa unyenyekevu, unaona kabisa mtu anamakosa halafu anaonyesha nyodo hata mie namwasha makofi watu wako wanaibiwa halafu wewe unamchekea nyani utavuna mabua na ndicho kinawaangusha viongozi wengi kutaka kujifanya wanabalance ili wasionekane wabaya.
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
Akiwa kwenye ziara yake Longido, Makonda kama kawaida yake akiwa anatatua kero za wananchi, kamati hii ilihojiwa sababu ya ujenzi wa shule kusuasua.

Wakati mwanakamati huyo anajieleza Makonda alimwamvia haongei na mchumba wakw bali wananchi, nina mke mzuri nyumbani!

Kwamba alokuwa anaongea kwa lengo la kumtega? Na yeye angemjibu nina mume handsome nyumani angekuwa amekosea? Maadili ya kazi yanasemaje? Hata kama unamhoji mtu ameiba ndio unatakiwa umdhalilishe namna hiyo?

Atashutakiwa na nani?
Vyeti feki hakuguswa itakuwa hiyo ya kunyanyasa?

Hii nchi kuna mambo ya ajabu sana ya kulindana.
Makonda Kwanza Kwa uchafu alioufanya hakutakiwa abakie kwenye ofisi za walipa kodi wa nchi hii.
 
Kila kitu kina utaratibu wake, kama alikuwa hamsikii angemwambia kistaarabu aongeze sauti, sio kumjibu kama alivyomjibu
Kinacho mtafuna Makonda ni malezi yake utotoni na malezi aliyopewa na Jiwe.

Anajiona kama yupo huru kufanya lolote na asiguswe ila na viongozi wetu wakuu inabidi wajitafakali kwenye kufanya teuzi.
 
Huyo baba ni mjomba wako?
Hujisikii aibu kumtetea? Au hujaona hiyo clip?
Kuna watu wana sauti ndogo sana
Anamwambiaji aongeze sauti sjui asimrembee km anatoa posa bla bla mke wake this mke that. Vina mahusiano gani ktk mahojiano??
Angemwambia tu weka maiki vizuri mdomoni ili usikike, asingeeleweka?
Hao ndiyo vijana wa lumumba wao kazi yao ni kuwatetea wanaoyatimba
 
Tulishasema mara nyingi watu huwa hawasikii. Hii iko nje ya maadili ya utumishi na sio uungwana kumtamkia mtu yoyote hadharani maneno kama hayo. Kisa tu kutaka vigelegele vya wananchi kwa maneno yako machafu.

Shame! Shame! Shame!
 
Back
Top Bottom