Msamaria ni mtu anayejitoa kumsaidia mhitaji, si kwamba anaweza akawa anacho kikubwa la hasha bali ni mtu aliyejaaliwa kutoa kwa ajili ya wengine na kama hana basi hata kufanya mipango ya kupata kwa mwingine ama wengine.... Wasamaria ni watu wa kaliba ya aina yao...kwakuwa hawa ni tofauti kabisa na wahisani na wafadhili... Wanaotoa kwa malengo maalum
Kama taifa tu vijana wetu, ndugu zetu jamaa na watanzania wenzetu walioko nje ya nchi... Ughaibuni! Hawa kati yao kuna wanaosoma na wengine ni wafanyabiashara, wafanyakazi nk... Hawa ni watu wanaofahamu kwa undani matatizo ya nyumbani na kuguswa vilivyo nayo...
Ni hawa ndugu zetu kupitia vyama vyao (diasaporas) nk wamekuwa wakijitoa kusaidia nyumbani kwa hali na mali kwa kile kidogo wanachopata..hasa kwenye majanga na dharura za nchi.. Kiukweli tumeona juhudi na jitihada zao na kutowashukuru ni kukosa shukrani
Kwenye msafara wa mamba kenge pia wamo.... Pamoja na sifa zote hizo lakini kuna wakati huwa ndugu zetu hawa wanatumika vibaya na pengine bila wenyewe kufahamu
Sakata la makontena 36 yaliyojaaa samani za shule lina sura nyingi za kuchanganya, kuvutia na kuchukiza pia... Mijadala imekuwa mingi lakini naamini kuna maswali ya msingi mpaka sasa hayajaulizwa.. Ngoja tuyapitie baadhi
. Chama cha wasamaria wetu waliotoa huo msaada kinasemaje? Mbona wako kimya? Au hawaguswi na msaada wao kuwa na danadana na sintofahamu nyingi?
. Kwa mzigo mkubwa kama ule kwa hakika pesa iliyotumika si haba na wahisani waliochanga wako vizuri... Hivi hawana uchungu wa kuhoji chochote?
. Wakati wa bakuli la mchango kupita, je walijulishwa kwamba wanachangia shule za Dar tu!? Nina hakika si wote wanatoka Dar
. Je wakati wa kupitisha bakuli la mchango waliambiwa kwamba wanamchangia mtu halafu akawakilishe au wanachangia taasisi?
. Je waliridhia shehena ya mzigo waliojichangisha kwa ajili ya shule za serikali uandikwe jina na anuani binafsi?
. Kama baada ya kuhangaika kote huko na kufanikiwa kupata samani zilizojaza makontena 36, je Kwanini sasa wako kimya kabisa!? Kama waliweza kula ng'ombe mzima Kwanini washindwe na mkia?
. Swali la mwisho.. Yako wapi makontena 16 ya mwanzo yaliyofanikiwa kutolewa? Je kuna shule zilifanikiwa kupata chochote?
Mwisho mamlaka husika zingejitokeza kutoa ufafanuzi kwenye hili kuliko kuliachia lielee tu na kusambaa kiholela kila mtu akiongea lake
Hili litasaidia mno kuondoa sintofahamu iliyojitokeza na pia kutowavunja moyo wahisani wengine hapo mbeleni lakini kubwa kuliko yote kuipa serikali heshima inayostahili na kuiepusha kutumiwa vibaya na wapuuzi wachache
Jr[emoji769]