Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Me napendekeza wana jf tujichange tuyanunue...kwan bei gani!??

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaaaaa mkuu umetisha kama vipi tuchange tu halafu tuyanunue JF ina members mamilioni kila mtu buku 10000 tunayanunua halafu tunagawa kwa watoto yatima basi ...................@Maxence Melo ahamasishe hii kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bashitee bhanaa mwanzoni aliyakanaa kabisaa hayoo makontenaaa.... Leo anaanza kulialiaa tenaa Kanisanii serious!!???? Huyu jamaa anamatatizo ya Akilii... Alafuu hao TRA Kama Laana wanapewaa Kilaa sikuu tena zinginee za halali maana wanafanya fitina za wazii kwa wanyongeee....Sasa Bashitee na hips zileee atuliee tuu asitakee hurumaa za Jiwee....fwakeniii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda laana kwa hisani ya Mungu Baali Jiwe wa Chattle kiongozi uchwara wa Malaika wote


lakini mbona huyu 0 anaachwa si apigwe chini tu jamani
 
Anaweweseka huyu si bure na anavyopenda kulialia sasa.
Kila mmoja wetu ataonja adha ya utawala huu kwa wakati wake. Kwanini hamlilii Malaika wa Mungu akamsaidia maana kwenda kulia kanisani ni kuonyesha kuwa amemsahau huyo malaika anaishi wapi. Yupo Ikulu ya Tanzania, tena kwenye mkoa wake, wa Dar-Es-salaam.
 
Taarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.

Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.

Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?

Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.

Kazi njema wakuu wote!
 
Back
Top Bottom