Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Haya maneno aliyasemea kanisani au nje baada ya hiyo ibada? Kama alipewa nafasi kutoa utumbo huu kanisani.....nashindwa hata nisemeje kwa kweli.
 
conformation. kilichomo kwenye makontena ya makonda pale bandarini ni fenicha za hotel yake hapo mwanza.. ndo mana kil siku tunasema huyo anayeitwa mwadilifu sio mwadilifu sio hivyo.tuone kwenye hili atafanyaje?
Tuwekee picha ya hotel yake
 
Mkuu ina maana wewe vitu vyako vikipigwa mnada utakaa kimya?
Umesikia huu ndio mnada wa kwanza kufanyika?
minada yooote inayofanyika huko hutangazwa je umemsikia nani anapayuka mpaka kuomba msaada kwa maaskofu wamuombee je na wengine nao wamuige huyu bashite kupayuka kama unavotaka??? mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu😕😕😕😡
 
Hakuna mcha Mungu hata mmoja aliye mwepesi kuomba laana imfikie adui yake. Ni shetani tu na wafuasi wake ndo wenye tabia na roho ya namna hii sababu ya kujwa na kiburi kilichopitiiza. Lakini ukiona mtu anaanza kusema sawa tu Mungu anakuona ujue anaashiria kukata tamaa na ni dalili za kushindwa na kulemewa katika vita. Kuna siku niliwahi kuandika humuhumu ya kuwa watu wengi tu wanakamatwa na kuteswa polisi na kupelekwa mahakani kwa madai ya kutoa lugha za uchochezi lakini huyu jamaa siku zote amekuwa akiwatukana watu hadharani kuwaita wajinga wapumbavu na kuwadharau hata watu wazima na hachukuliwi hatua. Nadhani sheria za Tanzania sio moja kwa kila mtu, yaani nataka kusema watanzania wote tuko sawa mbele ya sheria lakini wengine wako sawa zaidi. Sina hela tu, ningekuwa nazo ningeenda kununua vitu vyote hivyo niione hiyo laana ya Mungu wake mpenda visasi na uonevu. LEO NIMEPATA SOMO ZURI SANA. KUMBE KILA BINADAMU HUWA ANATENGENEZA MUNGU WAKE MWENYEWE KULINGANA NA MAHITAJI YAKE!!!!! SITASHANGAA KUSIKIA NA MAJAMBAZI NAO WANAMUOMBA MUNGU WAO KABLA YA KWENDA KUKABA
 
conformation. kilichomo kwenye makontena ya makonda pale bandarini ni fenicha za hotel yake hapo mwanza.. ndo mana kil siku tunasema huyo anayeitwa mwadilifu sio mwadilifu sio hivyo.tuone kwenye hili atafanyaje?
nimekusoma... tangulia PUB agizia kesto bardiiiiiiiiii 3 wambie nakuja kulipa😛
 
Taarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.

Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.

Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?

Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.

Kazi njema wakuu wote!
Kama kweli ni vifaa vya mashuleni basi TEA walipie hizo kodi na kugawa kwenye shule zenye mahitaji ya vifaa hivyo
 
Back
Top Bottom