Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Makonda: Atakayenunua makontena yangu atalaaniwa yeye na kizazi chake! Atoa onyo kwa atakayethubutu kununua

Movies tu izi tuendelee kuangalia si ndo tumechagua haya maneno
 
Sheria ni msumeno atii bila kulialia hata aende wap yatapigwa mnada tu namba moja wakimwambia huyu mtu hafai anamtetea ona sasa anavyomuabisha masuala ya kodi na kanisani wap na wap jamani?
 
Taarifa huripotiwa kwenye vyombo vya habari kama runinga, redio, magazeti, majarida na mitandao ya kijamii. Iliporipotiwa taarifa ya uingizwaji na uwepo wa makontena yenye jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwanzoni iliripotiwa kuwa Makonda 'aliyakana' makontena hayo.

Baadaye, ripoti zinadokeza kuwa RC Makonda 'aliyatambua' makontena hayo yaliyokuwa mikononi mwa TRA na kudai kuwa yalikuwa na samani za shule za mkoa wa Dar es Salaam. 'Akatishia' hata 'kuwashtaki' TRA kwa Rais. Mambo yakawa kimya hadi sasa inaporipotiwa kuwa TRA wamejaribu kuyapiga mnada bila mafanikio.

Sasa inaarifiwa kuwa RC Makonda amekwenda kanisani 'kufanya maombi maalum' ya kukwamisha mnada wa makontena yake. Ametishia kuwa yeyote ambaye atayanunua atapata laana! Kimsingi, ni Dhahiri sasa kuwa RC Makonda anayatambua na kuyapigania makontena yake. Makontena hayo yana nini hasa? Kwanini yalikuja kwa jina lake?

Namsihi RC Makonda, katika hili la makontena yanayoshikiliwa na TRA, aeleweke. Aiache TRA ifanye kazi yake na si kutaka kuionyesha TRA kama iliyo kwenye 'mission' naye kuyahusu hayo makontena. Mnada ufanyike na mambo mengine yaendelee. Namsihi RC Makonda kuacha pia kuwatisha 'kimaombi' wateja wanaotaka kuyanunua makontena hayo.

Kazi njema wakuu wote!
Wewe ni mwansheria uchwara kama uchwara yoyote yule. Mhalifu aliyetishia vyombo vya serikali vinavyotekeleza majukumu yake anaombwa? Siyo kuwa anachukuliwa sheria?
 
Wapinzani uchwara walikuwa wanasema ati makontena yamejaa samani za majumbani pamoja na Toyota SUV moja,lakini kwa sasa yameshafunguliwa wamekuwa wakimya sana...Wapinzani Uchwara acheni fitna.
Nenda kanisani ukasaidie kulia, acha kelele zisizo na msingi hapa
 
Kwan makonda ni nan hasa kias kwamba awanyime uhuru taasisi kubwa ya kiserikali kufanya kazi zake kwa uhuru?

Kuna mambo mengine viongoz Wetu wanafanya kias kwamba unajiuliza uyu mpaka leo anafanya nin kwann asipangiwe kazi nyingine ya kufanya au apigwe tuu chin..!!!!

Uyo jamaa kwa jinsi magu anavyo mlea ipo siku atakuja toa kauli za dhiaka kwa rais na uwongoz wake....

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli ni kwamba raia yeyote anayeingilia mnada wa TRA (katika kukusanya madeni ya kodi) na kuwatisha washiriki wasinunue bidhaa kwenye mnada anafanya kosa la jinai.
Ninaamini angekuwa ni sisi kina yakhe tumechimba biti mnada wa TRA tungeshaonyeshwa kwenye press conferrence ya Kamanda Mambosasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam! shoka mfupani utamu wake is now expressed to rc lakini huyu si alivamia clouds tv si aende huko tra au bandarini akapore hayo mankontena?
 
Kama kweli ni vifaa vya mashuleni basi TEA walipie hizo kodi na kugawa kwenye shule zenye mahitaji ya vifaa hivyo
TEA wanaweza kulipa vifaa ambavyo hawajaagiza?Tena vimekuja kwa jina la Makonda!
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda jana alifanya ibada maalum kanisani kwa ajili ya makontena yake yenye samani za shule yanayoshikiliwa na TRA

Katika ibada hiyo Makonda alionya watakao nunua makontena yake watapata laana kali

Pia aliwarushia dongo TRA akisema ni watu wabaya wasio na huruma na kudai kuwa wanamchukia Makonda

"Kama wanachukia Makonda waondoe nembo ya majina yangu kwenye makontena hayo" alisema Makonda

Ni mara nyingine viongozi wa serikali wanasuguana na taasisi za serikali katika kutekeleza majukumu yake huku kiongozi huyo wa mkoa akihisi anaonewa na ni wivu unaofanywa na TRA kisa anafanya vizuri katika mkoa wake

Juzi Paul Makonda alikaririwa na vyombo vya habari kuhusu kupigwa mnada makontena yake,akisema yeye hatishiki na ni mlima hawezi kuyumbishwa na wale wasiomtakia mema katika harakati zake za maendeleo ya Dar es salaam

Kwa hali ilivyo sasa ni dhahiri kuwa Makonda analaumu serikali kumhujumu na hakubaliani na TRA na mambo inayomfanyia
Makanisa yetu yamekua makanisa ya ajaaabu sana
 
Naam! shoka mfupani utamu wake is now expressed to rc lakini huyu si alivamia clouds tv si aende huko tra au bandarini akapore hayo mankontena?

hahaaa aende na silaha nje nje kama akina harmorapa hawajakimbia..yeye kuchukua makontena kilainii
 
Back
Top Bottom