Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na sasa Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM wakati akipokelewa mkoani Dar es Salaam amesema;
"Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupita kwenye mitandao, wengi wanahamaki na wengi wana bashasha, lakini wanaohamaki wengi wao wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi
Wanawaza Makonda ataenda kufanya nini? Nimeona na wengine wameanza kuwataja Watu wengine kwamba 'Utaona sasa usiyemtaka kaja'"
"Wengine wanasema tumejifunza nini katika jambo la Makonda? Wengine wanasema mbona siku hizi hatumuoni alikuwa amejificha wapi?
Mimi sina kisasi kwa mtu yeyote na asiwepo mtu yeyote akafikiri mimi lengo langu ni kumkandamiza, asiwepo yeyote akafikiri wakati huu nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale walionifanyia mabaya, la hasha!"
"Wale wote wanaohisi ya kwamba kuna jambo halikuwa sawa, mie naelewa Mungu aliwatumia kunisaidia kumjua Mungu zaidi. Naaamini Mungu aliwatumia kunifanya niwe mnyeyekevu zaidi, aliwatumia kuniandaa zaidi
Msiwe na hofu kwangu ninyi wote ni Watumishi wa Mungu"