Makonda: Baada ya kuteuliwa wapo waliowaza naenda kufanya nini. Sina Kisasi na mtu, sitajitutumua kuonesha mabavu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na sasa Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM wakati akipokelewa mkoani Dar es Salaam amesema;

"Tangu niteuliwe nimepata nafasi ya kupita kwenye mitandao, wengi wanahamaki na wengi wana bashasha, lakini wanaohamaki wengi wao wanawaza Makonda ataenda kulipa kisasi

Wanawaza Makonda ataenda kufanya nini? Nimeona na wengine wameanza kuwataja Watu wengine kwamba 'Utaona sasa usiyemtaka kaja'"

"Wengine wanasema tumejifunza nini katika jambo la Makonda? Wengine wanasema mbona siku hizi hatumuoni alikuwa amejificha wapi?

Mimi sina kisasi kwa mtu yeyote na asiwepo mtu yeyote akafikiri mimi lengo langu ni kumkandamiza, asiwepo yeyote akafikiri wakati huu nitajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale walionifanyia mabaya, la hasha!"

"Wale wote wanaohisi ya kwamba kuna jambo halikuwa sawa, mie naelewa Mungu aliwatumia kunisaidia kumjua Mungu zaidi. Naaamini Mungu aliwatumia kunifanya niwe mnyeyekevu zaidi, aliwatumia kuniandaa zaidi

Msiwe na hofu kwangu ninyi wote ni Watumishi wa Mungu"
 
..anatuhumiwa kumshambulia Lissu.

..pia anatuhumiwa kumpoteza Ben Saanane.

..vilevile anatuhumiwa kuwateka Roma Mkatoliki, Ney wa Mitego, na Mo Dewji.

..sasa anadai uovu huo anaotuhumiwa nao ulimsaidia kumjua Mungu?!
 
MC wa Chama alipe kisasi?
Atengeneze tena genge la uhalifu aone kama safari hii atapata pa kujificha.
 
..anatuhumiwa kumshambulia Lissu.

..pia anatuhumiwa kumpoteza Ben Saanane.

..vilevile anatuhumiwa kuwateka Roma Mkatoliki, Ney wa Mitego, na Mo Dewji.

..sasa anadai uovu huo anaotuhumiwa nao ulimsaidia kumjua Mungu?!
mtoto aliyetumia cheti cha mwenzake anaishi kijanja janja mbele ya wapumbavu kwenye chama
 
..anatuhumiwa kumshambulia Lissu.

..pia anatuhumiwa kumpoteza Ben Saanane.

..vilevile anatuhumiwa kuwateka Roma Mkatoliki, Ney wa Mitego, na Mo Dewji.

..sasa anadai uovu huo anaotuhumiwa nao ulimsaidia kumjua Mungu?!
Tuhuma tu hizo, ni makosa kumhukumu mtu kwa tuhuma tu zisizo na uthibitisho.
 
..anatuhumiwa kumshambulia Lissu.

..pia anatuhumiwa kumpoteza Ben Saanane.

..vilevile anatuhumiwa kuwateka Roma Mkatoliki, Ney wa Mitego, na Mo Dewji.

..sasa anadai uovu huo anaotuhumiwa nao ulimsaidia kumjua Mungu?!
Nenda mahakamani ukapeleke ushahidi wako huko. Unazidiwa hata na Mdude Chadema aliipinga DP World kwa kwenda mahakamani?
 
Marekani huwa hawakurupuki ktk kutoa taarifa ya jambo fulani.

Wako makini sana .
 
Back
Top Bottom