Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hizi ni miongoni mwa kauli zilizotolewa na Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha katika hotuba kabambe ya Utambulisho aliyoitoa Mjini humo alipokuwa anakabidhiwa ofisi .
Hapa akikuwa akiwapa makavu waliokuwa wanamsengenya kwamba hajajifunza pamoja na kuwekwa benchi muda mrefu.
---
Makonda amesisitiza kwamba Arusha lazima iwe na mwonekano na mandhari ya kuvutia watalii kwani mkoa huo ndiyo kitovu cha utalii nchini. Katika kueleza jambo hilo Makonda amesema
Hapa akikuwa akiwapa makavu waliokuwa wanamsengenya kwamba hajajifunza pamoja na kuwekwa benchi muda mrefu.
---
Makonda: Hamna nilichojifunza zaidi ya kuwashughulikia wazembe, wavivu na Wala Rushwa
Akitoa hotuba baada ya utambulisho wake Mkuu wa Mkoa mpya wa Arusha Paul Makonda amesisitiza Viongozi wote kuwajibika na kutoa tahadhari kwa Wazembe. Akiongea mbele ya watu waliojitokeza kumpokea Paul Makonda amesema:Mmenifurahia sana ila tutageukana muda sio mrefu. Sitajali wewe ni nani, baba yako ni nani, ulipataje hicho cheo, aidha ulipata kwa kuhonga, kwa rushwa au kwa uganga nitakula sahani moja na wewe.
Lazima kila mtu awajibike kwenye nafasi yake. Msiseme huyu alikuwa Mwenezi sasa katoka kwenye Uenezi atakuja amepoa. Wengine wanasema eti saivi labla atakuwa amejifunza, hamna nilichojifunza zaidi ya kuwashughulikia wazembe wavivu na Wala rushwa. Sina elimu yoyote mimi hata niwe Mkuu wa Mkoa wa siku moja inatosha lakini awepo mtu mmoja tu ajue kuna mwanaume amepita hapa.
Kwahiyo kila mtu kwenye nafasi yake, kama ni Mkuu wa Wilaya shika Wilaya yako barabara kama ni Mkurugenzi ishike Halmashauri yako kikamilifu.
Makonda: Majengo yaliyopauka yaliyo katikati ya mji lazima yapakwe rangi kama hawataki tutabomoa
Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amewataka wamiliki wa nyumba zilizopo katikati ya jiji hilo kuzipaka rangi ili ziwe na mwonekano mzuri vinginevyo nyumba hizo zitabomolewa.Makonda amesisitiza kwamba Arusha lazima iwe na mwonekano na mandhari ya kuvutia watalii kwani mkoa huo ndiyo kitovu cha utalii nchini. Katika kueleza jambo hilo Makonda amesema
Tunataka Arusha iwe salama salimini tunapata watalii wengi sana haitapendeza wakija wakute hapapo salama. Usalama namaanisha wa kila kitu pamoja na kufanya biashara usiku. Hatutaki Arusha iwe mji mkubwa uliolala. Hao Watalii wakija hapa halafu baadaye wanaenda kulala hiyo hela tunaipata lini? Wametoka kwao hawajaja kulala huku wamekuja kushangaa. Lazima tuhakikishe usalama pamoja na usafi wa mji wetu.
Nilikuwa namdokeza RAS siku moja inabidi akae na wale watu wenye hizi daladala za hapa mjini angalau nasisi tuwe na mabasi ya ghorofa katikati ya mji. Na wenye majengo yao katikati ya mji Wapake rangi kama hawawezi tutabomoa, hatuwezi kuwa na mji umejaa uchafu rangi zinachanganyikana tu. Kamji kazuri haka, kana mandhari nzuri ni sisi wenyewe kukapanga