Makonda kusuka au kunyoa: Kinana awataka watendaji wafuate muongozo wa Rais kwa kutodhalilisha watendaji hadharani

Makonda kusuka au kunyoa: Kinana awataka watendaji wafuate muongozo wa Rais kwa kutodhalilisha watendaji hadharani

CCM ukiielewa utacheka sana. Kwa ufupi Makonda na Kinana wanafurahisha makundi mawili yanayotofautiana. Kuna wananchi wanaofurahia baadhi ya anayofanya Makonda na kuna wasiopendezwa. Sasa hawa wajumbe wa wawili wa kamati kuu wanataka sapoti ya makundi yote kwa CCM. Unayependezwa na kauli ya Mzee we wetu na unayependezwa na kauli ya kijana nae wetu. Kazi iendelee
 
Komredi Makonda aliwahi kumdhalilisha nani hadharani tangu amekuwa Katibu Itikadi, Uenezi na Mafunzo? Mtaje mmoja.
Na kama kweli Komredi Kinana kamsema Makonda huoni kuwa yeye ndio kamdhalilisha Komredi Makonda hadharani? Alishindwa vipi kumwambia ofisini? Na unafikiri nani wa kishughulikiwa hapo?
 
Kumdhalilisha mtu ni kumtaka afanye kitu ambacho hatakiwi kufanya au kinachochafua utu wake.

Makonda ye anahamasisha utendaji na uwajibikaji bila kuoneana haya. Huyo samia mwenyewe amewashawaambia viongozi wenzie stupid hadharani tena mara mbili.

Kinana anajaribu kufukuzana na Makonda. Kitu ambacho atafeli. Hao kina Kinana walipewa nafasi Makonda akiwa benchi wakadhani wamepewa ulaji. Mwanaume anapiga kazi ndio wanashtuka.

Sent from my SM-A225F using JamiiForums mobile app
Ngoja Tusubiri tuone !!
 
Komredi Makonda aliwahi kumdhalilisha nani hadharani tangu amekuwa Katibu Itikadi, Uenezi na Mafunzo? Mtaje mmoja.
Na kama kweli Komredi Kinana kamsema Makonda huoni kuwa yeye ndio kamdhalilisha Komredi Makonda hadharani? Alishindwa vipi kumwambia ofisini? Na unafikiri nani wa kishughulikiwa hapo?
Mmmh !! Ngoja tuone !
 
Makonda salsa asuke au anyone, Kinana ametoa kauli kwamba falsafa ya Rais Samia ni kufuata Katiba sheria na kanuni, na kwamba watendaji wasidhalilishwe na viongozi.

Naiona falsafa ya makonda ya kudhalilisha ili a late umaarufu inagonga mwamba, je nini hatma yake?

Atabadili gia angani na kwanza kueneza itikadi ya chama badala ya kutembea huku na kule akidhalilisha watendaji?.
View attachment 2841593
Kwani Makonda kamdhalilisha nani so far..tangu arejee!!?
 
Huyu anafubaza upepo wa Mama! Mhe. Rais usimkubalie huyu mnafiki! MTU ambaye hawajibiki Wacha awajibishwe.

Ndiomaana na wewe uliamua kiwatukana stupid (pumbavi/wapumbavu)
 
Kumbe wao kwa wao huwa hawapendi kudhalilishana !!
Ila wao ni sahihi kuwadhalilisha wazee wenye umri hata wa miaka Sabini kwa sababu tu ya kukosoa kwa maneno ya kawaida kabisa !
Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni !!
Ngoja Tusubiri tuone KARMA huwa inafanyaje kazi zake !!
Fimbo ya mnyonge hulipwa na Mungu 🙏🙏 !
 
Haelewi mchezo unavyokwenda,Kanda ya Ziwa Mwanaume anayesikilizwa ni Makonda,anafikiri Mama mjinga kumrudisha Makonda!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Kanda ya Ziwa ya wapi anakosikilizwa Makonda? Nipo Kanda ya Ziwa, hapa Mwanza, sijawahi kumsikia yeyote akitoa positive comments kwa Makonda. Au hao watu anaowasombasomba kwaajili ya mikutano yake, ndio wamekuwa wawakilishi wa watu wote wa kanda ya Ziwa?

Si Makonda wala si Kinana, mwenye ushawishi Kanda ya Ziwa.
 
Zama za Mzee Kinana zimepita, wakati mwingine Wazee wawe na busara za kukaa pembeni kuwaachia damu Changa madaraka. No thanks
Hata kama ni kuachia damu changa, ndiyo wa kuachiwa awe mtekaji, muuaji, mfoji vyeti vya masomo, Bashite?
 
Makonda salsa asuke au anyone, Kinana ametoa kauli kwamba falsafa ya Rais Samia ni kufuata Katiba sheria na kanuni, na kwamba watendaji wasidhalilishwe na viongozi.

Naiona falsafa ya makonda ya kudhalilisha ili a late umaarufu inagonga mwamba, je nini hatma yake?

Atabadili gia angani na kwanza kueneza itikadi ya chama badala ya kutembea huku na kule akidhalilisha watendaji?.
View attachment 2841593
Ficha upumbavu wako, pamoja na muuaji wa Tembo
 
Back
Top Bottom