Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema
"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.
Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."
Hiyo ni kauli ya kijasiri kabisa iliyotolewa na Mheshimiwa Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa.kauli hiyo imetolewa akiwa anahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Tunduma.Ni kauli iliyotikisa na kutetemesha hadi mpakani mwa zambia huko kutokana na namna ilivyotolewa kijasiri na kijana jasiri.
Amesema amekuwa akiambiwa na kupewa masharti mengi mengi sana kutoka kwa watu ya kuwa mara asisalimiane hivyo na watu,mara awe makini na vyumbani ,mara yeye ni kijana bado mdogo kwa hiyo awe makini sana mara hivi mara vile. Kwa ujasiri na ukali akasema ya kuwa yeye haogopi kurogwa wala kuwekewa sumu.akasema ya kuwa yeye analindwa na Mungu tu.
Huku akishangiliwa na maelfu ya watu alisema ya kuwa Mungu akimtaka basi atammchukia tu .katika hotuba hiyo alisema kwa ukali na ujasiri kuwa tusitishaneeee hii ni wakati akieleza kuwa unakuta mwingine anasema anaongea jambo hili la kisheria kama nani? Naye akasema huyo anayeongea hivyo naye anaongea kama nani? Akasema kwanza wamesomeshwa kwa kodi za watanzania na wanalipwa kwa kodi za watanzania hivyo wasilete za kuleta.
Akasema watumishi wazembe atakula nao sahani moja na kwamba dawa yao inachemka moyoni,maana wengine wamekuwa wanalindana na kukumbatiana katika maovu,halafu wakipanda jukwaani wanasema mama anaupiga mwingi. wakati wanajuwa kuwa wala hawafanyi kazi zaidi ya uzembe na uvuvi halafu wanatoa sifa za uongo kwa Mheshimiwa Rais. amesema Ole wao wakiendelea na tabia hizo,maana hawatavumiliwa wala kuachwa salama.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Naona Makonda anapingwa sana hata na baadhi ya wana CCM, hususan viongozi.Katika Kipindi kimoja cha Medani za Siasa nilimsikia Lema akimnanga waziwazi Makonda kuwa alishiriki mauaji na kuteka watu. Pia Gerald Hando alitamka hivi karibuni kuwa Makonda alikuwa mtekaji.
Nadhani tabia ya kuruhusu shutuma nzito za aina hiyo zina baraka ya Waziri wa Habari.
Shutuma za aina hiyo huwa zinatakiwa kuthibitishwa.Huo ni uonezi.