Makonda: Kwa taarifa yenu sifi! Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu

Makonda: Kwa taarifa yenu sifi! Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu

Naona Makonda anapingwa sana hata na baadhi ya wana CCM, hususan viongozi.Katika Kipindi kimoja cha Medani za Siasa nilimsikia Lema akimnanga waziwazi Makonda kuwa alishiriki mauaji na kuteka watu. Pia Gerald Hando alitamka hivi karibuni kuwa Makonda alikuwa mtekaji.

Nadhani tabia ya kuruhusu shutuma nzito za aina hiyo zina baraka ya Waziri wa Habari.
Shutuma za aina hiyo huwa zinatakiwa kuthibitishwa.Huo ni uonezi.
Uthibitisho gani?. Si ni juzi alisema ingekiwa kipindi Cha nyuma CHADEMA wangemtambua.
 
Hizi Siasa za Kurogana na Kuwekeana Sumu niliamini ziko Vyama vya Upinzani sasa Kauli ya Mwenezi wa CCM imenishtua Sana

Imenikumbusha enzi zile Wabunge wa Chadema walikuwa na dada zao Viti Maalum kwa ajili ya kuwapikia chakula kuepuka kulishwa Sumu Mitaani

Hata Dr Slaa alilalamika Chumba chake kurushiwa ungaunga kama ule wa Joka la makengeza bungeni

Yaani tunarudi kule kule dadeki 🐼
Kama kawaida yako. Mnafiki wa taifa
 
Amuulize Magufuli, hapo cha muhimu awe makini tu. Akipuuzia watamuondoa CCM wauaji wakubwa. Tena huyo Nchimbi ndo balaa kabisa. Huyo Nchimbi ndo mmoja wa wanaomiliki account ya Kigogo kule twitter.
Duh
 
Makonda ni kijana mdogo? Kwahiyo nina muda bado kumbe.

Hata hivyo naamini yeyote ambaye alitaka kumuua Makonda angefanya hivyo kipindi yupo benchi.

Alikua vulnerable na hata jamii ilimsahau. Kama mtu hakufanya hivyo pale sioni ni kivipi afanye hivyo sasa hivi.

Hivyo kwa maoni yangu kauli ya Makonda ni ya kujihami na siyo kwamba kuna tukio hilo.
Sasa mkuu, kipindi yupo benchi alikuwa na madhara gani kwao. Think hata JPM kwanini alikuja kupata maadui baada ya kuingia uwanjani wakati yupo benchi kama waziri hawakumuona?
 
SIR- 100 kama ana akili asikilizee maneno.
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema

"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.

Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."

 
Nimecheka kwa nguvu, ccm mdomoni wanahubiri 4R za rais, sasa hayo ya kuwekeana sumu yanatoka wapi tena? Bundi ametua kwenye nyumba ya wafitini lazima mpoteane. Siku zote umoja wa wahalifu haudumu. Hapa lazima matokeo ya utekaji wa muhalifu makonda lazima yavujishwe na wanaccm.
Nani anataka kutoboa mtumbwi😁
 
Back
Top Bottom