Makonda: Kwa taarifa yenu sifi! Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu

Makonda: Kwa taarifa yenu sifi! Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu

Hizi Siasa za Kurogana na Kuwekeana Sumu niliamini ziko Vyama vya Upinzani sasa Kauli ya Mwenezi wa CCM imenishtua Sana

Imenikumbusha enzi zile Wabunge wa Chadema walikuwa na dada zao Viti Maalum kwa ajili ya kuwapikia chakula kuepuka kulishwa Sumu Mitaani

Hata Dr Slaa alilalamika Chumba chake kurushiwa ungaunga kama ule wa Joka la makengeza bungeni

Yaani tunarudi kule kule dadeki 🐼
Ukiona mpaka kaongea jua kafanyiwa hilo jaribio
 
Ndio maana huwa sielewi kwa nini mtumishi wa Mungu anakuwa mwanasiasa
Mtumishi wa Mungu ni yule atendaye na kuhubiri KWELI iletayo wokovu. Aweza kuwa mkulima, mfugaji, seremala, ...., kiongozi na siyo lazima awe kanisani, msikitini au nyumba yoyote ya ibada.
Kuna tofauti kubwa kati ya kiongozi wa dini na mtumishi wa Mungu.
 
Kwa nini aweke mawazo yake kwenye kuwekewa sumu?Kuna nini huko CCM?Mlifikiri mpo salama wakati CDM wanafanyiwa ujahili?Mkasahau kwamba wakishamalizana na CDM watahamia kwenu.Kikombe mlichokiumba na mkinywe kwa ujazo wake.Amen...🙏🙏🙏🙏
 
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema

"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.

Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."

Tuliwaambia mkishamaliza kuwaua wapinzani mtaanza kuuana wenyewe ndiyo haya sasa juzi tu wamemuua Thadei Ole Mushi sasa wamehamia kwa Makonda.
IMG-20191216-WA0001.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Hiyo ni kauli ya kijasiri kabisa iliyotolewa na Mheshimiwa Makonda Katibu wa itikadi, uenezi na mafunzo wa CCM Taifa.kauli hiyo imetolewa akiwa anahutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Tunduma.Ni kauli iliyotikisa na kutetemesha hadi mpakani mwa zambia huko kutokana na namna ilivyotolewa kijasiri na kijana jasiri.

Amesema amekuwa akiambiwa na kupewa masharti mengi mengi sana kutoka kwa watu ya kuwa mara asisalimiane hivyo na watu,mara awe makini na vyumbani ,mara yeye ni kijana bado mdogo kwa hiyo awe makini sana mara hivi mara vile. Kwa ujasiri na ukali akasema ya kuwa yeye haogopi kurogwa wala kuwekewa sumu.akasema ya kuwa yeye analindwa na Mungu tu.

Huku akishangiliwa na maelfu ya watu alisema ya kuwa Mungu akimtaka basi atammchukia tu .katika hotuba hiyo alisema kwa ukali na ujasiri kuwa tusitishaneeee hii ni wakati akieleza kuwa unakuta mwingine anasema anaongea jambo hili la kisheria kama nani? Naye akasema huyo anayeongea hivyo naye anaongea kama nani? Akasema kwanza wamesomeshwa kwa kodi za watanzania na wanalipwa kwa kodi za watanzania hivyo wasilete za kuleta.

Akasema watumishi wazembe atakula nao sahani moja na kwamba dawa yao inachemka moyoni,maana wengine wamekuwa wanalindana na kukumbatiana katika maovu,halafu wakipanda jukwaani wanasema mama anaupiga mwingi. wakati wanajuwa kuwa wala hawafanyi kazi zaidi ya uzembe na uvuvi halafu wanatoa sifa za uongo kwa Mheshimiwa Rais. amesema Ole wao wakiendelea na tabia hizo,maana hawatavumiliwa wala kuachwa salama.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

View attachment 2896605View attachment 2896606View attachment 2896607Lucas mwashambwa weka namba.
 
Sasa mkuu, kipindi yupo benchi alikuwa na madhara gani kwao. Think hata JPM kwanini alikuja kupata maadui baada ya kuingia uwanjani wakati yupo benchi kama waziri hawakumuona?
JPM tangu waziri wa Ujenzi alikua na wapinzani.

Makonda si alisema anawindwa na wauza dawa za kulevya ila alivyokua benchi hawakumtafuta.

Hata hivyo ni ngumu political figure akasuka mpango wa kumuua mtu ambaye yupo kwenye spotlight na asihisiwe
 
Makonda amefanywa Katibu mwenezi,itikadi, uenezi na mafunzo ili amalizwe?

Mtakumbuka Thadei Ole Mushi alijenga ccm ilijenga urafiki wa kinafiki na Ole Mushi wakafikia mahali Comred chongolo x general signatory of Ccm

Akaanza kuzunguka nae kuinadi Dp world kwenye ziara za ccm

Haikuchukuwa muda zikaja romours Ole Mushi amelishwa sumu

Baada ya muda yeye mwenyewe akajitokeza kwenye ukrasa wake wa mitandao ya kijamii na kukanusha.
Lakini wale walio ufahamu uandishi wa Mushi

Wakasema siyo yeye.

Haikuchukuwa muda tukaambiwa amefariki.

Paul Makonda acha unachokifanya
 
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema

"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.

Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."


Pamoja na hayo, lakini ajiangalie sana. Maana wahuni siyo watu.
 
Ndio maana huwa sielewi kwa nini mtumishi wa Mungu anakuwa mwanasiasa
Uko sawa kabisa,

Mtumishi wa Mungu kuwa mwanasiasa ni ngumu sana,

Ukiona imetokea, jua wanasiasa wameshindwa kutenda HAKI Kwa wananchi, Daudi inabidi apewe special mission kurescue situation.
 
Back
Top Bottom