Makonda: Kwa taarifa yenu sifi! Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu

Makonda: Kwa taarifa yenu sifi! Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu

Tangu kuanzishwa kwa CCM, siasa za kurogana na kuwekeana sumu na kuuana ndiyo jadi yao.

Kwa sisi tuliokuwa na akili miaka ya 1970s tunaelewa sana hayo mambo, hasa kwa waliokuwa pale idarani.

Ipo siku mafile ya siri yatawekwa hadharani kudhihirisha umafia wa wana CCM na serikali zake.

"CCM hatuachiani maji mezani", Jakaya M. Kikwete.
Mpaka mkubwa wa Nchi kusema vile ujue humo ndani ni balaa !!
Law of the universe “what goes around comes around “
Ngoja tuone !!
 
Amuulize Magufuli,hapo cha muhimu awe makini tu.Akipuuzia watamuondoa CCM wauaji wakubwa. Tena huyo Nchimbi ndo balaa kabisa. Huyo Nchimbi ndo mmoja wa wanaomiliki account ya Kigogo kule twitter.
Duh 🙄 !
Ngoja tuone !
 
Sasa Shujaa Magufuli apumzike kwa Amani

Ahsante Sana kwa Zawadi uliyotuachia ya Huyu Bwana mdogo Paul Makonda 😄

Navalonge swela 😂
wapumbavu ni wapumbavu tu, we hujawahi kuwa na akili, kinachokusumbua ukabila. Magufuli alikuwa shetani aliyeharibu nchi yetu hatakiwi hata kutajwa kokote.
 
Hizi Siasa za Kurogana na Kuwekeana Sumu niliamini ziko Vyama vya Upinzani sasa Kauli ya Mwenezi wa CCM imenishtua Sana

Imenikumbusha enzi zile Wabunge wa Chadema walikuwa na dada zao Viti Maalum kwa ajili ya kuwapikia chakula kuepuka kulishwa Sumu Mitaani

Hata Dr Slaa alilalamika Chumba chake kurushiwa ungaunga kama ule wa Joka la makengeza bungeni

Yaani tunarudi kule kule dadeki [emoji209]
Makonda amerudi,unashangaa nini? Kesi za utekaji hujasikia zilivyorudi kwa kasi? Uchaguzi unakaribia,usishangae kusikia tena maelfu ya viroba yakionekana ufukweni.Mungu awalinde sana wale wote wanaoenda kinyume na huyu mtu,siku zao zaweza kuwa chache.
 
Makonda ni kijana mdogo? Kwahiyo nina muda bado kumbe.

Hata hivyo naamini yeyote ambaye alitaka kumuua Makonda angefanya hivyo kipindi yupo benchi.

Alikua vulnerable na hata jamii ilimsahau. Kama mtu hakufanya hivyo pale sioni ni kivipi afanye hivyo sasa hivi.

Hivyo kwa maoni yangu kauli ya Makonda ni ya kujihami na siyo kwamba kuna tukio hilo.
Hujui kitu kaa kimya wewe dogo
 
Kwenye sanaa ya mauwaji ya watu mashuhuri (assassination) huwa inashauriwa kuwa haijalishi ni kwa kiasi gani unafahamu hatari iliyopo mbele yako juu ya kuondolewa, kamwe usiiseme hatari hiyo kwenye hadhara, inaweza kuwahisha kuondolewa kwako hata na wale ambao haukuwategemea kwa sababu tayari unakuwa umewapa cover wasiotegemewa dhidi ya waliotegemewa.

Rejea
  • Robert Ouko alipokabiliwa na mauwaji alikaa kimya mpaka siku alipokwenda kumalizwa ikulu nairobi then zikaanza kutengenezwa taswira kuwa ni uhasama wa kifamilia.
  • Jacob Juma, baada ya kutambua yupo katika hatari ya kuuwawa alimshutumu moja kwa moja William Ruto kwamba akipatwa na lolote baya aulizwe Ruto, matokeo yake na aliuwawa ndani ya siku chache sana kisha watu kama kina Cyrus Jirongo wakaanza kumnyooshea kidole Ruto.
Paul Makonda awe makini na kauli za kuhusu uhai wake kuwindwa, inawezekana akawa anaropoka kuchangamsha genge ila ikaja kumgharimu kweli. Aione Bashite
 
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema

"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.

Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."

Makondo leo nimemwelewa kitu kuanzia kuewekewa Sumu chumbani mpaka kwenye Chakula nimemwelewa sana, watu wanawinda vibaya sana
 
Makonda mwombe Mungu isije ikawa ya mzee wako ukumbukwe tu inaitwa kutumiwa kuna madhara yake
 
Katibu wa NEC-CCM wa Itikadi na Uenezi, Paul Makonda akiwa katika ziara yake Tunduma Mkoani Songwe amesema

"Si nimepewa usemaji? nitasema kweli bila kumung'unya maneno na kwa taarifa yenu sifi na Mungu hana mpango wa kuniondoa kwanza. Mtege sumu kwenye vyumba mnapoteza muda tu, mtafute waganga mnapoteza muda tu. Nataka kila kiongozi awajibike kwenye nafasi yake.

Waliopo serikalini wote wana magari, nyumba na wanaheshimika kwa kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwanini hatumsaidii kazi? Tabia ya kusubiri Rais ana ziara ndiyo mnajitokeza na mkifika pale ooh Mama unaupiga mwingi hapa ni wewe tu!... Ngojeni dawa yenu inachemka."

Mtajuana wenyewe huko, mnauana
 
Paul Makonda awe makini na kauli za kuhusu uhai wake kuwindwa, inawezekana akawa anaropoka kuchangamsha genge ila ikaja kumgharimu kweli. Aione Bashite
Kashashtukia mchezo watu washamtonya unajua nini mnapopanga mipango ya nanihu kuna wale ambao hawapendi Ila nao wanakua washiriki na nanihu sasa hao ndio wanaovujisha data kuwatonya upande wa pili kwamba jamani eeh muwe makini huku kuna mpango umeandaliwa
 
Badala ya kufanya kazi ya boss aliomtuma anaanza kuchomekea vi-hadithi vyake vya ‘personal issues’ na vijimigogoro vilivyopo ndani ya CCM.

Ndio watu wanamuhitaji na ameweka wazi anachofanya katumwa na boss wake (apeleke mvua waone panapo vuja).

Kazi yenyewe anaitendea haki. Ila haya mambo ya kuanza kujiona special na kujitapa kama vile ‘god chosen’ ndio mwanzo wa kujigangia mikosi. Besides udhani kama katumwa kuongelea changamoto zake binafsi alizopitia na kurusha mipasho, bali kazi ni kusikiliza kero za wananchi.
 
Walishindwa kumuua akiwa kijiweni ndio wake wamuue leo
 
Back
Top Bottom