Makonda, Lukuvi pamoja na Kabudi waelekea ziarani Ngorongoro

Makonda, Lukuvi pamoja na Kabudi waelekea ziarani Ngorongoro

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini mh Godbless Lema amesema atakwenda Ngorongoro kuungana na Makonda Lukuvi Kabudi na Afande Awadh katika kuwasikiliza Wamasai na kilio Chao

Lema amesema ukurasani X

My take; Sukuma gang hawajawahi kufeli 😃
Hapo msukuma ni mmoja tu hao wengine hata hatuwajui huku usukumani🤣🤣🤣
 
..Kabudi, Lukuvi, na Makonda, ni wanasiasa wenye kiburi kwelikweli.

..Lakini leo mbele ya Wamaasai wameweka pembeni viburi vyao,na kuwapigia magoti wananchi.

..Nimemsikia Makonda akiomba nyimbo za Kimaasai.

..Kabudi amemtaja neno HAKI mara kadhaa. Mwana-Ccm ni mwiko kutaja neno haki lakini kwa wananchi wamelitaja.

..Kwa kifupi wananchi wa Ngorongoro wameonyesha njia. Wamekataa kunyanyaswa.


View: https://m.youtube.com/watch?v=Xj9xjdD7bcw&pp=ygURa2FidWRpIG5nb3Jvbmdvcm8%3D


Kwa hiyo Uteuzi wa Lukuvi na Kabudi ilikuwa ni Maandalizi ya kwenda kuwaondoa Wamasai .....!!?
 
Kwa hiyo Uteuzi wa Lukuvi na Kabudi ilikuwa ni Maandalizi ya kwenda kuwaondoa Wamasai .....!!?

..kwenda kuwapigia magoti Wamaasai.

..Serikali wameshikwa pabaya. Utalii wa Tanzania unategemea sana Serengeti na Ngorongoro.

..Wamaasai walikuwa hawajui thamani yao.

..aliyewa-organize waandamane ktk msimu wa Watalii ana akili sana.

..Serikali isingeweza kutumia nguvu.
 
Serikali inayoongozwa na Mama Samia ni sikivu Sana Na inaishi maneno yake Kwa vitendo.

Ni suala zuri kusikiliza mahitaji ya wanyonge na sio kutuma nguvu. Hivi ndivyo anavyotaka Rai's watu mpendwa. Asante Kwa taarifa mkuu
 
Kwa hiyo mbowe anavyowaroga wenzie hapo makao makuu huo sio ukatili?
Kijana wa karne hii unaandika ujinga kama huu hadharani bila shaka kuna tatizo kubwa sana kwenye maisha yako
 
Wadau hamjamboni nyote?

Hatimaye Mawaziri Vigogo ya Serikali ya Rais Samia ambao ni Profesa Kabudi, William Lukuvi na Kamishna wa mafunzo Jeshi la polisi Awadhi wakutana na Paul Makonda na kufanya kikao kizito na Kamati ya Usalama ya Mkoa Arusha.
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu William Lukuvi (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda wakiwa katika picha ya pamoja walipowasili kwenye ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ambapo wakiwa wilayani humo leo Agosti 23, 2024 watafanya shughuli mbalimbali.

Soma Pia:
Viongozi hao ambao wameongozana na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi nchini Awadhi Juma Haji, tayari wamekutana na Kamati ya Usalama ya mkoa wa Arusha. Viongozi hao wanatarajiwa kwenda Ngorongoro kuzungumza na wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro.

Tendeni haki itawainua vinginevyo mtapotea
 
Hatua ya 1: Tengeneza tatizo.

Hatua ya 2: Jitenge na hilo tatizo.

Hatua ya 3: Jifanye unaguswa na tatizo ulilolitengeneza.

Hatua ya 4: Tatua hilo tatizo katika namna inayofanikisha malengo yako.

Hatua ya 4: Hakikisha unapongezwa kwa juhudi.
 
Back
Top Bottom