Ndugu zangu Watanzania,
Hiyo ndio habari kuu inayoendelea kusambaa Nchini kwote na nje ya mipaka ya Tanzania .Ambapo Mwamba Mwenyewe na kijana jasiri kusini mwa jangwa la Sahara Mheshimiwa Paul Christian Makonda ataongoza msafara mzito wa mawaziri wazito na wasomi kwelikweli kuitembelea na kuzungumza na wananchi wa Ngorongoro.
Ambapo katika msafara huo yupo waziri wa katiba na sheria Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi. Huyu ni waziri na mhadhiri mstaafu wa chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha sheri.ambaye amewahi kuweka rekodi ya Mwanafunzi bora kabisaa katika Historia ya Taifa letu na huo kikuu cha UDSM .
kwa kupata alama za juu sana katika sheria .narudi kusisitiza kuwa alama za juu katika sheria.maana ukienda katika uchumi yupo Mwamba Mwingine Profesa Ibrahim haluna Lipumba..
Lakini pia katika ziara hiyo yupo pia Waziri Mwingine wa muda mrefu sana na katika awamu tofauti tofauti na aliyekuwa mshauri wa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan Mheshimiwa William Lukuvi.
Kwa hakika naamini kwa safu hiyo ya magwiji hawa basi wananchi wa Ngorongoro watapigwa Simo zuri mpaka wabakie wanabubujikwa machozi ya furaha bila kukatika utafikiri wamepakwa pilipili machoni.
Kikubwa endelea kubwa hapa hapa jukwaani na kuendelea kuwa karibu yangu ili kuendelea kupata habari motomoto kutoka huko Ngorongoro mkoani Arusha. Tarajieni hotuba nzito nzito kutoka kwa miamba na majabali haya zitakazo teka Nchi
View attachment 3077170
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.