Shukrani sana. Baada ya Kikwete niliamini hatatokea Rais mwingine mbovu zaidi kwenye utendaji kama yeye lakini baada ya miezi michache ya huyu dikteta uchwara nikagundua dhana yangu haikuwa sawa hata chembe na ndiyo kwanza mwaka mmoja tu sijui baada ya miaka mitano nchi yetu itakuwa katika hali gani. Usitegemee kuona lolote la maana kutoka sera MUFILISI, kudharau katiba na Bunge na maamuzi ya kukurupuka. Huko lori linakokwenda kuna giza nene sana, lori halina taa wala break na dreva haoni vizuri ana matatizo ya macho hivyo ni MAJANGA TU!
Nafikiri wengi humu tulitaka Raisi aliye kama JPM, na wengi tulimfurahia na tunaendelea kumfurahia.
Waliobadili mawazo juu yake wengi sana hawakutegemea atakuwa nanmisimamo kama hii ambayo zamani ilikuwa ndoto ukifikiria na kusaidia kunyoosha nchi kwenye mengi na pia kutuendeleza "Hapa kazi tu" itakumbukwa milele. Kwa Kikwete na wa kabla yake hatuna la kukumbuka sana labda ile moja ya Mwinyi na haikunikaaaa na ndio maana siikumbuki ninavyoandika.
Kwa awamu hii tunajua laki si pesa imekufa na walio chini nao wanapumua, ealiokuwa wengi juu na dharau zao imesikitisha kuwa walikuea wanatumia njia za mikato na ufisadi ulikomaaa. Hata mtu sasa hivi ukienda kwenye ofisi za umma unajitambua kama mwananchi anayepaswa kuhudumiwa na sio ile ilikuwa mtu unaenda unafikiri sio ofisi ya umma bali ya mtu binafsi.
Itazoeleka tu katika mengi, kuhusu mengine ni wananchi naowana budi kuchangia ujuzi na maarifa kulipaisha taifa letu.
Mh. Magufuli hapendi wavivu na ndio ile ya kila mtu afanye kazi...yaani kila mtu ajiingizie kipato kivyovyote tu awezavyo.
Ni mengi naishia hapa ila kuwa na subira...najua ameumiza wengi hawakutegemea ila wangeishi maisha ya mstarini wasingelalamika hivi na kumchukia wanavyofanya.
Hakuna kurudi nyuma bali kuanza kuzoea kwa mazuri, miaka nane natamani iwe kama miaka 20. Kuna mengi tunasubiri kufaidika mitaani kama beinza vingi kuzidi kushuka watu waambulie kujipaisha.
Lori linataa na hakuna giza mbeleni, Mola analiongoza kuwa na imani meanga uleeee na utazidi kuwepo.
Unaona na viongozi wengi wanafurahia kuwa na uwezo wa kufata sheria bila kuombwa kupindisha kwa sababu ya kupewa bahasha za khaki. Mengi viongozi waliogopa kusema au kufanya awamu hii wanayatenda, na ndio watu hawaishi kulalamika itazoeleka tu. Hakuna mteremko awamu hii
Unajua Magufuli 2020 kama kawa. Na Makonda nae kuzidi kupaa kama kawa, ona anavyojadiliwa humu leo hadi raha.