Makonda: Marufuku kudai nyongeza ya mshahara! Nashangaa watu wanapita na mabango, mie ningewachapa

Makonda: Marufuku kudai nyongeza ya mshahara! Nashangaa watu wanapita na mabango, mie ningewachapa

Makonda sasa kaota mapembe na mkia. Haaaaaaa, mpuuzi sn.
 
Hili doa kubwa sana kwa Raisi Magufuri na chama cha mapinduzi
 
Natamani kweli alifanye hilo alilisema, ili chama kizidi kutengeneza maadui.
 
Huyu jamaa sijui madaraka ya ukuu wa mkoa anayalinganisha na nini,,, kudai nyongeza ya mishahara siamini kama ni dhambi ambayo adhabu yake ni kuchapwa viboko,, makonda punguza kiburi hii ni dunia tu.
 
Shule inasaidia kuongeza maarifa na akili kichwani, lakini kwa kuwa Bashite ana elimu ya darasa la saba sishangai kwa matamko haya ya kifedhuri dhidi ya watumishi wa Umma
 
Hii nchi imeshakuwa ya kidikteta kamili. Yaani kiongozi wa serikali anasema angechukua sheria mkononi na kuwachapa viboko washika mabango.

Angekuwa nchi ya dunia ya kwanza angetakiwa ajiuzulu kwa kuhamasisha uvunjaji wa sheria.
 
Na support Kauli yake.
Ipo sahihi kabisa.. usiitafsiri moja kwa moja.. hapo anachomaanisha ni kuwalenga watumishi ambao hawatimizi majukumu yao.

Kama hujawahi kukutana na hawa watumishi hasa hasa kwenye halmashauri zao basi usiombe ukutane na hawa Miungu watu kwenye hizi halmashauri. Ukiwa na shida.. utakoma kuringa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Shule inasaidia kuongeza maarifa na akili kichwani, lakini kwa kuwa Bashite ana elimu ya darasa la saba sishangai kwa matamko haya ya kifedhuri dhidi ya watumishi wa Umma
Wapo watu wana elimu ya darasa la 7 na wengine hawakusoma lkn wana busara,hekima na heshima.Huyo c......o ni kiburi chake tu na ulimbukeni wa madaraka.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kauli hiyo ya Mheshimiwa Paul Makonda, Mkuu wa mkoa wa Dsm, haina hata chembe ya Hekima. Na ni udhalilishaji wa watumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom