Makonda: Mwakani tunaanzisha ligi ya wazawa tu!

Makonda: Mwakani tunaanzisha ligi ya wazawa tu!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Waziri wa michezo bwana Paul Makonda amesema kuwa kuanzia mwakani ataanzisha ligi ya wachezaji wa ndani tu kama ilivyokuwa michuano ya Afrika (CHAN) iliyohusisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika tu. Kwa kuwa michuano hii ya Afrika imefutwa rasmi na CAF, sasa ni wakati muafaka kuifufua kwa ngazi ya nchi. Kwa hiyo, michuano hii itaanza kupeperuka rasmi kuanzia msimu wa 2026/2027 ambapo ni wachezaji wa ndani tu watakaosajiliwa kushiriki ligi hii.

Kwa mujibu wa Makonda, lengo la kuanzisha michuano hii ni kuboresha kiwango cha mpira miongoni mwa wachezaji kutoka Tanzania na kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki. Hii itasaidia pia kuipandisha nchi kwenye viwango vya soka vya FIFA.

Bila kuwapotezea muda, hebu msikilize wewe mwenyewe kupitia link hii hapa chini:

MAONI YANGU
Namuunga mkono bwana Paul Makonda kwani ligi ya sasa imejaa ukiritimba na kusababisha wachezaji wa ndani kutoshiriki ipasavyo. Ligi mpya itahakikisha inashirikisha wachezaji hata kutoka huko mashinani, pasipo ubaguzi wowote. Utaratibu wa sasa wa kuruhusu timu kusajiri wachezaji wa kigeni 12 ni wa ovyo sana. Sikubaliani nao abadan. Nakubaliana na bwana Makonda (great thinker) kwa kuanzisha ligi ya wazawa haraka iwezekanavyo.
​
 
Hilo ni wazo zuri, ila michuano itakosa msisimko kama ile ligi ya taifa sababu ua ubora mbovu wa wachezaji wetu, tutaona mpira MCHAFUKOGE.
Hii ligi isihusishe wachezaji wa ligi kuu wala ligi daraja la kwanza na la pili.
Kikubwa Wawekeze kwenye academy, tupate product bora, wachezaji wetu wengi wazawa uwezo wao ni wa kawaida mnooo..
Shida ni ukiritimba, vipajo vya maana wakati mwingine vinaachwa, wanachukuana kwa kujuana ama rushwa.
 
Unapendekeza hii ligi ichezwe kipindi gani na isimamiwe na kugharamiwa na nani mkuu?
 
Unapendekeza hii ligi ichezwe kipindi gani na isimamiwe na kugharamiwa na nani mkuu?
Ikishakuwa ligi maana yake ni msimu mzima iende. Mwezi wa ianzie mwezibwa 4 mwishoni ama wa 5 hivi, mwishoni mwa npl ikiwa imeisha na inapigwa mpaka mwezi wa 10 hivi, ni mwendo wa bandika bandua,
Wa kusimamia lazima awe tff ambae ndio muwakilishi wa fifa.
Gharama za mwanzo lazima serikali itoe ambayo ndio imesema inataka kuanzisha ligi ya wazawq, ila baadae watafute wawekezaji...
Ila hii sio suluhu saana kama hawawekezi kwenye academies
 
Back
Top Bottom