Makonda: Mwakani tunaanzisha ligi ya wazawa tu!

Waziri wa michezo bwana Paul Makonda amesema kuwa kuanzia mwakani ataanzisha ligi ya wachezaji wa ndani tu kama ilivyokuwa michuano ya Afrika (CHAN) iliyohusisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika tu. Kwa kuwa michuano hii ya Afrika imefutwa rasmi na CAF, sasa ni wakati muafaka kuifufua kwa ngazi ya nchi. Kwa hiyo, michuano hii itaanza kupeperuka rasmi kuanzia msimu wa 2026/2027 ambapo ni wachezaji wa ndani tu watakaosajiliwa kushiriki ligi hii.

Kwa mujibu wa Makonda, lengo la kuanzisha michuano hii ni kuboresha kiwango cha mpira miongoni mwa wachezaji kutoka Tanzania na kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki. Hii itasaidia pia kuipandisha nchi kwenye viwango vya soka vya FIFA.

Bila kuwapotezea muda, hebu msikilize wewe mwenyewe kupitia link hii hapa chini:

MAONI YANGU
Namuunga mkono bwana Paul Makonda kwani ligi ya sasa imejaa ukiritimba na kusababisha wachezaji wa ndani kutoshiriki ipasavyo. Ligi mpya itahakikisha inashirikisha wachezaji hata kutoka huko mashinani, pasipo ubaguzi wowote. Utaratibu wa sasa wa kuruhusu timu kusajiri wachezaji wa kigeni 12 ni wa ovyo sana. Sikubaliani nao abadan. Nakubaliana na bwana Makonda (great thinker) kwa kuanzisha ligi ya wazawa haraka iwezekanavyo.
​
Upumbavu huo,mwambieni aache kukurupuka
 
Mkifanikiwa hata tu kuangalia hizi mechi za timu za kati mf. KMC vs Mtibwa, aisee ndo utajua kuwa Ligi yetu bila Wageni haiwezi kuwa na maana.

Yaani happ linapigwa kabum u tu, hamna ufundi wa mbinu.. mchawi nguvu, mbio na pumzi.. kuna muda ukiangalia unaweza sema "mbona hata mimi nikiamua kufanya mazoezi naweza kucheza"
 
Tatizo ni wachezaji wa kigeni ndio wanaturudisha nyuma. Siku tukianza ligi ya wazawa tupu, ubora wa wachezaji wazawa utapanda mkuu.
 
Waziri wa michezo bwana Paul Makonda amesema kuwa kuanzia mwakani ataanzisha ligi ya wachezaji wa ndani tu kama ilivyokuwa michuano ya Afrika (CHAN) iliyohusisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika tu. Kwa kuwa michuano hii ya Afrika imefutwa rasmi na CAF, sasa ni wakati muafaka kuifufua kwa ngazi ya nchi. Kwa hiyo, michuano hii itaanza kupeperuka rasmi kuanzia msimu wa 2026/2027 ambapo ni wachezaji wa ndani tu watakaosajiliwa kushiriki ligi hii.

Kwa mujibu wa Makonda, lengo la kuanzisha michuano hii ni kuboresha kiwango cha mpira miongoni mwa wachezaji kutoka Tanzania na kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki. Hii itasaidia pia kuipandisha nchi kwenye viwango vya soka vya FIFA.

Bila kuwapotezea muda, hebu msikilize wewe mwenyewe kupitia link hii hapa chini:

MAONI YANGU
Namuunga mkono bwana Paul Makonda kwani ligi ya sasa imejaa ukiritimba na kusababisha wachezaji wa ndani kutoshiriki ipasavyo. Ligi mpya itahakikisha inashirikisha wachezaji hata kutoka huko mashinani, pasipo ubaguzi wowote. Utaratibu wa sasa wa kuruhusu timu kusajiri wachezaji wa kigeni 12 ni wa ovyo sana. Sikubaliani nao abadan. Nakubaliana na bwana Makonda (great thinker) kwa kuanzisha ligi ya wazawa haraka iwezekanavyo.
​
Akili zakè zipo makalioni
 
Ni bora gharama za kuandaa hayo mashindano wangetumia kukarabati viwanja
 
Kuna mtu nilimsikia mtaani akasema omba sana usiwe na akili kama bashite sijui alikuwa anamaanisha nini hadi Leo?
Bashite ni great thinker; kila mtu anatamani kuwa kama yeye.
 
Ikishakuwa ligi maana yake ni msimu mzima iende. Mwezi wa ianzie mwezibwa 4 mwishoni ama wa 5 hivi, mwishoni mwa npl ikiwa imeisha na inapigwa mpaka mwezi wa 10 hivi, ni mwendo wa bandika bandua,
Wa kusimamia lazima awe tff ambae ndio muwakilishi wa fifa.
Gharama za mwanzo lazima serikali itoe ambayo ndio imesema inataka kuanzisha ligi ya wazawq, ila baadae watafute wawekezaji...
Ila hii sio suluhu saana kama hawawekezi kwenye academies
Sasa ikichezeshwa na hawa marefa feki wa TFF si ndio watazidi kuiharibu mkuu?
 
Mbona wapo kibao tu timu za bongo
Wapo lakini hawapati nafasi za kucheza kwa sababu ya mrundikano wa wachezaji wa kigeni. Ndio maana bwana Makonda kaanzisha ligi ya wazawa ili wote wapate nafasi ya kucheza.
 
Ligi kuu ina timu 16,siyo tatu(simba,yanga, Azam) hata hizo tatu akina mwanengo wanapata nafasi na tunaona madudu
 
Tatizo ni wachezaji wa kigeni ndio wanaturudisha nyuma. Siku tukianza ligi ya wazawa tupu, ubora wa wachezaji wazawa utapanda mkuu.
Mkuu; Wageni hutumika kuwachallenge wazawa, bila hivyo watazembea.

Timu ikijaa wazawa, tunarudi nyuma. Wachezaji wengi hawana Intelligency ya mpira.

Wao ni mbio na pumzi tu...

Nitajie mchezaji wa kizawa ambae leo tukimpeleka Timu ya taifa ya Senegal au Misri, atakaa hata bench...

Kaka, Hii ligi imesogezwa na Wageni. Hii ni fact.
 
Mkuu inaonekana bado hujajua dhima ya ligi ya wazawa. Dhima ya kwanza ni kuwapa nafasi wachezaji wazawa kucheza mpira. Hayo mengine yatafuata.
 
Back
Top Bottom