Makonda: Mwakani tunaanzisha ligi ya wazawa tu!

Makonda: Mwakani tunaanzisha ligi ya wazawa tu!

Nilichana kadi ya ccm miaka mingi sasa, sababu ya viongozi wenye akili kama za huyu bashite!
 
hakitatokea kitu kama hicho. Hao ni binadamu sio maroboti, mashindano mengi muda mchache,hao hao wachezaji wanahtajika wacheze NBC PL, CAFCL,CAFCC, CRDB FA CUP,MUUNGANO,MAPINDUZI, FIFA SERIES,KUFUZU CHAN,KUFUZU AFCON alafu tena eti wawe na ligi ya wachezaji wa ndani tena? Hii napinga kwa nguvu zote.
Wachezaji wataongezeka mkuu. Watakuwa wana rotate.
 
unadhani timu za kariakoo zitakuwa zinafanya rotations kwamba iwaache wachezaji wa ndani vinara iwaingize wale ndonyandonya ifungwe? We angalia tu hata sasa, timu gani ya kariakoo huwa inafanya rotations,na ikifanya hivyo matokeo yake ni yapi? Hili swala lazima lishirikishe timu na wadau wa michezo. Ulishaona wapi nchi ina ligi mbili?
Mkuu tusiandikie mate ilhali wino upo. Subiri mwakani uone ligi hii itakavyonoga.
 
Wazawa hawawezi kuimarika Kwa kuwaondelea ushindani kutoka Kwa foreigners
Feisali, Kapombe, Mudathir, Job, Bacca, Kagoma, Bado, Seleli,
Wamecheza mbele ya wageni wengi

England Kuna wachezaji wa kigeni wanatwanga pale ila haiwanyimi nafasi waingereza akina Saka, Palma, Maino, Belngham, n. K kuwa Bora

Hii Dunia Iko wazi inatakiwa wachezaji wetu wapambane wakacheze nje wanakotoka wageni

Samata anatwanga Le Havre pale France
Msuva, dismas, wanacheza nje vizuri tu

Kwaiyo Bashite ni lofa mmoja ropo ropo asiye na akili
Sasa wewe hutaki wachezaji wazawa wacheze mkuu?
 
Tatizo ni wachezaji wa kigeni ndio wanaturudisha nyuma. Siku tukianza ligi ya wazawa tupu, ubora wa wachezaji wazawa utapanda mkuu.
Utapandia wapi huo ubora?

Academies ndo suluhu la kudumu
 
Waziri wa michezo bwana Paul Makonda amesema kuwa kuanzia mwakani ataanzisha ligi ya wachezaji wa ndani tu kama ilivyokuwa michuano ya Afrika (CHAN) iliyohusisha wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika tu. Kwa kuwa michuano hii ya Afrika imefutwa rasmi na CAF, sasa ni wakati muafaka kuifufua kwa ngazi ya nchi. Kwa hiyo, michuano hii itaanza kupeperuka rasmi kuanzia msimu wa 2026/2027 ambapo ni wachezaji wa ndani tu watakaosajiliwa kushiriki ligi hii.

Kwa mujibu wa Makonda, lengo la kuanzisha michuano hii ni kuboresha kiwango cha mpira miongoni mwa wachezaji kutoka Tanzania na kuwawezesha watanzania wengi zaidi kushiriki. Hii itasaidia pia kuipandisha nchi kwenye viwango vya soka vya FIFA.

Bila kuwapotezea muda, hebu msikilize wewe mwenyewe kupitia link hii hapa chini:

MAONI YANGU
Namuunga mkono bwana Paul Makonda kwani ligi ya sasa imejaa ukiritimba na kusababisha wachezaji wa ndani kutoshiriki ipasavyo. Ligi mpya itahakikisha inashirikisha wachezaji hata kutoka huko mashinani, pasipo ubaguzi wowote. Utaratibu wa sasa wa kuruhusu timu kusajiri wachezaji wa kigeni 12 ni wa ovyo sana. Sikubaliani nao abadan. Nakubaliana na bwana Makonda (great thinker) kwa kuanzisha ligi ya wazawa haraka iwezekanavyo.
​
Wazo ni zuri lakini utekelezaji wake ni mgumu mno
 
Unapanda kwa mchezaji kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara mkuu.
Si kuna yale mashindano ya ndondo cup? Kuna wageni mule?

Ubora hupanda kwa kupata maarifa kwa wabobezi. Hakuna shortcut zaidi ya academies
 
Si kuna yale mashindano ya ndondo cup? Kuna wageni mule?

Ubora hupanda kwa kupata maarifa kwa wabobezi. Hakuna shortcut zaidi ya academies
Acadmies mbona zipo mkuu? Kila timu ya ligi kuu ina timu B, ambao ni zao la academies. Hii ligi mpya itakuja kuboresha zaidi.
 
haha unaacha kuwekeza kwenye mizizi unawawazia vijeba anyway unajua hawa jamaa wameona wasanii, wanasiasa, wachekeshaji, redio tv nk mmewachomolea betri kilichobaki ni mpira
Ndiyo sababu kawekwa hapo kimkakati oneni hii miaka 4 mpira unakavyotumika kama spinning tool yangu macho tu
Yanga chama langu nasikitika kukuacha ila sina budi
 
uyo ajui mpira kama wewe ingekua inamata lig ya uingereza spain italy germany wangefanya ivo lig ya uingereza imejza wagen kbao na team ya taif inafany vzur ya spain inawagen kbao ugerman pia na tim zao za nation znafnya vzur b4 wagen wazaw uwa hamna ktu ilawanapokuj ma pro wakigen ht wazaw uadopt mamb mazur na uchezaj kaa wagen inasaidia wazaw kuimalika
 
Back
Top Bottom