Makonda na Musiba, Magufuli hayupo. Je, mmejiandaa kisaikolojia?

Makonda na Musiba, Magufuli hayupo. Je, mmejiandaa kisaikolojia?

Kifo cha rais John Pombe Maguli ni pigo kubwa kwa taifa na Afrika kwa ujumla. Ni rais ambaye amejijengea sifa, maadui hata marafiki. Tanzania, bila unafiki wala kificho itamkumbuka baada ya mwanzilishi wake Mwl Julius Nyerere.

Alikuwa mkweli na muwazi ingawa maradhi yake yalizungukwa na kificho bila sababu ya msingi kana kwamba hakuwa binadamu wa kawaida. Hata hivyo, wakati tukiomboleza, kuna watu saa hizi hawamuombolezi kwa vile wanampenda bali maisha yao yatakuwa hatarini tokana na kujipendekeza kwao wakidhani wangefanikiwa kumtumia.

Ndoto ya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi pia imo mashakani. Si vizuri kuongelea urithi wakati hata marehemu hajazikwa. Hata hivyo, urais si mali binafsi, lazima tuanze kufikiri mbele.

Wakati tukifanya hivyo, kuna watu watajuta kuzaliwa na wengine hasa mafisadi waliofichwa mahabusu wanasherehekea na wale waliosaidiwa wanasaga meno. Kati ya hao Daudi Bashite aka Makonda na Msiba Musiba watakuwa na hali ngumu.

Haya ni mawazo yangu kama baba yenu.

RIP JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI. YOU INDEED WAS OPEN AND TRUSTWORTHY FOR YOUR NATION AND PEOPLE.

Mpaka Chalamila wa Mbeya
 
Mi nashauri Mh. Samia amtafute makamu wake ambaye ni mchumi mmbobezi ambaye amtamsaidia kuurudisha uchumi kwenye mstari, lakini mtu mwenye ufahamu wa diplomasia vizuri itamsaidia pia kuurudisha mahusiano na nchi marafiki na mwisho mtu walau mwenye uzoefu wa shughuli za serikali.

Possible candidates include former CAG, former Katibu mkuu kiiongozi Sefue,

Proffesor Mkenda, Mizengo Linda.

Mheshimiwa aepuke kutea makada ambao wanaweka chama mbele na sio taifa
Kwanza kabisa anatakiwa abadili uongozi wote, kuanzia mawaziri, na watendaji wote, aachane na walamba viatu, mapof njaa. Aondoe ule ubaguzi wa kanda. Mama naamini anajua hayo
 
Miradi ya kule kwetu hasa Chato msahau kabisaaaaa.
Kumbuka huyu mama kwao hakufanya mambo ya kijinga kama walivyofanya Chato na huko kwa PM
Wabongo bana,hivi unadhani mama samia atabadilisha chochote?,tegemeeni vurugu nyingi zaidi,afadhali magu alikuwa anawadhibiti hao MATAGA,Kwa huyu mama ndio watakuja na nguvu like never before
Kingine miradi ,msitegemee kuna mradi utalala,yote hii itaendelezwa,magufuli alikuwa mjanja sana,mwisho huyu mama ulikuwa humwambii kitu kwa magu,utegemee tofauti?,thubutu,yaani ikulu Dodoma isimalizwe??,utaniambia ni muda tu..
 
Kifo cha rais John Pombe Maguli ni pigo kubwa kwa taifa na Afrika kwa ujumla. Ni rais ambaye amejijengea sifa, maadui hata marafiki. Tanzania, bila unafiki wala kificho itamkumbuka baada ya mwanzilishi wake Mwl Julius Nyerere.

Alikuwa mkweli na muwazi ingawa maradhi yake yalizungukwa na kificho bila sababu ya msingi kana kwamba hakuwa binadamu wa kawaida. Hata hivyo, wakati tukiomboleza, kuna watu saa hizi hawamuombolezi kwa vile wanampenda bali maisha yao uyatakuwa hatarini tokana na kujipendekeza kwao wakidhani wangefanikiwa kumtumia.

Ndoto ya Dodoma kuwa makao makuu ya nchi pia imo mashakani. Si vizuri kuongelea urithi wakati hata marehemu hajazikwa. Hata hivyo, urais si mali binafsi, lazima tuanze kufikiri mbele.

Wakati tukifanya hivyo, kuna watu watajuta kuzaliwa na wengine hasa mafisadi waliofichwa mahabusu wanasherehekea na wale waliosaidiwa wanasaga meno. Kati ya hao Daudi Bashite aka Makonda na Msiba Musiba watakuwa na hali ngumu.

Haya ni mawazo yangu kama baba yenu.

RIP JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI. YOU INDEED WAS OPEN AND TRUSTWORTHY FOR YOUR NATION AND PEOPLE.
Umenikumbusha watu wasiojulikana, sijuii wataendelea kuwepo ama ndiyo wameshatengenezwa
 
Back
Top Bottom