Makonda ni nani hasa kwenye Siasa za Tanzania? Kwanini nguvu kubwa inatumika kumrejesha ulingoni?

Anonymous

Senior Member
Joined
Apr 6, 2006
Posts
118
Reaction score
339
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM anatarajiwa kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini tetesi za mambo yanayoelezwa kuendelea ili kumpokea yanatia aibu, kutia hasira na kufedhehesha sana.

Inadaiwa Mkuu wa Wilaya ya Chato ameziamuru Taasisi zote za Kiserikali Wilayani mwake kutoa shilingi 500,000/- kila mmoja kwaajili ya maandalizi ya kumpokea Makonda.

Kama hiyo haitoshi Taaasisi hizo zinadiwa kupewa maelekezo ya kwenda katika mpaka wa Chato na Bukoba ili kumpokea Mwenezi huyo

Ujinga huu unafanywa kuhujumu mali za umma maana Makonda hausiki kabisa na mali za umma bali za chama chake, kuchukua fedha kwenye taasisi za Umma na kisha kutumia gharama zisizo za msingi kupeleka magari eti kumpokea ni UJINGA uliopiliza

Hawa watu wanatakiwa kujua Watanzania sio wajinga na bado nchi ina shida lukuki za kimaendeleo
 
Kura za Kanda ya ziwa, na kuwavuta wafuasi wa jiwe ambao bado wamelala matanga, Kanda ya ziwa Ina wapiga kura wengi
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM anatarajiwa kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini tetesi za mambo yanayoelezwa kuendelea ili kumpokea yanatia aibu, kutia hasira na kufedhehesha sana...

Chama Makini na Madhubuti, huzaa Serikali Madhubuti, Mahiri na Imara zaidi.
Serikali ya CCM ni Mathubuti sana...

Hiyo ni mwanzo tu wa kutoa mrejesho kwa Wananchi juu ya kilichofanywa na serikali tangu iingie Madarakani....

Chama legelege huzaa Serikali legelege....
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM anatarajiwa kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini tetesi za mambo yanayoelezwa kuendelea ili kumpokea yanatia aibu, kutia hasira na kufedhehesha sana...
CCM wanatafuta jitu lisilojali la kucheza rafu 2024-25 na kulitupia lawama zote huku jitu hilo likilindwa kwa fedha za watanzania.
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM anatarajiwa kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini tetesi za mambo yanayoelezwa kuendelea ili kumpokea yanatia aibu, kutia hasira na kufedhehesha sana...
Wanalazimisha kurudisha upepo wa Magufuli kanda ya ziwa kwa lazima
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM anatarajiwa kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini tetesi za mambo yanayoelezwa kuendelea ili kumpokea yanatia aibu, kutia hasira na kufedhehesha sana.

Inadaiwa Mkuu wa Wilaya ya Chato ameziamuru Taasisi zote za Kiserikali Wilayani mwake kutoa shilingi 500,000/- kila mmoja kwaajili ya maandalizi ya kumpokea Makonda.

Kama hiyo haitoshi Taaasisi hizo zinadiwa kupewa maelekezo ya kwenda katika mpaka wa Chato na Bukoba ili kumpokea Mwenezi huyo

Ujinga huu unafanywa kuhujumu mali za umma maana Makonda hausiki kabisa na mali za umma bali za chama chake, kuchukua fedha kwenye taasisi za Umma na kisha kutumia gharama zisizo za msingi kupeleka magari eti kumpokea ni UJINGA uliopiliza

Hawa watu wanatakiwa kujua Watanzania sio wajinga na bado nchi ina shida lukuki za kimaendeleo
Watu washajua nyuma ya Makonda kuna nguvu kubwa sana ya Chama na Dola!! Ukileta jeuri utakula jeuri yako!! Ya nini yote hayo? Watanzania wana akili sana, wanasema mtumikie kafiri upate mradi wako! Mwulize Nape Nauye yaliyompata baada ya kujifanya jeuri na kuamua kupambana na Makonda!! Ujue kimsingi ni awamu hiyo hiyo ndiyo bado iko madarakani!! Makonda ni "punda" tu kabebeshwa mzigo kuhakikisha unapitishwa 2025 salama!! Sasa wewe lete jeuri yako uone yatakayokupata!! Jina linaweza lisirudi kwenye mchakato wa 2025, sasa nani ana ubavu huo? Ninaamini kabisa Nape hawezi kurudia makosa hayo!!
 
Acha uzwazwa.

Huyu ni msemaji wa chama,

Hayo ni maagizo ya CCM kwa mawaziri KUPITIA msemaji wake
 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM anatarajiwa kufanya ziara mikoa ya Kanda ya Ziwa lakini tetesi za mambo yanayoelezwa kuendelea ili kumpokea yanatia aibu, kutia hasira na kufedhehesha sana.

Inadaiwa Mkuu wa Wilaya ya Chato ameziamuru Taasisi zote za Kiserikali Wilayani mwake kutoa shilingi 500,000/- kila mmoja kwaajili ya maandalizi ya kumpokea Makonda.

Kama hiyo haitoshi Taaasisi hizo zinadiwa kupewa maelekezo ya kwenda katika mpaka wa Chato na Bukoba ili kumpokea Mwenezi huyo

Ujinga huu unafanywa kuhujumu mali za umma maana Makonda hausiki kabisa na mali za umma bali za chama chake, kuchukua fedha kwenye taasisi za Umma na kisha kutumia gharama zisizo za msingi kupeleka magari eti kumpokea ni UJINGA uliopiliza

Hawa watu wanatakiwa kujua Watanzania sio wajinga na bado nchi ina shida lukuki za kimaendeleo
Makonda ni mtoto pendwa wa kanda ya ziwa, tushapiga hesabu (kwa mujibu wa sensa) tushafanya tathmini hiyo kanda hawamkubali bimkubwa so kwenye sanduku lijalo tunatumia karata ya naibu PM na huyu dogo. Mmeshaelewa sasa?
 
Kura za Kanda ya ziwa, na kuwavuta wafuasi wa jiwe ambao bado wamelala matanga, Kanda ya ziwa Ina wapiga kura wengi
Uchaguzi ujao bila ya karata ya JPM itakuwa ngumu sana. Walijaribu kumbomoa ili asahaulike, ili isihitajike kumtaja, sanduku hilo hapo na bado ana nguvu. Niwaambie, JNHPP imewekwa kuifungua 2024 mwishoni pamoja na SGR. Impact ni kubwa
 
C
Wanalazimisha kurudisha upepo wa Magufuli kanda ya ziwa kwa lazima
CDM walishindwa kwenye ziara zao kutumia kete ya Magufuli kanda ya ziwa wakaishia kumkandia mwanzo mwisho bila kusoma upepo wa siasa wenzao wanatumia vyema kete hiyo
 
Na bado hamjasema,, Makonda anaufyekelea mbali mtandao wa Sacco's ya kaskazini,, mapovu yanavyowatoka sasa,, karibu nyumbani kijana shikilia hapohapo hadi waseme,,
[/QUOTE

Huo ni ujinga uliosapoti hapo, tuna taka Kuona mafisadi, yanashughurikiwa, hao unahangaika nao hawwana serikali.
 
Inadaiwa Mkuu wa Wilaya ya Chato ameziamuru Taasisi zote za Kiserikali Wilayani mwake kutoa shilingi 500,000/- kila mmoja kwaajili ya maandalizi ya kumpokea Makonda.
Kuchanga shilingi laki 5 ili kumpokea mwizi, mtekaji na mpiga watu risasi inahitaji moyo sana.

Akifika hapo Chato atoe maelezo ni lini atarejesha nyumba ya GSM qliyoipora.
 
Na bado hamjasema,, Makonda anaufyekelea mbali mtandao wa Sacco's ya kaskazini,, mapovu yanavyowatoka sasa,, karibu nyumbani kijana shikilia hapohapo hadi waseme,,
Muda ni mwalimu mzuri...
 
Biteko na Bashite ni mkakati wa kinafki kujiandaa na 2025 kuwaonyesha watu wa kanda ya ziwa kuwa tuko pamoja ndani ya chama.
 
Back
Top Bottom