Makonda: Rais Samia alilibeba jina langu na kuingia nalo Kamati Kuu bila kujali kelele za chura akiamini nitamsaidia kazi. Viongozi wa Dini mniombee!

Hhaa chura wa ufipa wabugia Sembe watakurukia sana
 
Hakupaswa kuyasema haya hadharani kwani ni kumvunjia heshima ya usiri wa uongozi Kwa mwenyekiti wake , afungwe kizibiti maneno mapema kabla hajaweka mapengo makubwa miongoni mwa wanachama.
Hivi Makonda ameshindwa elezea mafanikio ya chama katika kukuza uchumi, upatikanaji wa Nishati Kwa unafuu na iliyo Bora, Ujenzi wa miundombinu , Huduma Bora za afya , uimara wa ulinzi na usalama wa nchi na mengineyo . Akishtuka na kuitumia vizuri nafasi aliyopewa Kwa awamu hii atakuwa hazina nzuri na funzo Kwa mabadiliko ya vijana kutokana na maono ya watawala.
 
Wangemwachia tu huru yule Binti aliyeimba wanatuona manyani,kumbe wanatuona Chura tu
 
Matusi makubwa sana kwa wana CCM, yaani katika CCM yote wakiwepo wabunge,mawaziri,Wakuu wa mikoa na Wilaya na kada zote wameshindwa kumsaidia Rais ila Paul Makonda pekee ndiye mwenye uwezo huo. Kwani yeye na Rais wana siri gani hiyo ??????
 
Kwa hiyo viongozi wengine na wajumbe wa kamati kuu anawaita VYURA?
Kweli jamaa anadharau sana kwa vile anabebwa na Samia. Hii hadi inatuogopesha what's behind the scene?
 
Keshaanza kufunguka... Na bado hajasema ... Atasema tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…