Makonda: Rais Samia alilibeba jina langu na kuingia nalo Kamati Kuu bila kujali kelele za chura akiamini nitamsaidia kazi. Viongozi wa Dini mniombee!

Makonda: Rais Samia alilibeba jina langu na kuingia nalo Kamati Kuu bila kujali kelele za chura akiamini nitamsaidia kazi. Viongozi wa Dini mniombee!

"Rais Samia alilibeba jina langu na kuingia nalo Kamati Kuu bila kujali kelele za chura akiamini nitamsaidia kazi," amesema Komredi Makonda.

Kashaanza tena kuharibu...mzee wa kubebwa
 
Ama kwa hakika leo nime enjoy sana wala sijaumia bando.nime enjoy kuona wenye kero wakiitwa na kupewa majibu hapo kwa hapo.hio ndio michakato hat sis bawaacha tunapenda sana.
Majibu ya hapo kwa hapo huwa ni sinema tu mara nyingi za kuwalainisha watu.
 
Mwenezi wa CCM Komredi Makonda amewaomba Viongozi wa Dini wazidi kumuombea ili mosi, amuheshimishe Mungu wa Mbinguni na pili, atimize majukumu ambayo Rais Samia anaamini atamsaidia.

"Rais Samia alilibeba jina langu na kuingia nalo Kamati Kuu bila kujali kelele za chura akiamini nitamsaidia kazi," amesema Komredi Makonda.

Jambo TV

Sijui huyu bwana na makeke aliyoingia nayo kama atadumu hata miezi sita, tutaona, labda mama amkanye vinginevyo atarudi mitaani tu huyu!
 
Anayoyaongea yana baraka ya mama said, kuanzia wastaafu wenye muwasho hadi hili kama jina lilibebwa na mama said kwenda kamati kuu.
 
Matusi makubwa sana kwa wana CCM, yaani katika CCM yote wakiwepo wabunge,mawaziri,Wakuu wa mikoa na Wilaya na kada zote wameshindwa kumsaidia Rais ila Paul Makonda pekee ndiye mwenye uwezo huo. Kwani yeye na Rais wana siri gani hiyo ??????

Acha Nongwa.
 
Kwahiyo anamaanisha huko kamati kuu wamejazana Vyura ukimtoa Mwenyeki?
 
Makonda apige kazi sisi mashabiki zake tunataka awe mstaarabu wa kweli na aongee vema
 
Makonda amesema kwamba ndani ya CCM Kuna chura, na kwamba chura hao humpigia kelele Mwenyekiti wa CCM, ninavyojua viongozi waandamizi wa CCM ni Kinana, Dk Mwingi, na Chongolo, je hao ndio wanampigia kelele Samia?
 
Mkuu acha mvua inyeshe ili tupaone panapovuja. Mamlaka ya uteuzi naona ilipima "strengs vs weaknesses" zake na hatimaye kujiridhisha anakidhi viwango vyote vya kuwa ni "asset" ndani ya chama kupitia nafasi aliyopewa.

Hayo mengine kuhusu kuwa ni "liability" kwa chama chake muda utaamua. Chama kimemuamini katika nafasi aliyokabidhiwa, natambua hatafanana kiutendaji na watangulizi wake katika nafasi hiyo.

Vijembe, matendo, na kauli zake hizi zinaashiria ana maelekezo maalumu kutoka kwa bosi wake. Acha mvua inyeshe tuone sehemu inapovuja kupitia utendaji wake.
 
Makonda amesema kwamba ndani ya CCM Kuna chura, na kwamba chura hao humpigia kelele Mwenyekiti wa CCM, ninavyojua viongozi waandamizi wa CCM ni Kinana, Dk Mwingi, na Chongolo, je hao ndio wanampigia kelele Samia?
Watajuta kumpa mhuni chama atawavuluga.
 
Makonda anajua anafanya nini!pia ccm ilipoa sana na uchagvzi umekaribia mpeni muda tu!
 
Back
Top Bottom