Usidanganywe, hao walio ndani ya serikali wanaelewa kelele za Makonda ni mradi wa mama kurejesha matumaini ya chama bila kujua ana angushwa yeye.
Unadhani ma DED, DC na RC huko apitapo huyo wana hofu na maigizo hayo?
Utahofu nini wakati mfumo huo wa upigaji umeanzia juu kuja chini tena bila uficho?
Wananchi wanashangilia kubwabwaja kwa Bashite kwa vile hawajui mateso yao hayajaanzia kwa hao viongozi wao wa chini bali yameanzia juu.
Hivi kelele za Makonda umeona zimempeleka nani mahakamani? Ni mikutano ya hadhara na vyombo vya habari kutangaza sana kisha akiondoka business as usual.
Sasa ni hoja ya kupewa sumu. Nani anampa sumu? Au anatangaza kuwa wale wauaji wenzake ndani ya Chama ndio wanaweka sumu kwenye chakula? Kwa vile kawajua jee hatua zimechukuliwa?
Sent from my SM-A125F using
JamiiForums mobile app