Bahenga walisema sikio la kufa halisikii dawa. Mwenezi unadai kuna watu wanataka kukuua. Tena si upinzani Bali ni CCM. Unakichafua chama chako mwenyewe kuwa na wauaji
Sasa nakutonya, uko kwenye mtego ndio maana kwenye maadhimisho ya miaka 47 hukusikia kiongozi mwengine ngazi ya Taifa akiongea zaidi ya Kinana.
Ni hivi, umeachwa uzunguke mikoa yote tena shangaa walivyokuongezea posho ghafla. Umetegwa ukimaliza mikoa yote then utafanya nini? Kwishney, hapo ndipo wakubwa zako wataanza kukunanga na wewe. Kwa Sasa wanakucheka sana.
Wewe ni jiwe linaloandaliwa kuwa chanzo cha ajali ya kisiasa kwa Rais Samia Suluhu Hassan 2025. Endelea kuzunguka huku wakimzunguka mama. Wewe na Samia mtapoteana muda si mrefu. Chukua hiyo!