Sikatai, ni kweli hiyo migahawana bar zipo zinazofanya vizuri kwenye usafi LAKINI NI MICHACHE SANA YAANI NI KAMA ILIVYO IDADI YA WANAWAKE WENYE DIMPLES NA MWANYA.Shida siyo kushikwa kwa mkono, mikono inayoshikwa mkono maana, mtu alieshika wakati wa kuandaa alinawa kwanza mikono, maana wakati wa kuanda vyakula vingi, ni ngumu kuto shika kwa mkono. Mchele mtu atachagua kwa mkono, mchicha utakatwa kutumia mkono, nyama ya mchuzi vipande hukatwa kushikwa kwa mkono tena toka buchani.
Maji tililika huwezi kwenda migahawa, na bar ya maana ukakosa maji tililika kama kama ni mkazi wa Dar nenda hata pale kwenye mgawa unaotazamana na mlimani city uone tofauti na huko unakokula, nenda hata mgahawa high way manzese muhudumu hashiki kijiko kitakacho tumika na mteja kwa mkono, na kinawekwa kwenye maji ya moto, sehemu za kunawia zipo maji tililika. Sema, kuna watu tumeumbwa kubisha.
Ninachokushangaa unaonekana unabeza hoja yangu wakati lengo langu ni kufahamishana ili watu wachukue tahadhari na wadau wa hiyo biashara nao wazingatie usafi. Sielewi ni kwanini unakuwa NEGATIVE KIASI HICHO.