Makosa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili, kwanini yanashamiri?

Naamini 'ga' mwishoni mwa kitenzi yamaanisha kitendekacho mara kwa mara.
 
Ila kosa kubwa ambalo limeota mizizi na juzi nimeliona gazeti moja limetumia ni uridhi badala ya urithi;matumizi ya dhi na thi ni janga la kitaifa
Kwenye magazeti ndio huwa inanisikitisha maana utasema hawana wahariri yaani na matumizi ya lugha za mtaani kwenye shughuli za serikali nayo imeshamiri...kuchomekea kwenye speech ama mazungumzo hakuna shida, shida inakuja pale yale maneno ya mtaani yanayochomekewa kwenye mazungumzo alafu unayakuta kwenye taarifa ya kimaandishi mfano "fyekelea mbali" kwenye taarifa rasmi ya Ikulu iliandikwa kama lugha rasmi vile
 
Kuchanganya 'dh' na 'th' utaona

Kudhibitisha au dhamani.

Ujinga mwingine ni kuyaongezea konsonati majina ya kibantu.
Mfano Lissu badala ya Lisu, Zitto badala ya Zito, Kigwangalla badala ya Kigwangala wajinga.
Kessy na Mchaky vipi?
 
Kwenye aya ya mwisho ulipaswa kuandika uandishi na sio uhandishi.
Vinginevyo umefafanua vizuri sana.
 
2
Kuchanganya 'dh' na 'th' utaona

Kudhibitisha au dhamani.

Ujinga mwingine ni kuyaongezea konsonati majina ya kibantu.
Mfano Lissu badala ya Lisu, Zitto badala ya Zito, Kigwangalla badala ya Kigwangala wajinga.
2o8 = tuonane
 
Hivi uhandishi unamaanisha ndiyo nini ?
 
Awez badala ya Hawezi
Ujaacha badala ya Hujaacha
Uendelei badala ya Huendelei

mkuu ni kweli, yaani hiyo kuacha 'h' huwa mpaka nachukia nikiona msg ya namna hiyo. Nimejaribu sana kurekebisha walio karibu nami lakini naona imekuwa ngumu kweli.
 
Kweli kabisa Mzee kifimbocheza.

Hayo pia yanaiharibu lugha yetu.
Pia kuna vijimaneno vya wanawake lakini cha ajabu waweza kukuta mtoto wa kiume anayatumia.
1.Jomon
2.kudamshi

hahahaa bilashaka ulimaanishi maneno kama haya
 
Lazima ujue kutofautisha swaga na andishi rasmi.
Makosa hayo ukiyakuta kwenye kitabu au gazeti huko ndo unaweza kupima ukubwa wa tatizo

Kuna mtu anachanganya r na l au 'a' na 'h', hii si swaga tena bali ni ulemavu katika uandishi. Iwe ni mawasiliano yasiyo rasmi au la, inakera

Kwa kweli nikikutana na kitabu kina shida hizo mbili hapo juu nakitupa...potelea mbali ujumbe uliomo na hela niliyopoteza
Kuna kipindi gazeti la mwananchi lilikuwa na shida hiyo, sijui hakuwa na mhariri.

Na hakuna watu wabishi kama hao walemavu, ukiwakosoa ni ligi
 
Tusisahau pia neno saa linapotamkwa au kuandikwa kwa wingi kwamba masaa! Hapa utakuta hata Waandishi wa Habari wakisema "Waziri Mkuu alihutubia kwa masaa matatu!

Hili neno" masaa " badala ya" saa " nikijaribu kumuelekeza mtu kwa mfano, Dar es salaam kwenda Morogoro ni mwendo wa" saa " 4. Mtu hakuelewi hadi utumie" masaa"4.
 
Kuna watanzania wengi sasa hivi wanasema "nyimbo ya" badala ya "wimbo wa". Mpaka watangazaji kwenye maredio, yaani imekuwa ni kama kawaida kusema hivyo wakati ni makosa.
 
hizo ni slang mkuu. kuna lugha rasmi, kuna lugha ya mtaani na kwa sasa mitandao ya kijamii imekuja na utamaduni wake wa jinsi ya kuwasiliana. kuna wakati ukisoma ujumbe mfupi wa simu unaweza usielewe utadhani kilichoandikwa si Kiswahili.
Mkuu, unajua maana ya slang?
 
Kuchanganya 'dh' na 'th' utaona

Kudhibitisha au dhamani.

Ujinga mwingine ni kuyaongezea konsonati majina ya kibantu.
Mfano Lissu badala ya Lisu, Zitto badala ya Zito, Kigwangalla badala ya Kigwangala wajinga.
hapa wao wenye majina haya ndio wamejiongezea
 
Sentensi ipi hapa ni sahihi.

1) Na kula Bia

2)Nakunywa Bia

Nimeona na kusikia wengi wa wasanii hasa Wa muziki Wa kitumia hiyo Namba moja.
 
Mkuu Chige ninaomba msaada wako kuna jamaa yangu mfaransa anajifunza kiswahili. Huwa ananiuliza maswali ya kiufundi nyakati nyingine, ambayo kimsingi ni nje ya taaluma yangu.

Nimeona kwa uchangiaji wako, nikahisi waweza kuwa ni wa msaada. Nina c&p ujumbe chini wa swali husika la huyo mgeni:

Rafiki, I have a question

There is a sentence:
Wanawake niliowaona ni wazuri.
Is that correct?

Siwezi kufaham kwa nini kuna -wa- ndani ya "verb".
There is the relative -o- and I can get that (The women THAT I saw...), but why the repetition of "women" in -wa-?

Why should we repeat the relative -o- and the object -wa- (wanawake)?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…