Makosa katika maandishi ya lugha ya Kiswahili, kwanini yanashamiri?

Kuna watanzania wengi sasa hivi wanasema "nyimbo ya" badala ya "wimbo wa". Mpaka watangazaji kwenye maredio, yaani imekuwa ni kama kawaida kusema hivyo wakati ni makosa.
Huwa nikisikia tu "nyimbo yangu" hata kama angekuwa anajieleza nani, maelezo yote hata yawe mazuri vipi nalazimika kuyasahau.

Sijui walimu wao walikuwa wanawafundishi huu ujinga?
 
Nayaona sana haya makosa kwenye maandiko ya wasanii wetu nyota kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii

Mwanzo nilidhani kiwango cha elimu ya sasa ndiyo chanzo cha makosa ya kiuandishi kuzidi ila nayaona hadi kwa wasanii wakongwe waliopata elimu ya zamani
 
Kuna watanzania wengi sasa hivi wanasema "nyimbo ya" badala ya "wimbo wa". Mpaka watangazaji kwenye maredio, yaani imekuwa ni kama kawaida kusema hivyo wakati ni makosa.
Wengine wanakwenda mbali zaidi kwa kusema ' mwimbo' badala ya wimbo.
 
Hapana kuna makabila hayana matumizi kwa baadi ya herufi mfano wa herufi hizo ni
R
L
Kuna yale ambayo irabu huzitamka kama consonant H mfano wakerewe lakini kuna mengine hayana hizi dh na th hivyo yanatumia z
Hivyo makosa mengine ya matumizi ya herufi yanachangiwa na lugha mama na siyo mwandishi kutokujua.
 
Hiyo sentensi kaichambua kama sentensi za kiingereza ndiyo maana amejikuta anaona kuna makosa.
Ila ukiangalia viambishi vyote katika sentensi hiyo vinajitosheleza na kuipa sentensi maana.
 
Hiyo sentensi kaichambua kama sentensi za kiingereza ndiyo maana amejikuta anaona kuna makosa.
Ila ukiangalia viambishi vyote katika sentensi hiyo vinajitosheleza na kuipa sentensi maana.
Na hicho nilitaka kuongea kabla lakini nikachelea kusema wazi wazi wakati sina utaalamu huo!
 
Kwenye kuongea, watu kama hawa wanavumilika manake unajua kabisa ni athari za makabila yao! Lakini wanaposhindwa hata kuadika!!!

(Mahali) ninakoenda ni mbali sana, halafu unaandika mahari ninakoenda ni mbari sana kwa sababu tu, labda ni Mkurya! Hapana kwa kweli.. mambo mengine nahisi ni kama tunajiendekeza tu!
 
Nikweli mkuu upo sahihi lakini niliyoeleza pia ni moja kati ya sababu nyingi zinazochangia hili tatizo
 
Mengine ni kama: nimefulai badala ya nimefurahi, vifua mbere badala ya vifua mbele, Daslam badala ya Dar es Salaam nk
 
Kuna watanzania wengi sasa hivi wanasema "nyimbo ya" badala ya "wimbo wa". Mpaka watangazaji kwenye maredio, yaani imekuwa ni kama kawaida kusema hivyo wakati ni makosa.
Hata wewe sasa hapo kwenye maredio , hatuna neno hilo. Haya mambo ya umoja na uwingi lazima uwe makini kwenye maneno kama sufuria......, mbwa......, jiko....... na hapo uwingi wa jiko ni nini? (sidhani kama litakuacha salama neno hilo)
 
Jiko= meko
 
Mkuu lengo kuu la kuwa na lugha ni kisaidia mawasiliano.
Kwahio basi as long as tukiongea tunaelewana basi hio lugha ni sahihi.

Sisi ni binadamu kwahio kamusi zinatakiwa kutufwata sisi na sio sisi kuzifwata kamusi..
Utakua unamaanisha neno 'my'
mai
 
Onyo-maonyesho
Ona-maonesho.
Kwa upande wa kibiashara ni maonesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…